Muhimu: Kwa maelezo muhimu kuhusu matumizi salama ya kifaa na betri yako, soma maelezo
ya ”Kwa usalama wako” na ”Usalama wa Bidhaa” katika mwongozo uliochapishwa wa mtumiaji,
au kwenye www.nokia.com/support kabla utumie kifaa. Ili kujua jinsi ya kuanza kutumia kifaa
chako kipya, soma mwongozo uliochapishwa wa mtumiaji.
Jiepushe kugusa eneo la antena bila sababu wakati antena inatumika. Ugusaji antena huathiri
ubora wa mawasiliano na unaweza kupunguza maisha ya betri kwa sababu ya kiwango cha juu
zaidi cha nishati wakati wa utendaji kazi.
Usiunganishe kwenye bidhaa ambazo zinaunda ishara ya kutoa, kwa kuwa hii inaweza kuharibu
kifaa. Usiunganishe chanzo chochote cha stima kwenye kiunganisha cha sauti. Ukiunganisha
kifaa chochote cha nje au kifaa chochote cha kichwa kando na zile zilizoidhinishwa kutumiwa na
kifaa hiki, Kiunganishi cha sauti, kuwa makini sana na viwango vya sauti.
Sehemu nyingine za kifaa hiki zina sumaku. Vitu vya chuma vinaweza kuvutwa na kifaa. Usiweke
kadi za karadha au vitu vingine vyenye kutumia hifadhi ya sumaku karibu na kifaa hiki, kwa
sababu maelezo yaliyohifadhiwa kwenye vitu hivyo yanaweza kufutika.
Baadhi ya vifaa vya ziada vilivyotajwa katika kiongozi hiki, kama vile chaja, kifaa cha kichwani, au
kebo ya data, huenda vikauzwa kando.
Usalama > Kilinda vitufe na uweke Msimbo wa usalama kwa washa. Ikiwa kuna msimbo
uliowekwa mapema, ni 12345. Ibadilishe ili ulinde faragha yako na data binafsi. Kumbuka, hata
hivyo, wakati unabadilisha msimbo, unahitaji kukumbuka msimbo mpya, kwa kuwa HMD Global
haiwezi kuufungua au kuiruka.
SANIDI NA UWASHE SIMU YAKO
Jifunze jinsi ya kuingiza SIM kadi, kadi ya kumbukumbu, na betri, na jinsi ya kuwasha simu yako.
SIM Ndogo
Muhimu: Kifaa hiki kimeundwa ili kutumiwa na SIM kadi ndogo pekee tu (angalia mfano).
Matumizi ya kadi zisizotangamana za SIM zinaweza kuharibu kadi au kifaa, na zinaweza
kuharibu data iliyohifadhiwa kwenye kadi. Tafadhali wasiliana na opereta wa simu yako kwa
matumizi ya SIM kadi ambayo ina mkato wa nano-UICC.
Tumia tu kadi za kumbukumbu zinazotangamana zilizoidhinishwa kutumiwa na kifaa hiki. Kadi
zisizotangamana zinaweza kuharibu kadi na kifaa na kuharibu data iliyohifadhiwa kwenye kadi.
Kumbuka: Zima kifaa na usiiunganishe na chaja au kifaa kingine chochote kabla ya kubandua
vifuniko vyovyote. Epuka kugusa visehemu vya elektroniki wakati wa kubadilisha vifuniko
vyovyote. Daima hifadhi na kutumia kifaa kikiwa na vifuniko vyake vimewekwa.
Sanidi na uwashe simu yako (SIM moja)
1. Weka kucha yako ya kidole katika nafasi
ndogo chini ya simu, inua na uondoe
kifuniko.
2. Ikiwa betri iko ndani ya simu, itoe.
4. Ikiwa una kadi ya kumbukumbu, telezesha
kadi ya kumbukumbu kwenye nafasi ya
kadi ya kumbukumbu.
5. Lainisha maeneo ya mguso ya betri, na
uweke betri ndani.
3. Telezesha SIM kwenye kipenyo cha SIM
eneo la mguso likiangalia chini.
1. Weka kucha yako ya kidole katika nafasi
ndogo chini ya simu, inua na uondoe
kifuniko.
2. Ikiwa betri iko ndani ya simu, itoe.
3. Telezesha SIM ya kwanza kwenye kipenyo
cha SIM 1 eneo la mguso likiangalia chini.
Telezesha SIM ya pili kwenye kipenye cha 2
cha SIM. SIM kadi zote zinapatikana kwa
wakati mmoja wakati kifaa hakitumiki,
Washa simu yako
Bonyeza na ushikilie kitufe cha .
Ondoa SIM kadi
lakini ijapokuwa SIM kadi moja inatumika,
kwa mfano, kwa kupiga simu, ile nyingine
haipatikani.
4. Ikiwa una kadi ya kumbukumbu, telezesha
kadi ya kumbukumbu kwenye nafasi ya
kadi ya kumbukumbu.
5. Lainisha maeneo ya mguso ya betri, na
uweke betri ndani.
6. Rejesha kifuniko cha nyuma.
Fungua kifuniko cha nyuma, ondoa betri, na uondoe SIM.
Ondoa kadi ya kumbukumbu
Fungua kifuniko cha nyuma, ondoa betri, na utoe kadi ya kumbukumbu.
Simu yako na SIM kadi hutumia misimbo tofauti ya usalama.
• Misimbo ya PIN au PIN2: Misimbo hii hulinda SIM kadi yako dhidi ya matumizi
yasiyoidhinishwa. Ukisahau misimbo au iwe haijatolewa pamoja na kadi yako, wasiliana
na mtoa huduma wa mtandao wako. Ukicharaza msimbo vibaya mara 3 zikifuatana, unahitaji
kufungua msimbo kwa kutumia msimbo wa PUK au PUK2.
• Misimbo ya PUK au PUK2: Misimbo hii inahitajika ili kufungua msimbo wa PIN au PIN2. Ikiwa
misimbo haijatolewa na SIM kadi yako, wasiliana na mtoa huduma wako wa mtandao.
• Msimbo wa usalama: Msimbo wa usalama hukusaidia kulinda simu yako dhidi ya matumizi
yasiyoidhinishwa. Unaweza kuweka simu yako kukuuliza msimbo wa usalama ambao
unafasili. Weka msimbo kuwa siri na mahali salama, kando na simu yako. Ukisahau msimbo
na simu yako imefungwa, simu yako itahitaji huduma. Huenda gharama ya ziada ikatumika,
na data yote ya kibinafsi kwenye simu huenda ikafutwa. Kwa maelezo zaidi, wasiliana na care
point iliyo karibu ya simu yako, au muuzaji wa simu yako.
• Msimbo wa IMEI: Msimbo wa IMEI hutumiwa kutambua simu katika mtandao. Huenda pia
ukahitaji kupeana nambari kwa huduma zako za care point au muuzaji wa simu. Ili kuona
nambari yako ya IMEI, piga *#06# . Msimbo wa IMEI wa simu yako umechapishwa pia kwenye
lebo ya simu yako, ambayo iko chini ya betri. IMEI inaonekana pia kwenye sanduku halisi la
mauzo.
CHAJI SIMU YAKO
Betri yako imechajiwa nusu kiwandani, lakini utahitajika kuichaji upya kabla uweze kutumia simu
yako.
Chaji betri
1. Chomeka chaja kwenye soketi ya ukuta.
2. Unganisha chaja kwenye simu. Ukimaliza, chomoa chaja kwenye simu, kisha kwenye soketi
ya ukuta.
Kama betri imeisha moto kabisa, huenda ikachukua dakika kadhaa kabla ya kiashiria chaji
kuonyeshwa.
Kidokezo: Unaweza kuchaji kwa kutumia USB wakati umeme wa ukutani haupatikani. Data
inaweza kuhamishwa ukichaji kifaa. Ubora wa nishati ya kuchaji kwa USB hutofautiana,
na huenda ikachukua muda mrefu kuchaji kuanza na kifaa kuanza kufanya kazi. Hakikisha
kompyuta yako imewashwa.
PATA MENGI KUTOKA KWA SIM KADI MBILI (SIMU ZA SIM MBILI)
Simu yako inaweza kutumia SIM kadi mbili, na unaweza kuzitumia kwa malengo tofauti.
Chagua ni SIM kadi gani itatumika
1. Chagua Menyu > > Uunganikaji > SIM Mbili .
2. Ili kuchagua ni SIM gani ya kutumia kupiga simu, chagua
SIM inayopendelewa ya kupiga simu , na uchague SIM1 au SIM2 .
3. Ili kuchagua ni SIM gani ya kutumia kutuma ujumbe, chagua SIM inayopendelewa ya ujumbe ,
na uchague SIM1 au SIM2 .
4. Ili kuchagua ni SIM gani ya kutumia kwa data ya rununu, chagua Mu. wa dat. rununu , washa
Data ya rununu , na uchague aidha SIM1 au SIM2 .
Sambaza simu kati ya SIM zako 2
Pata mengi kutoka kwa SIM kadi zako 2. Ukisambaza simu zako kati ya SIM zako, wakati mtu
anapokupigia simu kwenye SIM yako moja wakati una simu kwenye laini nyingine, unaweza
kudhibiti simu zako kutoka kwa SIM zote kama vile ungefanya na SIM moja pekee.
Hakikisha umeingiza SIM kadi 2 kwenye simu yako.
1. Chagua Menyu > > Uunganikaji > SIM Mbili > Nambari za SIM .
2. Charaza nambari za SIM zako zote na uchague Hifadhi .
3. Tembeza juu hadi Sambaza simu , na uchague Kati ya SIM mbili , Kutoka SIM1 hadi SIM2 ,
Je, una tatizo la kusikia simu yako ikiita katika mazingira yenye kelele, au simu ina sauti ya juu
sana? Unaweza kubadilisha sauti kama upendavyo.
Tembeza juu au chini ili ubadilishe sauti wakati wa simu au wakati unasikiliza redio.
ANDIKA MATINI
Andika kwa kutumia vitufe
Kuandika kwa kutumia vitufe ni rahisi.
Bonyeza kitufe kwa kurudia hadi herufi ionyeshwe.
Ili kucharaza katika nafasi bonyeza 0 .
Ili kuandika herufi maalum au alama ya kituo, bonyeza * .
Ili kubadilisha kati ya vibambo, bonyeza # kwa kurudia.
Ili kuandika nambari, bonyeza na ushikilie kitufe cha nambari.
Tumia matini ya kubashiri
Ili kuharakisha uandishi wako, simu yako inaweza kukisia unachoanza kuandika. Matini ya
kubashiri hutegemea kamusi iliyoundiwa ndani. Kipengele hiki hakipatikani kwa lugha zote.