Nokia 225 4G User guide [sw]

Mwongozo wa mtumiaji
Toleo 2021-01-04 sw
Mwongozo wa mtumiaji
1 Kuhusu mwongozo huu wa mtumiaji
Muhimu: Kwa maelezo muhimu kuhusu matumizi salama ya kifaa na betri yako, soma maelezo
ya ”Kwa usalama wako” na ”Usalama wa Bidhaa” katika mwongozo uliochapishwa wa mtumiaji, au kwenye www.nokia.com/support kabla utumie kifaa. Ili kujua jinsi ya kuanza kutumia kifaa chako kipya, soma mwongozo uliochapishwa wa mtumiaji.
Mwongozo wa mtumiaji

Yaliyomo

1 Kuhusu mwongozo huu wa mtumiaji 2
2 Yaliyomo 3
3 Anza kutumia 5
Vitufe na sehemu . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . 5
Sanidi na uwashe simu yako . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . 6
Chaji simu yako . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . 9
Vitufe . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . 9
4 Simu, majina, na ujumbe 11
Simu . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . 11
Majina . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . 11
Tuma ujumbe . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . 12
5 Binafsisha simu yako 13
Badilisha toni . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . 13
Badilisha mwonekano wa skrini yako ya mwanzo . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . 13
Pata mengi kutoka kwa SIM kadi mbili . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . 13
6 Kamera 14
Picha na video . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . 14
7 Intaneti na miunganisho 15
Vinjari wavuti . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . 15
Bluetooth® . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . 15
8 Muziki 16
Kicheza muziki . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . 16
Sikiliza redio . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . 16
Mwongozo wa mtumiaji
9 Saa, kalenda, na kikokotoo 17
Weka saa na tarehe wewe mwenyewe . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . 17
Saa ya kengele . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . 17
Kalenda . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . 17
Kikokotoo . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . 17
10 Safisha simu yako 19
Ondoa maudhui binafsi kwenye simu yako . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . 19
11 Maelezo ya bidhaa na usalama 20
Kwa usalama wako . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . 20
Simu za dharura . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . 22
Kuhudumia kifaa chako . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . 23
Uchakataji upya . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . 24
Alama ya pipa iliyo na mkato . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . 24
Maelezo ya betri na chaja . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . 24
Watoto wadogo . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . 25
Vifaa vya matibabu . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . 25
Vifaa vya matibabu vinavyopachikwa . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . 25
Vifaa vya kusaidia kusikia . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . 26
Linda kifaa chako dhidi ya maudhui mabaya . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . 26
Magari . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . 26
Mazingira yanayoweza kulipuka . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . 26
Habari ya utoaji cheti (SAR) . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . 27
Kuhusu Usimamizi wa haki za Dijitali . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . 28
Hakimiliki na ilani nyingine . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . 28
Mwongozo wa mtumiaji
3 Anza kutumia

VITUFE NA SEHEMU

Simu yako
Mwongozo huu wa mtumiaji unatumika kwa modeli zifuatazo: TA-1276, TA-1296, TA-1279, TA­1289, TA-1282, TA-1316, TA-1321.
1. Kitufe cha kutembeza
2. Kitufe cha kupiga simu
3. Kitufe cha uchaguzi cha kushoto
4. Kifaa cha masikio
5. Kiunganisha vifaa vya kichwa
6. Mweko
7. Kitufe cha uchaguzi cha kulia
8. Kitufe cha nishati/kukata simu
9. Kipaza sauti
10. Kamera
11. Kipenyo cha kufungua kifuniko cha nyuma
12. Kiunganisha USB
Mwongozo wa mtumiaji
Jiepushe kugusa eneo la antena bila sababu wakati antena inatumika. Unganisha na antena huathiri ubora wa mawasiliano na unaweza kupunguza maisha ya betri kwa sababu ya kiwango cha juu zaidi cha nishati wakati wa uendeshaji.
Usiunganishe kwenye bidhaa ambazo zinaunda ishara ya kutoa, kwa kuwa hii inaweza kuharibu kifaa. Usiunganishe chanzo chochote cha stima kwenye kiunganisha cha sauti. Ukiunganisha kifaa chochote cha nje au kifaa chochote cha kichwa kando na zile zilizoidhinishwa kutumiwa na kifaa hiki, Kiunganishi cha sauti, kuwa makini sana na viwango vya sauti. Sehemu nyingine za kifaa hiki zina sumaku. Vitu vya chuma vinaweza kuvutwa na kifaa. Usiweke kadi za karadha au vitu vingine vyenye kutumia hifadhi ya sumaku karibu na kifaa hiki, kwa sababu maelezo yaliyohifadhiwa kwenye vitu hivyo yanaweza kufutika.
Baadhi ya vifaa vya ziada vilivyotajwa katika mwongozo huu wa mtumiaji, kama vile chaja, kifaa cha kichwani, au kebo ya data, huenda vikauzwa kando.
Dokezo: Unweza kuweka simu yako kuulizia msimbo wa usalama ili kulinda faragha na data yako ya kibinafsi. Chagua Menyu > > Usalama > Kilinda vitufe > Msimbo wa usalama . Hata hivyo kumbuka, kwamba unahitaji kukumbuka msimbo, kwa kuwa HMD Global haiwezi kuufungua au kuuruka.

SANIDI NA UWASHE SIMU YAKO

Nano-SIM
Muhimu: Kifaa hiki kimeundwa ili kutumiwa na SIM kadi ya nano pekee (angalia mfano).
Matumizi ya kadi zisizotangamana za SIM zinaweza kuharibu kadi au kifaa, na zinaweza kuharibu data iliyohifadhiwa kwenye kadi.
Kumbuka: Zima kifaa na usiiunganishe na chaja au kifaa kingine chochote kabla ya kubandua vifuniko vyovyote. Epuka kugusa visehemu vya elektroniki wakati wa kubadilisha vifuniko vyovyote. Daima hifadhi na kutumia kifaa kikiwa na vifuniko vyake vimewekwa.
Mwongozo wa mtumiaji
Fungua kifuniko cha nyuma
1. Weka kucha yako ya kidole katika nafasi ndogo chini ya simu, inua na uondoe kifuniko.
2. Ikiwa betri iko ndani ya simu, itoe.
Ingiza SIM kadi
1. Telezesha kishikio cha SIM kadi upande wa kushoto na ukifungue.
2. Weka nano-SIM katika nafasi ya SIM ikiangalia chini.
3. Funga kishikiliaji, na uitelezeshe upande wa kulia ili uifunge mahali pake.
Mwongozo wa mtumiaji
Ingiza SIM ya pili
1. Telezesha kishikilia SIM kadi cha kipenyo cha SIM2 upande wa kulia na uifungue.
2. Weka nano-SIM katika kipenyo cha SIM2 ikiangalia chini.
3. Funga kishikiliaji, na ukitelezeshe upande wa kushoto ili ukifunge mahali pake. SIM kadi zote zinapatikana kwa wakati mmoja wakati kifaa hakitumiki, lakini ijapokuwa SIM kadi moja inatumika, kwa mfano, kwa kupiga simu, ile nyingine haipatikani.
Kidokezo: Ili kujua ikiwa simu yako inaweza kutumia SIM kadi 2, angalia lebo kwenye sanduku la mauzo. Ikiwa kuna misimbo 2 ya IMEI kwenye lebo, una simu yenye SIM mbili.
Ingiza kadi ya kumbukumbu
Mwongozo wa mtumiaji
1. Telezesha kadi ya kumbukumbu kwenye nafasi ya kadi ya kumbukumbu.
2. Rudisha betri.
3. Rejesha kifuniko cha nyuma.
Washa simu yako
Bonyeza na ushikilie .

CHAJI SIMU YAKO

Betri yako imechajiwa nusu kiwandani, lakini utahitajika kuichaji upya kabla uweze kutumia simu yako.
Chaji betri
1. Chomeka chaja kwenye soketi ya ukuta.
2. Unganisha chaja kwenye simu. Ukimaliza, chomoa chaja kwenye simu, kisha kwenye soketi ya ukuta.
Kama betri imeisha moto kabisa, huenda ikachukua dakika kadhaa kabla ya kiashiria chaji kuonyeshwa.
Kidokezo: Unaweza kuchaji kwa kutumia USB wakati umeme wa ukutani haupatikani. Data inaweza kuhamishwa ukichaji kifaa. Ubora wa nishati ya kuchaji kwa USB hutofautiana, na huenda ikachukua muda mrefu kuchaji kuanza na kifaa kuanza kufanya kazi. Hakikisha kompyuta yako imewashwa.

VITUFE

Tumia vitufe vya simu
• Ili kuona programu na vipengele vya simu yako, kwenye skrini ya mwanzo, chagua Menyu .
• Ili kwenda kwenye programu au kipengele, bonyeza kitufe cha kutambaza juu, chini, kushoto, au kulia. Ili kufungua programu au kipengele, bonyeza kitufe cha kutambaza.
Funga vitufe
Ili kuepuka kubonyeza vitufe kwa bahati mbaya, funga vitufe. bonyeza . Ili ufungue vitufe, bonyeza kitufe cha kutembeza, na uchague Fungua > * .
Mwongozo wa mtumiaji
Andika kwa kutumia kitufe
Bonyeza kitufe kisha utumie kitufe cha kutembeza ili uchague herufi unayotaka.
Ili kucharaza katika nafasi bonyeza 0 .
Ili kucharaza kibambo maalum au alama ya kituo, chagua > Ingiza chaguo > Ingiza alama .
Ili kubadilisha kati ya vibambo, bonyeza # kwa kurudia.
Ili kuandika nambari, bonyeza kitufe cha nambari na utumie kitufe cha kutembeza ili uchague nambari.
Mwongozo wa mtumiaji
4 Simu, majina, na ujumbe

SIMU

Piga simu
Jifunze jinsi ya kupiga simu kwa kutumia simu yako mpya.
1. Ingiza namba ya simu. Ili kucharaza kibambo cha +, kinachotumiwa kwa simu za kimataifa, bonyeza * mara mbili.
2. Bonyeza . Ukiulizwa, chagua ni SIM gani ya kutumia.
3. Kukata simu, bonyeza .
Jibu simu
Bonyeza .

MAJINA

Ongeza jina
1. Chagua Menyu > > + Mwasiliani mpya .
2. Andika jina, na ucharaze nambari.
3. Chagua > Sawa .
Ili kuongeza waasiliani zaidi, chagua > Ongeza mwasiliani mpya .
Hifadhi mwasiliani kutoka kwenye rekodi ya simu
1. Chagua Menyu > .
2. Tembeza kwa nambari unataka kuhifadhi, chagua > Ongeza kwa Waasiliani >
Mwasiliani mpya .
3. Ongeza jina la mwasiliani, kagua kwamba nambari ya simu ni sahihi, na uchague > Sawa .
Pigia simu mwasiliani
Unaweza kupigia simu mwasiliani moja kwa moja kutoka kwenye orodha ya waasiliani.
Chagua Menyu > , tembeza kwa mwasiliani unataka kupigia simu, na ubonyeze kitufe cha kupiga simu.
Mwongozo wa mtumiaji

TUMA UJUMBE

Andika na utume ujumbe
1. Chagua Menyu > > + Ujumbe mpya .
2. Katika sehemu ya Wapokeaji, ingiza nambari ya mpokeaji, au uchague >
Waasiliani ili kuongeza waasiliani kutoka
kwa orodha yako ya waasiliani.
3. Andika ujumbe kwenye sehemu ya ujumbe.
4. Ili kuingiza smaili au alama kwenye ujumbe,
chagua > Chaguo za kuingiza >
Ingiza smaili au Ingiza alama .
5. Chagua Tuma .
Mwongozo wa mtumiaji
5 Binafsisha simu yako

BADILISHA TONI

Weka toni mpya
1. Chagua Menyu > > Ubinafsishaji > Sauti .
2. Chagua toni unataka kubadilisha.
3. Telezesha kwenye toni unataka na uchague Chagua .

BADILISHA MWONEKANO WA SKRINI YAKO YA MWANZO

Chagua pazia mpya
Unaweza kubadilisha madharinyuma ya skrini yako ya mwanzo.
1. Chagua Menyu > > Ubinafsishaji > Funga mandharinyuma ya skrini > Pazia .
2. Telezesha mandharinyuma unataka na uchague Chagua .
3. Ikiwa umependezwa na pazia, chagua .

PATA MENGI KUTOKA KWA SIM KADI MBILI

Simu yako inaweza kuwa na SIM kadi mbili, na unaweza kuzitumia kwa malengo tofauti.
Chagua ni SIM kadi gani itatumika
Chagua Menyu > > Muunganisho > SIM Mbili .
• Ili kuchagua SIM gani ya kutumia kupiga simu, chagua SIM inayopendelewa kupiga simu .
• Kuchagua ni SIM gani ya kutumia kwa ujumbe, chagua SIM inayopendelewa ya ujumbe .
• Kuchagua ni SIM gani ya kutumia kwa data ya simu, chagua Muunganisho wa data ya simu > SIM unayopendelea .
Dokezo: Unaweza kuweka jina jipya la SIM kadi zako ili iwe rahisi kuzitofautisha. Chagua
Menyu > > Muunganisho > SIM mbili > Mipangilio ya SIM . Chagua SIM na jina la SIM .
Mwongozo wa mtumiaji
6 Kamera

PICHA NA VIDEO

Hauhitaji kamera tofauti wakati simu yako ina kila kitu unachohitaji ili kunasa kumbukumbu.
Piga picha
1. Chagua Menyu > .
2. Kupiga picha, chagua .
Ili kutazama picha uliyopiga, chagua > Galari .
Chaguo za kamera
Chagua Menyu > > , na uteue chaguo unataka, kama vile Athari au Kipima saa .
Rekodi video
1. Ili kuwasha kamera ya video, chagua Menyu > na utembeze kwa .
2. Ili kukomesha kurekodi, chagua .
3. Ili kukomesha kurekodi, chagua .
Ili kutazama video uliyorekodi, teua Menyu > Video .
Mwongozo wa mtumiaji
7 Intaneti na miunganisho

VINJARI WAVUTI

Unganisha kwenye intaneti
Kumbuka kwamba huenda kivinjari kikatofautiana na eneo lako na kufanya kazi kitofauti.
1. Chagua Menyu > .
2. Andika anwani ya wavuti, na ubonyeze Sawa .

BLUETOOTH®

Unganisha simu yako kwenye vifaa vingine kwa kutumia Bluetooth.
Washa Bluetooth
1. Chagua Menyu > > Muunganisho > Bluetooth .
2. Washa Bluetooth .
3. Chagua Vifaa vinavyopatikana na kifaa cha Bluetooth unataka kuunganisha.
Mwongozo wa mtumiaji
8 Muziki

KICHEZA MUZIKI

Unaweza kusikiliza faili zako za muziki wa MP3 kwa kutumia kicheza muziki.
Sikiliza muziki
Kucheza muziki, unahitaji kuhifadhi faili za muziki kwenye kadi ya kumbukumbu au kumbukumbu ya simu.
1. Chagua Menyu > .
2. Chagua Nyimbo ili uone muziki wako wote uliohifadhiwa.
3. Tembeza kwa wimbo na uchague Cheza .
Unaweza pia kuunda orodha yako mwenyewe ya kucheza.
Ili kurekebisha sauti, tembeza juu au chini.

SIKILIZA REDIO

Sikiliza kituo chako ukipendacho cha redio kwenye simu yako
Chagua Menyu > . Simu yako hutafuta vituo kiotomatiki unapowasha redio. Ili kubadilisha sauti, tembeza juu au chini. Ili kuhifadhi kituo, chagua > Ongeza kwenye vipendwa . Ili kubadilisha kwa kituo kilichohifadhiwa, chagua > Vipendwa , na uchague kituo. Ili kufunga redio, chagua > Funga redio .
Mwongozo wa mtumiaji
9 Saa, kalenda, na kikokotoo

WEKA SAA NA TAREHE WEWE MWENYEWE

Badilisha saa na tarehe
1. Chagua Menyu > > Saa na tarehe >
Tarehe na saa .
2. Zima Sasisha kiotomatiki .
3. Ili kuweka saa, chagua Saa na uingize saa.
4. Ili kuweka tarehe, chagua Tarehe na uingize tarehe.
5. Chagua Hifadhi .

SAA YA KENGELE

Jifunze jinsi ya kutumia saa ya kengele ili kukuamsha na ufike maeneo kwa wakati unaofaa.
Weka kengele
Huna saa? Tumia simu yako kama saa ya kengele.
1. Chagua Menyu > .
2. Chagua + Kengele mpya na uingize saa ya kengele na maelezo mengine.
3. Chagua > Hifadhi .

KALENDA

Ongeza tukio la kalenda
1. Chagua Menyu > .
2. Tembeza kwa tarehe, na uchague > Ongeza tukio jipya .
3. Ingiza maelezo ya tukio, na uchague Hifadhi .

KIKOKOTOO

Jifunze jinsi ya kuongeza, kuondoa, kuzidisha na kugawanya kwa kutumia kikokotoo cha simu yako.
Mwongozo wa mtumiaji
Jinsi ya kuhesabu
1. Chagua Menyu > .
2. Ingiza nambari ya kwanza ya hesabu yako, tumia kitufe cha kutembeza ili uchague shughuli, na uingize nambari ya pili.
3. Bonyeza kitufe cha kutambaza ili upate matokeo ya hesabu hiyo.
Chagua ili kufuta sehemu za nambari.
Mwongozo wa mtumiaji
10 Safisha simu yako

ONDOA MAUDHUI BINAFSI KWENYE SIMU YAKO

Ukinunua simu mpya, au uwe unataka kutupa au kuchakata upya simu yako, hivi ndivyo unavyoweza kuondoa maelezo na maudhui yako ya kibinafsi. Kumbuka kwamba ni wajibu wako kuondoa maudhui yote ya kibinafsi.
Ondoa maudhui kwenye simu yako
Wakati unaondoa maudhui ya kibinafsi kwenye simu yako, zingatia kama unaondoa maudhui kwenye kumbukumbu ya simu au SIM kadi.
Ili kuondoa ujumbe, chagua Menyu > . Chagua > Futa mazungumzo , chagua ujumbe zote na .
Ili kuondoa waasiliani, chagua Menyu > . Chagua > Futa waasiliani , chagua waasiliani wote na .
Ili kuondoa maelezo yako ya simu, chagua Menyu > . Chagua > Futa zote > Sawa .
Kagua ikiwa maudhui yote ya kibinafsi yameondolewa.
Mwongozo wa mtumiaji
11 Maelezo ya bidhaa na usalama

KWA USALAMA WAKO

Soma maelekezo haya rahisi. Kutoyafuata kunaweza kuwa hatari au kinyume cha sheria na masharti. Kwa maelezo zaidi, soma mwongozo kamili wa mtumiaji.
ZIMA KATIKA MAENEO YALIYOKATAZWA
Zima kifaa wakati matumizi ya simu za mkononi yamekatazwa au wakati yanaweza kusababisha mwingiliano au hatari, kwa mfano, ndani ya ndege au hospitalini, au karibu na vifaa vya matibabu, mafuta, kemikali, au maeneo yenye mlipuko. Tii maagizo yote katika maeneo yaliyozuiwa.
USALAMA BARABARANI HUJA KWANZA
Tii sheria zote za mahali ulipo. Daima iache mikono yako iwe huru wakati unaendesha gari. Kitu cha kuzingatia kwanza unapoendesha gari unapaswa kuwa usalama barabarani.
MWINGILIANO
Mwongozo wa mtumiaji
Vifaa vyote visivyotumia waya vina uwezekano wa kupata mwingiliano, ambao unaweza kuathiri utendaji kazi wake.
HUDUMA ILIYOIDHINISHWA
Watu walioidhinishwa tu ndio wanaweza kuweka au kukarabati bidhaa hii.
BETRI, CHAJA, NA VIFAA VINGINE VYA ZIADA
Tumia betri, chaja, na vifaa vya ziada ambavyo vimeidhinishwa na HMD Global Oy kwa ajili ya matumizi na kifaa hiki tu. Usiunganishe bidhaa ambazo haziendani pamoja.
WEKA KIFAA KIKIWA KIKAVU
Ikiwa kifaa chako kinaweza kuzuia maji, tafadhali rejelea ukadiriaji wake wa IP kwa mwongozo zaidi wa kina.
Mwongozo wa mtumiaji
LINDA UWEZO WAKO WA KUSIKIA
Kuzuia madhara yanayowezekana ya kusikia, usisikilize katika viwango vya juu vya sauti kwa muda mrefu. Kuwa mwangalifu wakati unashikilia kifaa chako karibu na sikio wakati kipaza sauti kinatumika.
SAR
Kifaa hiki kinatimiza matakwa ya maelekezo ya ujiwekaji wazi kwa frikwensi za redio wakati kikitumika ama kwenye mkao wa kawaida kwenye sikio au wakati kikiwekwa angalau sentimita
1.5 (inchi 5/8) kutoka kwenye mwili. Thamani maalum za juu za SAR zinaweza kupatikana katika sehemu ya Maelezo ya Cheti ya (SAR) ya mwongozo huu wa mtumiaji. Kwa maelezo zaidi, angalia sehemu ya Maelezo ya Cheti (SAR) ya mwongozu huu wa mtumiaji au nenda kwenye
www.sar-tick.com.

SIMU ZA DHARURA

Muhimu: Miunganisho katika hali zote haiwezi kuhakikishwa. Kamwe usitegemee tu simu
pasiwaya kwa mawasiliano muhimu kama vile tiba za dharura.
Kabla ya kupiga simu:
• Washa simu.
• Kama skrini na vitufe vya simu vimefungwa, vifungue.
• Nenda eneo lenye mawimbi ya simu ya kutosha.
1. Bonyeza kitufe cha kukata simu kwa kurudia, hadi skrini ya mwanzo ionyeshwe.
Mwongozo wa mtumiaji
2. Charaza namba rasmi ya dharura ya eneo lako la sasa. Nambari za simu ya dharura hutofautiana kimaeneo.
3. Bonyeza kitufe cha simu.
4. Toa maelezo yanayofaa kwa usahihi kama iwezekanavyo. Usikate simu hadi upewe ruhusa ya kufanya hivyo.
Huenda pia ukahitajika kufanya yafuatayo:
• Weka SIM kadi ndani ya simu.
• Ikiwa simu yako itakuuliza msimbo wa PIN, charaza nambari rasmi ya dharura ya eneo lako la sasa, na ubonyeze kitufe cha simu.
• Zima vizuizi vya simu katika simu yako, kama vile uzuiaji simu, upigaji uliopangwa, au kikundi maalum cha watumiaji.

KUHUDUMIA KIFAA CHAKO

Shughulikia kifaa chako, betri, chaja na vifaa vya ziada kwa uangalifu. Mapendekezo yafuatayo yatakusaidia kufanya kifaa chako kifanye kazi.
• Weka kifaa kikiwa kikavu. Taka za mtuamo, unyevu wa hewa, na aina zote za vimiminiko au unyevu zinaweza kuwa na madini yanayoweza kutia kutu saketi za elektroniki.
• Usitumie au kuhifadhi kifaa chako kwenye maeneo yenye vumbi au uchafu.
• Usihifadhi kifaa kwenye halijoto ya juu au ya chini. Halijoto ya juu huenda ikaharibu kifaa au betri.
• Usihifadhi kifaa kwenye halijoto baridi. Wakati kifaa kimerudi kwenye joto lake la kawaida, unyevunyevu unaweza kutengenezeka ndani ya kifaa.
• Usifungue kifaa kando na ilivyoagizwa katika kiongozi cha mtumiaji.
• Mabadiliko yasioidhinishwa yanaweza kuharibu kifaa hiki na kukiuka sheria zinazosimamia vifaa vya redio.
• Usiangushe, kugonga, au kutingisa kifaa au betri. Kukishika kiholela kunaweza kuivunja.
• Tumia kitambaa laini, kisafi na kikavu kusafisha uso wa kifaa hiki.
• Usipake rangi kifaa. Rangi inaweza kuzuia utendaji kazi wa kawaida.
• Weka kifaa chako mbali na sumaku au maeneo ya sumaku.
• Ili kuweka data yako muhimu salama, ihifadhi angalau katika maeneo mawili tofauti, kama vile kifaa chako, kadi ya kumbukumbu, au kompyuta au andika maelezo muhimu.
Wakati wa utendajikazi kwa muda mrefu, kifaa kinaweza kuwa na joto. Katika hali nyingi, hii ni kawaida. Kuepuka kupata joto sana, huenda kifaa kikapunguza kasi kiotomatiki, kikafunga programu, kikazima kuchaji, na ikiwezekana, kikajizima. Kama kifaa hakifanyi kazi sawasawa, kipeleke kwenye kitengo cha mtengenezaji aliyeidhinishwa kilicho karibu.
Mwongozo wa mtumiaji

UCHAKATAJI UPYA

Daima rudisha bidhaa zako za elektroniki, betri na nyezo za kifurushi zilizotumiwa kwa maeneo maalum ya ukusanyaji. Kwa njia hii utasaidia kuzuia utupaji taka usiodhibitiwa na kukuza uchakataji upya wa nyenzo. Bidhaa za umeme na elektroniki huwa na nyenzo nyingi za thamani, ikiwa ni pamoja na madini (kama vile shaba, aluminiamu, chuma, na magnesiamu) na madini ya thamani (kama vile dhahabu, fedha, na paladiamu) Nyenzo zote za kifaa zinaweza kufufuliwa kama nyenzo na nishati.

ALAMA YA PIPA ILIYO NA MKATO

Alama ya pipa iliyo na mkato
Alama ya pipa iliyo na mkato kwenye bidhaa, betri, maandishi, au kifurushi chako hukukumbusha kwamba bidhaa zote za elektroniki na betri lazima zipelekwe kwenye mkusanyiko tofauti wakati bidhaa inapokwisha. Usitupe bidhaa hizi kama takataka zisizochambuliwa za manispaa: zipeleke zichakatwe. Kwa maelezo juu ya eneo la uchakataji lililo karibu na wewe, wasiliana na mamlaka ya taka ya eneo lako.

MAELEZO YA BETRI NA CHAJA

Maelezo ya usalama wa betri na chaja
Ili kuchopoa chaja au kifaa chochote cha ziada, kamata na uvute plagi na siyo waya.
Wakati chaja yako haitumiki, ichomoe. Ikiachwa bila kutumika, betri iliyokuwa imejaa chaji itapoteza chaji yake kadri muda unavyopita.
Mwongozo wa mtumiaji
Daima jaribu kuweka betri kwenye halijoto kati ya 59°C na 77°F (15°C na 25°C) kwa utendakazi bora. Halijoto ya juu sana hupunguza uwezo na uhai wa betri. Kifaa chenye betri moto au baridi kinaweza kisifanye kazi kwa muda. Mkato wa umeme wa bahati mbaya unaweza kutokea kwa bahati mbaya kama kitu cha chuma kitagusa vipapi vya chuma kwenye betri. Huenda hii ikaharibu betri au kifaa kile kingine.
Usitupe betri kwenye moto kwa sababu zinaweza kulipuka. Tii sheria za eneo lako. Peleka ichakatwe upya ikiwezekana. Usitupe kama takataka za kawaida za nyumbani.
Usifungue, kukata, kuvunja, kukunja, kutoa, au kuharibu betri kwa njia yoyote ile. Kama betri itavuja, usiruhusu umaji uguse ngozi au macho. Hii ikifanyika, osha maeneo yaliyoathirika mara moja na maji, au tafuta msaada wa kitabibu. Usirekebishe, kujaribu kuingiza vitu vigeni kwenye betri, au kuizamisha au kuiweka kwenye maji au aina nyingine ya umaji. Betri zinaweza kulipuka kama zimeharibika.
Tumia betri na chaja kwa matumizi yaliyokusudiwa tu. Matumizi mabaya, au matumizi yasiyoidhinishwa au yasiyotangamana na betri au chaja huenda yakaleta hatari ya moto, mlipuko au hatari nyingine, na huenda ikabatilisha uhalali wowote ulioidhinishwa au waranti. Kama unaamini betri au chaja imeharibika, ipeleke kwa kituo cha huduma au muuza simu yako kabla ya kuendelea kuitumia. Kamwe usitumie betri au chaja yoyote iliyoharibika. Tumia chaja ndani ya nyumba tu. Usichaji kifaa chako wakati wa dhoruba ya radi.

WATOTO WADOGO

Kifaa chako na viboreshaji vyake sio sesere. Vinaweza kuwa na sehemu ndogo ndogo. Viweke mbali na watoto wadogo.

VIFAA VYA MATIBABU

Utendakazi wa kifaa cha kupitisha mawimbi ya redio, pamoja na simu pasiwaya, huenda zikaingiliana na utendakazi wa vifaa vya matibabu ambavyo havijakingwa vizuri. Wasiliana na daktari au mtengenezaji wa kifaa cha matibabu ili ubainishe kama kimekingwa vizuri dhidi ya nguvu ya nje ya redio.

VIFAA VYA MATIBABU VINAVYOPACHIKWA

Kuepuka mwingiliano unaowezekana, watengenezaji wa vifaa vilivyopachikwa vya matibabu wanapendekeza nafasi isiyopungua sentimita 15.3 (inchi 6) kati ya kifaa kisichotumia waya na kifaa cha matibabu. Watu ambao wana vifaa kama hivyo wanapaswa:
• Kila wakati weka kifaa pasiwaya umbali wa zaidi ya sentimita 15.3 (inchi 6) kutoka kwenye kifaa cha matibabu.
• Usibebe kifaa pasiwaya katika mfuko wa
shati.
• Shikilia kifaa pasiwaya kwenye sikio kando na kifaa cha matibabu.
• Zima kifaa pasiwaya kama kuna sababu
Mwongozo wa mtumiaji
yoyote ya kushuku kwamba mwingiliano unafanyika.
Ikiwa una maswali yoyote kuhusu kutumia kifaa chako pasiwaya na kifaa cha matibabu kilichopachikwa, wasiliana na mtoa huduma wako wa afya.
• Fuata maagizo ya mtengeneza kifaa cha matibabu kilichopachikwa.

VIFAA VYA KUSAIDIA KUSIKIA

Onyo: Wakati unatumia kifaa cha kuvaa kichwani, uwezo wako wa kusikiliza sauti za nje
unaweza kuathirika. Usitumie kifaa cha kuvaa kichwani mahali ambapo kinaweza kuhatarisha usalama wako.
Baadhi ya vifaa pasiwaya vinaweza kuingiliana na baadhi ya vifaa vya kusaidia kusikia.

LINDA KIFAA CHAKO DHIDI YA MAUDHUI MABAYA

Huenda kifaa chako kikakumbana na virusi na maudhui mengine mabaya. Kuwa mwangalifu wakati wa kufungua ujumbe. Huenda zikawa na programu mbaya au zikaharibu kifaa chako.

MAGARI

Huenda mawimbi ya redio yakaathiri vibaya mifumo ya elektroniki iliyowekwa vibaya au isiyokingwa vizuri katika magari. Kwa maelezo zaidi, wasiliana na mtengeneza gari lako au vifaa vyake. Watu walioidhinishwa tu ndio wanaweza kukarabati au kuweka kifaa ndani ya gari. Uwekaji wenye kasoro huenda ukawa hatari na ukabatilisha waranti yako. Hakikisha mara kwa mara kwamba vifaa vyote pasiwaya ndani ya gari vimefungwa vizuri na vinafanya kazi sawasawa. Usihifadhi au kubeba vifaa vinavyoweza kuchomeka au kulipuka katika eneo lile moja kama kifaa, sehemu zake, au vifaa vya ziada. Usiweke kifaa chako au viboreshaji kwenye eneo ambalo mfuko wa hewa hutumika.

MAZINGIRA YANAYOWEZA KULIPUKA

Zima kifaa chako katika eneo lolote lenya mazingira yanayoweza kulipika, kama vile karibu na pampu za mafuta katika vituo vya mafuta. Cheche zinaweza kusababisha mlipuko au moto unaoweza kuleta majeraha au kifo. Kumbuka vikwazo katika maeneo yenye mafuta; viwanda vya kemikali; au mahali ambapo shughuli za ulipuaji zinaendelea kufanyika. Maeneo yenye mazingira yenye uwezekano wa milipuko yanaweza kuwa na alama zisizo dhahiri. Haya kwa kawaida ni maeneo ambapo unaweza kushauriwa kuzima injini yako, chini ya sitaha kwenye boti, uhamishaji kemikali au suhula za kuhifadhi, na ambapo hewa ina kemikali au chembechembe kama vile nafaka, vumbi au poda ya chuma. Wasiliana na watengeneza magari yanayotumia mafuta aina ya gesi oevu ya petroli iliyoyeyushwa (kama vile propeni au buteni) ikiwa kifaa hiki kinaweza kutumiwa vizuri katika maeneo yao.
Mwongozo wa mtumiaji

HABARI YA UTOAJI CHETI (SAR)

Kifaa hiki cha mkononi kinatimiza maelekezo yanayohusu ujiwekaji wazi kwa mawimbi ya redio.
Kifaa chako cha mkononi ni transmita na kipokezi cha redio. Kimeundwa kisizidishe viwango vya ufichuzi vya mawimbi ya redio (maeneo ya mawimbi ya redio ya sumaku ya umeme), vinavyopendekezwa na miongozo ya kimataifa kutoka kwa shirika huru la kisayansi ICNIRP. Maelekezo haya yanajumuisha viwango vya usalama vilivyoundwa kuhakikisha usalama wa watu wote, Haijalishi umri na afya. Maelekezo ya ufichuzi yanategemea Kiwango Maalum cha Ufyonzaji (SAR), ambacho ni onyesho la nguvu ya kiwango cha masafa ya redio (RF) ambayo inawekwa kichwani au mwilini wakati kifaa kinatumika. Kiwango cha SAR cha ICNIRP cha vifaa vya simu ni 2.0 W/kg kwa wastani wa gramu kumi za tishu.
Vipimo vya SAR vinatekelezwa kwa kifaa katika mikao ya kawaida ya uendeshaji, wakati kifaa kinapitisha katika kiwango chake cha juu zaidi kilichoidhinishwa cha nishati, katika bendi zote zilizopimwa za masafa.
Tafadhali rejelea www.nokia.com/phones/sar kwa thamani ya juu ya SAR ya kifaa.
Kifaa hiki kinatimiza matakwa ya maelekezo ya ujiwekaji wazi kichwani au wakati kimewekwa angalau inchi 5/8 (sentimita 1.5) kutoka kwenye mwili. Wakati kikasha cha kubebea, kishikiza kwenye mkanda au aina nyingi ya kishikizi kikitumika kwa matumizi ya kuvaliwa mwilini, kinatakiwa kisiwe na chuma na kinatakiwa kuweka angalia umbali uliotajwa hapo juu kutoka kwenye mwili.
Kutuma data au ujumbe, muunganisho salama wa mtandao unahitajika. Utumaji unaweza kucheleweshwa hadi muunganisho huo upatikane. Fuata maagizo ya umbali wa kutenganisha hadi utumaji ukamilike.
Wakati wa matumizi ya kawaida, thamani za SAR kwa kawaida huwa chini ya thamani zilizotajwa hapa juu. Hii ni kwa sababu, kwa malengo ya ubora wa mfumo na kupunguza mwingiliano kwenye mtandao, nguvu ya kufanya kazi ya kifaa chako cha mkononi hupunguzwa kiotomati wakati nguvu kamili haihitajiki kwa simu. Nguvu towe inavyoendelea kuwa chini, ndivyo thamani ya SAR inavyokuwa chini.
Huenda modeli za vifaa zikawa na matoleo tofauti na zaidi ya thamani moja. Mabadiliko ya vijenzi na muundo yanaweza kufanyika baada ya muda na baadhi ya mabadiliko yanaweza kuathiri thamani za SAR.
Kwa maelezo zaidi, nenda kwenye www.sar-tick.com. Kumbuka kwamba vifaa vya mkononi huenda vikapitisha hata kama hupigi simu.
Shirika la Afya Duniani (WHO) limesema kwamba maelezo ya sasa ya kisayansi hayaashirii hitaji la tahadhari zozote maalum wakati wa kutumia vifaa vya mkononi. Ikiwa unavutiwa na kupunguza ufichuzi wako, wanapendekeza upunguze matumizi yako au utumie kifaa kisichotumia mikono ili kuweka kifaa mbali na kichwa na mwili wako. Kwa maelezo zaidi na ufafanuzi na majadiliano kuhusu ufichuzi wa RF, nenda kwenye tovuti ya WHO
www.who.int/peh-emf/en.
Mwongozo wa mtumiaji

KUHUSU USIMAMIZI WA HAKI ZA DIJITALI

Unapokuwa ukitumia kifaa hiki, tii sheria zote na heshimu utamaduni wa wenyeji, uhuru binafsi wa mtu na haki halali za wengine, ikiwemo hakimiliki. Kinga za hakimiliki zinaweza kukuzuia dhidi ya kunakili, kurekebisha au kuhamisha picha, muziki na vitu vingine.

HAKIMILIKI NA ILANI NYINGINE

Hakimiliki
Upatikanaji wa bidhaa, vipengele, programu na huduma unaweza kutofautiana kimaeneo. Kwa maelezo zaidi, wasiliana na mchuuzi au mtoa huduma wako. Kifaa hiki kinaweza kuwa na bidhaa, teknolojia au programu ambayo inategemea sheria na masharti ya usafirishaji nje ya nchi kutoka Marekani na nchi nyingine. Uchepushaji kinyume na sheria ni marufuku.
Yaliyomo katika waraka huu yametolewa ”kama yalivyo”. Isipokuwa kama inatakiwa hivyo na sheria husika, hakuna dhamana za aina yoyote, ama za moja kwa moja au zisizo bayana, pamoja na, lakini isiyokomea hapo, dhamana zisizo bayana za uuzikaji wa kibiashara na ufaaji kwa matumizi fulani, zinazotolewa kuhusiana na usahihi, uaminikaji au yaliyomo ndani ya waraka huu. HMD Global ina haki ya kupitia na kusahihisha waraka huu au kuuondoa wakati wowote bila kutoa taarifa kwanza.
Kwa kadiri inayohusiwa na sheria husika, hakuna wakati wowote ule HMD Global au wenye leseni wake watawajibika kwa upotevu wowote wa data au mapato au uharibifu wowote ule, uwe maalum, wa ajali, unatokana na, au usiokuwa wa moja kwa moja uliosababishwa.
Ni marufuku kutoa upya, kuhamisha au kusambaza sehemu ya yaliyomo au yote katika waraka huu katika hali yoyote ile bila ya kupewa kwanza idhini ya kuandikwa kutoka kwa HMD Global. HMD Global inaendesha sera ya kuendelea kubuni. HMD Global ina haki ya kufanya mabadiliko na kuboresha bidhaa yake yoyote iliyoelezwa katika waraka huu bila kutoa taarifa kwanza.
HMD Global haitoi uhakikisho wowote, waranti au kuwajibika kwa utendakazi, maudhui, au usaidizi wa mtumiaji wa programu za mhusika mwingine zilizotolewa na kifaa chako. Kwa kutumia programu, unakubali kwamba programu imetolewa kama ilivyo.
Upakuaji wa ramani, michezo, muziki na video na upakiaji wa picha na video huenda ukajumuisha upitishaji wa viwango vikubwa vya data. Huenda mtoa huduma wako akatoza kwa upitishaji data. Upatikanaji wa bidhaa, huduma na vipengele fulani unaweza zikatofautiana kimaeneo. Tafadhali wasiliana na muuzaji wa eneo lako kwa maelezo zaidi na upatikanaji wa chaguo za lugha.
Vipengele, utendakazi na ainisho nyingine za bidhaa zinaweza kutegemea mtandao na hutegemea masharti, sheria, na gharama za ziada.
Ainisho, vipengele na maelezo mengine yote ya bidhaa yaliyotolewa yanaweza kubadilika bila ilani.
Sera ya Faragha ya HMD Global, inapatikana kwenye http://www.nokia.com/phones/privacy, hutumika kwa matumizi yako ya kifaa.
Mwongozo wa mtumiaji
HMD Global Oy ndio ina leseni ya kipekee ya chapa ya Nokia ya simu na kompyuta kibao. Nokia ni alama ya biashara iliyosajiliwa ya Nokia Corporation.
Alama ya neno na nembo za Bluetooth zinamilikiwa na Bluetooth SIG, Inc. na matumizi yoyote ya alama hizo na HMD Global yako chini ya leseni.
Bidhaa hii inajumuisha programu huria. Kwa hakimiliki husika na ilani, vibali, na ukubalifu mwingine, chagua *#6774# kwenye skrini ya mwanzo.
Loading...