Nokia 2.4 User guide [sw]

Nokia 2.4
Mwongozo wa mtumiaji
Toleo 2021-01-04 sw
Nokia 2.4 Mwongozo wa mtumiaji
1 Kuhusu mwongozo huu wa mtumiaji
Muhimu: Kwa maelezo muhimu kuhusu matumizi salama ya kifaa na betri yako, soma maelezo
ya ”Kwa usalama wako” na ”Usalama wa Bidhaa” katika mwongozo uliochapishwa wa mtumiaji, au kwenye www.nokia.com/support kabla utumie kifaa. Ili kujua jinsi ya kuanza kutumia kifaa chako kipya, soma mwongozo uliochapishwa wa mtumiaji.
© 2020 HMD Global Oy. Haki Zote zimehifadhiwa. 2
Nokia 2.4 Mwongozo wa mtumiaji

Yaliyomo

1 Kuhusu mwongozo huu wa mtumiaji 2
2 Yaliyomo 3
3 Anza kutumia 6
Sasisha simu yako . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . 6
Vitufe na sehemu . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . 6
Ingiza SIM na kadi za kumbukumbu . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . 7
Chaji simu yako . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . 8
Washa na usanidi simu yako . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . 9
Mipangilio ya SIM Mbili . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . 10
Funga au fungua simu yako . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . 10
Tumia skrini ya mguso . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . 11
4 Misingi 15
Binafsisha simu yako . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . 15
Arifa . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . 15
Dhibiti sauti . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . 16
Usahihishaji matini kiotomatiki . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . 17
Kisaidizi cha Google . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . 17
Maisha ya betri . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . 18
Ufikiaji . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . 19
Redio ya FM . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . 19
5 Unganika na marafiki na familia yako 21
Simu . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . 21
Anwani . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . 21
Tuma ujumbe . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . 21
Barua . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . 22
© 2020 HMD Global Oy. Haki Zote zimehifadhiwa. 3
Nokia 2.4 Mwongozo wa mtumiaji
6 Kamera 23
Misingi ya kamera . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . 23
Video . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . 23
Tumia kamera yako kama mtaalamu . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . 23
Picha na video zako . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . 24
7 Intaneti na miunganisho 25
Amilisha Wi-Fi . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . 25
Vinjari wavuti . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . 25
Bluetooth® . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . 26
VPN . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . 28
8 Panga siku yako 29
Tarehe na saa . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . 29
Saa ya kengele . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . 29
Kalenda . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . 30
9 Ramani 31
Tafuta maeneo na upate maelekezo . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . 31
Pakua na usasishe ramani . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . 31
Tumia huduma za eneo . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . 32
10 Programu, visasisho, na hifadhi nakala 33
Pata programu kutoka kwenye Google Play . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . 33
Wezesha nafasi kwenye simu yako . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . 33
Sasisha programu ya simu yako . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . 34
Hifadhi nakala ya data yako . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . 34
Rejesha mipangilio halisi na uondoe maudhui binafsi kwenye simu yako . . . . . . . . . 34
11 Linda simu yako 36
Linda simu yako kwa kufuli ya skrini . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . 36
Linda simu yako kwa kutumia alama ya kidole chako . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . 36
Linda simu yako kwa kutumia uso wako . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . 37
Badilisha msimbo wako wa PIN ya SIM . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . 37
Misimbo ya ufikiaji . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . 38
© 2020 HMD Global Oy. Haki Zote zimehifadhiwa. 4
Nokia 2.4 Mwongozo wa mtumiaji
12 Maelezo ya bidhaa na usalama 40
Kwa usalama wako . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . 40
Huduma za mtandao na gharama . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . 43
Simu za dharura . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . 43
Kuhudumia kifaa chako . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . 44
Uchakataji upya . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . 44
Alama ya pipa iliyo na mkato . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . 45
Maelezo ya betri na chaja . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . 45
Watoto wadogo . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . 46
Vifaa vya matibabu . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . 47
Vifaa vya matibabu vinavyopachikwa . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . 47
Vifaa vya kusaidia kusikia . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . 47
Linda mtoto wako dhidi ya vitu vyenye madhara . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . 47
Magari . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . 48
Mazingira yanayoweza kulipuka . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . 48
Habari ya utoaji cheti (SAR) . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . 48
Kuhusu Usimamizi wa haki za Dijitali . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . 49
Hakimiliki na ilani nyingine . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . 49
© 2020 HMD Global Oy. Haki Zote zimehifadhiwa. 5
Nokia 2.4 Mwongozo wa mtumiaji
3 Anza kutumia

SASISHA SIMU YAKO

Programu ya simu yako
Sasisha simu yako na ukubali visasisho vinavyopatikana vya programu ili upate vipengee vipya na vilivyoboreshwa vya simu yako. Kusasisha programu kunaweza pia kuboresha utendakazi wa simu yako.

VITUFE NA SEHEMU

Simu yako
Mwongozo huu wa mtumiaji hutumika kwa modeli zifuatazo: TA-1270, TA-1275, TA-1274, TA-
1277.
1. Sensa ya alama ya kidole
2. Mweko
3. Kamera
4. Kisaidizi cha Google/Kitufe cha Utafutaji wa Google*
© 2020 HMD Global Oy. Haki Zote zimehifadhiwa. 6
5. Kipenyo cha SIM na kadi ya kumbukumbu
6. Kamera ya mbele
7. Maikrofoni
8. Kifaa cha sikioni
9. Kiunganisha kifaa cha sauti
Nokia 2.4 Mwongozo wa mtumiaji
10. Vitufe vya sauti
11. Kitufe cha Nishati/Kufunga/
12. Kiunganisha USB
Baadhi ya vifaa vya ziada vilivyotajwa katika mwongozo huu wa mtumiaji, kama vile chaja, kifaa cha kichwa, au kebo ya data, huenda vikauzwa kando.
*Kisaidizi cha Google hakipatikani katika lugha na nchi zingine. Ambapo hakipatikani, Kisaidizi cha Google hubadilishwa kwa Utafutaji wa Google. Angalia upatikanaji katika https://support.google.com/assistant.
Sehemu na viunganishaji, hali ya sumaku
Usiunganishe kwenye bidhaa ambazo zinaunda ishara ya kutoa, kwa kuwa hii inaweza kuharibu kifaa. Usiunganishe chanzo chochote cha stima kwenye kiunganisha cha sauti. Ukiunganisha kifaa chochote cha nje au vifaa vyovyote vya sauti kando na vile vilivyoidhinishwa kutumiwa na kifaa hiki, Kiunganishi cha sauti, kuwa makini sana na viwango vya sauti.
Sehemu nyingine za kifaa hiki zina sumaku. Vitu vya chuma vinaweza kuvutwa na kifaa. Usiweke kadi za mkopo au kadi nyingine zenye mkanda wa sumaku karibu na kifaa kwa kipindi cha muda mrefu, kwa kuwa kadi hizo zinaweza kuharibika.
13. Maikrofoni
14. Kipaza sauti

INGIZA SIM NA KADI ZA KUMBUKUMBU

Ingiza SIM kadi
1. Fungua trei ya SIM kadi: sukuma pini ya kufungua trei ndani ya shimo la trei na uondoe trei.
2. Weka nano-SIM kwenye kipenyo cha SIM kwenye trei na eneo la mguso likiangalia chini.
3. Ikiwa una kadi ya kumbukumbu, ingiza kwenye kipenyo cha kadi ya kumbukumbu.
© 2020 HMD Global Oy. Haki Zote zimehifadhiwa. 7
Nokia 2.4 Mwongozo wa mtumiaji
Ingiza SIM ya pili
1. Ikiwa una simu ya SIM mbili, ingiza SIM ya pili kwenye kipenyo cha SIM2.
2. Telezesha trei ndani. Tumia kadi halisi ya nano-SIM tu. Matumizi ya SIM kadi zisizotangamana yanaweza kuharibu kadi au kifaa, na yanaweza kuharibu data iliyohifadhiwa kwenye kadi. Tumia tu kadi za kumbukumbu zinazotangamana zilizoidhinishwa kutumiwa na kifaa hiki. Huenda kadi zisizotangamana zikaharibu kadi na kifaa na kuharibu data iliyohifadhiwa kwenye kadi.
Kidokezo: Ili kujua ikiwa simu yako inaweza kutumia SIM kadi 2, angalia lebo kwenye sanduku la mauzo. Ikiwa kuna misimbo 2 ya IMEI kwenye lebo, una simu yenye SIM mbili.
Muhimu: Usiondoe kadi ya kumbukumbu wakati programu inaitumia. Kufanya hivyo kunaweza kuharibu kadi ya kumbukumbu na kuharibu data iliyohifadhiwa kwenye kadi.
Kidokezo: Tumia kadi ya kumbukumbu ya microSD yenye kasi, na ya hadi GB 512 kutoka kwa mtengenezaji anayefahamika.

CHAJI SIMU YAKO

Chaji betri
© 2020 HMD Global Oy. Haki Zote zimehifadhiwa. 8
Nokia 2.4 Mwongozo wa mtumiaji
1. Chomeka chaja inayotangamana kwenye soketi ya ukuta.
2. Unganisha kebo kwenye simu yako.
Simu yako inakubali kebo ya USB ya micro-B. Pia unaweza kuchaji simu yako kutoka kwenye kompyuta kwa kutumia kebo ya USB, lakini inaweza kuchukua muda mrefu zaidi.

WASHA NA USANIDI SIMU YAKO

Wakati unapowasha simu yako kwa mara ya kwanza, simu yako hukuelekeza usanidi miunganisho ya mtandao na mipangilio ya simu yako.
Washa simu yako
1. Kuwasha simu yako, bonyeza na ushikilie kitufe cha nishati hadi simu iteteme.
2. Wakati simu imewashwa, chagua lugha na eneo lako.
3. Fuata maagizo yaliyoonyeshwa kwenye simu yako.
Hamisha data kutoka kwenye simu yako ya awali
Huwezi kuhamisha data kutoka kwenye simu yako ya zamani hadi kwenye simu yako mpya kwa kutumia akaunti ya Google
Ili kuhifadhi nakala ya data kwenye simu yako ya zamani kwenye akaunti yako ya Google, rejelea mwongozo wa mtumiaji wa simu yako ya zamani.
1. Gusa Mipangilio > Akaunti > Ongeza akaunti > Google .
2. Chagua ni data gani unayotaka irejeshwe kwenye simu yako mpya. Usawazishaji huanza kiotomatiki punde simu yako inapounganishwa kwenye intaneti.
Rejesha mipangilio ya programu kutoka kwenye simu yako ya awali ya Android™
Ikiwa simu yako ya awali ilikuwa ya Android, na uhifadhi nakala ya akaunti ya Google kwayo, unaweza kurejesha mipangilio ya programu yako na manenosiri ya Wi-Fi.
1. Gusa Mipangilio > Mfumo > Hifadhi nakala rudufu .
2. Badilisha Hifadhi nakala kwenye Google Drive kwa Washa .
© 2020 HMD Global Oy. Haki Zote zimehifadhiwa. 9
Nokia 2.4 Mwongozo wa mtumiaji

MIPANGILIO YA SIM MBILI

Ikiwa una simu ya SIM mbili, unaweza kuwa na SIM 2 kwenye simu yako, kwa mfano, moja ya kazi yako na nyingine ya matumizi yako ya kibinafsi.
Chagua ni SIM gani ya kutumia
Kwa mfano, wakati unapiga simu, unaweza kuchagua ni SIM gani ya kutumia kwa kugusa kitufe kinacholingana cha SIM 1 au SIM 2 baada ya kupiga nambari hiyo.
Simu yako huonyesha hali ya mtandao ya SIM zako kitofauti. SIM kadi zote zinapatikana kwa wakati mmoja wakati kifaa hakitumiki, lakini wakai SIM kadi moja inatumika, kwa mfano, wakati wa kupiga simu, ile nyingine inawezakosa kupatikana.
Dhibiti SIM zako
Hutaki kazi iingiliane na muda wako huru? Au una muunganisho wa bei nafuu wa data kwenye SIM moja? Unaweza kuamua ni SIM gani unayotaka kutumia.
Gusa Mipangilio > Mtandao na Intaneti > SIM Kadi .
Badili jina la SIM kadi
Gusa SIM unayotaka kubadilisha jina, na uandike jina unalotaka.
Chagua ni SIM gani ya kutumia kwa simu au muunganisho wa data
Chini ya SIM unayopendelea ya , gusa mpangilio unaotaka kubadilisha na uchague SIM.

FUNGA AU FUNGUA SIMU YAKO

Funga simu yako
Kiwa unataka kuepuka kupiga simu kwa makosa wakati simu yako iko kwenye mfuko au begi lako, unaweza kufunga vitufe na skrini yako.
Ili kufunga vitufe na skrini yako, bonyeza kitufe cha nishati.
Fungua vitufe na skrini
Bonyeza kitufe cha nishati, na utelezeshe juu kwenye skrini. Ukiulizwa, toa hati tambulishi za ziada.
© 2020 HMD Global Oy. Haki Zote zimehifadhiwa. 10
Nokia 2.4 Mwongozo wa mtumiaji

TUMIA SKRINI YA MGUSO

Muhimu: Epuka kugwara skrini ya mguso. Usitumie kamwe kalamu, penseli halisi, au kitu
kingine chenye ncha kali kwenye skrini ya mguso.
Gusa na ushikilie ili kukokota kipengee
Weka kidole chako kwenye kipengee kwa sekunde chache, na utelezeshe kidole chako kwenye skrini.
© 2020 HMD Global Oy. Haki Zote zimehifadhiwa. 11
Nokia 2.4 Mwongozo wa mtumiaji
Pitisha
Weka kidole chako kwenye skrini, na utelezeshe kidole chako kwenye mweleko unaotaka.
Tembeza kwenye orodha au menyu ndefu
Telezesha kidole chako kwa haraka katika mwelekeo wa juu au chini kwenye skrini, na uinue kidole chako. Ili kukomesha kutembeza, gusa skrini.
© 2020 HMD Global Oy. Haki Zote zimehifadhiwa. 12
Nokia 2.4 Mwongozo wa mtumiaji
Kuza ndani au nje
Weka vidole 2 kwenye kipengee, kama vile ramani, picha, au ukurasa wavuti, na utelezeshe vidole vako vikiwa kando au pamoja.
Funga mwelekeo wa skrini
Skrini huzunguka kiotomatiki wakati unapindua simu kwa digrii 90.
Kufunga skrini katika hali ya wima, telezesha chini kutoka upande wa juu wa skrini, na uguse
Zungusha kiotomatiki .
Rambaza kwa kutumia ishara
Kuwasha kwa kutumia urambazaji wa ishara, gusa Mipangilio > Mfumo > Ishara >
Urambazaji wa mfumo > Urambazaji wa ishara .
• Ili kuona programu zako zote, telezesha
kisha uondoe kidole chako.
juu kuanzia chini ya skrini.
• Ili kubadilisha kwa programu nyingine
• Ili kwenda kwenye skrini ya mwanzo,
iliyofunguliwa, gusa programu. telezesha juu kutoka chini ya skrini. Programu uliyokuwa ukitumia hubakia imefunguliwa chinichini.
• Ili kufunga programu zote zilizofunguliwa, telezesha kulia kupitia programu zote, na uguse FUTA ZOTE .
• Kuona programu gani umefungua, telezesha juu kutoka chini ya skrini bila kutoa kidole chako hadi uone programu,
• Ili urudi kwenye skrini ya awali ambayo ulikuwa unatumia, telezesha kutoka
© 2020 HMD Global Oy. Haki Zote zimehifadhiwa. 13
Nokia 2.4 Mwongozo wa mtumiaji
upande wa kulia au kushoto ya skrini. simu yako hukumbuka programu na tovuti zote
ulizotembelea tangu wakati wa mwisho skrini yako ilipofungwa.
Rambaza kwa kutumia vitufe
Kuwasha vitufe vya urambazaji, gusa Mipangilio > Mfumo > Ishara > Urambazaji wa mfumo > Urambazaji wa vitufe 3 .
• Ili kuona programu zako zote, pitisha juu
programu.
kwenye kitufe cha mwanzo .
• Ili kufunga programu zote zilizofunguliwa,
• IIi kwenda kwenye skrini ya mwanzo, gusa kitufe cha mwanzo. Programu uliyokuwa
telezesha kulia kupitia programu zote, na uguse FUTA ZOTE .
ukitumia hubakia imefunguliwa chinichini.
• Ili kurejesha kwenye skrini ya awali
• Ili kuona ni programu gani ulizofungua, gusa .
• Ili kubadilisha kwa programu nyingine iliyofunguliwa, telezesha kulia na uguse
uliyokuwa, gusa . simu yako hukumbuka programu na tovuti zote ulizotembelea tangu wakati wa mwisho skrini yako ilipofungwa.
© 2020 HMD Global Oy. Haki Zote zimehifadhiwa. 14
Nokia 2.4 Mwongozo wa mtumiaji
4 Misingi

BINAFSISHA SIMU YAKO

Badilisha mandhari yako
Gusa Mipangilio > Skrini > Mandhari .
Badilisha mlio wa simu yako
Gusa Mipangilio > Sauti > Mlio wa simu wa SIM1 au Mlio wa simu wa SIM2 , na uchague mlio.
Badilisha sauti ya taarifa ya ujumbe wako
Gusa Mipangilio > Sauti > Mipangilio ya kina > Sauti chaguo-msingi ya arifa .

ARIFA

Tumia paneli ya taarifa
Unapopokea arifa mpya, kama vile ujumbe au simu zisizojibiwa, aikoni ya kiashiriaji huonekana kwenye upau wa hali juu ya skrini. Ili kuona maelezo zaidi kuhusu arifa, kokota chini upau wa hali. Ili kufunga mwonekano, pitisha juu kwenye skrini.
Ili kufungua paneli ya arifa, kokota upau wa hali chini. Ili kufunga paneli ya arifa, pitisha juu kwenye skrini.
Ili kubadilisha mipangilio ya taarifa ya programu, gusa Mipangilio > Programu na arifa > na uguse jina la programu ili ufungue mipangilio ya programu. Gusa Arifa . Unaweza kuzima au kuwasha arifa kwa kila programu kivyake.
© 2020 HMD Global Oy. Haki Zote zimehifadhiwa. 15
Nokia 2.4 Mwongozo wa mtumiaji
Tumia ikoni za mpangilio wa haraka
Ili kuamilisha vipengele, gusa ikoni za mipangilio ya haraka kwenye paneli ya arifa. Ili kuona ikoni zaidi, kokoa menyu chini.
Ili kupanga upya ikoni, gusa , gusa na ushikilie ikoni, na uikokote kwenye eneo lingine.

DHIBITI SAUTI

Badilisha sauti
Ikiwa una tatizo la kusikia simu yako ikiita katika mazingira yenye kelele, au simu ina sauti ya juu, unaweza kubadilisha sauti kama upendavyo kwa kutumia vitufe vya sauti upande wa simu yako.
Usiunganishe kwenye bidhaa ambazo zinaunda ishara ya kutoa, kwa kuwa hii inaweza kuharibu kifaa. Usiunganishe chanzo chochote cha stima kwenye kiunganisha cha sauti. Ukiunganisha kifaa chochote cha nje au vifaa vyovyote vya sauti kando na vile vilivyoidhinishwa kutumiwa na kifaa hiki, Kiunganishi cha sauti, kuwa makini sana na viwango vya sauti.
Badilisha sauti ya midia na programu
Bonyeza kitufe cha sauti upande wa simu yako ili uone upau wa hali ya sauti, gusa , na ukokote kitelezi kwenye upau wa sauti kwa midia na programu kushoto au kulia.
Weka simu kimya
Ili kuweka simu kuwa kimya, bonyeza kitufe cha kupunguza zaidi, gusa ili uweke simu yako kutetema pekee na uguse ili kuiweka kimya.
© 2020 HMD Global Oy. Haki Zote zimehifadhiwa. 16
Nokia 2.4 Mwongozo wa mtumiaji

USAHIHISHAJI MATINI KIOTOMATIKI

Jifunze jinsi ya kuandika maandishi kwa haraka na vizuri kwa kutumia usahihishaji matini wa kibodi.
Tumia mapendekezo ya neno la kibodi
Simu yako hupendekeza maneno unapokuwa ukiandika, ili kukusaidia kuandika kwa haraka na kwa usahihi zaidi. Mapendekezo ya maneno yanaweza kutopatikana katika lugha zote.
Wakati unapoanza kuandika neno, simu yako itapendekeza maneno yanayowezekana. Neno unalotaka likionyeshwa kwenye upau wa mapendekezo, chagua neno. Ili kuona mapendekezo zaidi, gusa na ushikilie pendekezo.
Dokezo: Ikiwa neno lililopendekezwa limewekwa alama ya koza, simu huitumia kiotomatiki ili kubadilisha neno uliloandika. Ikiwa neno si sahihi, gusa na ushikilie ili kuona mapendekezo mengine machache. Ikiwa hutaki kibodi kupendekeza maneno unapokuwa ukicharaza, zima sahihisho za matini. Gusa Mipangilio > Mfumo > Lugha na ingizo > Kibodi pepe . Teua kibodi unayotumia kwa kawaida. Gusa Usahihishaji matini na uzime mbinu za kusahihisha matini ambayo hutaki kutumia.
Sahihisha neno
Ukigundua ya kwamba umekosea tahajia ya neno, gusa ili kuona mapendekezo ya kusahihisha neno.
Zima kikagua tahajia
Gusa Mipangilio > Mfumo > Lugha na ingizo > Mipangilio ya kina > Kikagua tahajia , na uzime Tumia kikagua tahajia .

KISAIDIZI CHA GOOGLE

Kisaidizi cha Google hupatikana katika masoko na lugha zilizoteuliwa pekee. Ambapo hakipatikani, Kisaidizi cha Google hubadilishwa kwa Utafutaji wa Google. Kisaidizi cha Google kinaweza kukusaidia kwa mfano, kutafuta maelezo mtandaoni, kutafsiri maneno na sentensi, kuandika vidokezo na uteuzi wa kalenda. Unaweza kutumia Kisaidizi cha Google hata wakati simu yako imefungwa. Hata hivyo, Kisaidizi cha Google hukuomba ufungue simu yako kabla ya kufikia data yako ya kibinafsi.
© 2020 HMD Global Oy. Haki Zote zimehifadhiwa. 17
Nokia 2.4 Mwongozo wa mtumiaji
Tumia kitufe cha Kisaidizi cha Google
Ili kufikia huduma za Kisaidizi cha Google, tumia kitufe cha Kisaidizi cha Google upande wa simu yako:
• Bonyeza kitufe mara moja ili kuanzisha Kisaidizi cha Google.
• Bonyeza na ushikilie kitufe mara moja ili kuzungumza na Kisaidizi cha Google. Uliza swali lako na uachilie kitufe. Utaona jibu la Kisaidizi cha Google kwenye skrini ya simu yako.
Ikiwa nchi au eneo lako halikubali Kisaidizi cha Google, bado unaweza kutumia kitufe cha Kisaidizi cha Google:
• Bonyeza kitufe mara moja ili kufungua utafutaji wa Google.
• Bonyeza na ushikilie kitufe ili kutumia utafutaji wa sauti ya Google. Uliza swali lako na uachilie kitufe. Utaona jibu la Google kwenye skrini ya simu yako.

MAISHA YA BETRI

Pata mengi kutoka kwa simu yako ukipata maisha ya betri unayotaka. Kuna hatua unazoweza kuchukua kuokoa nishati kwenye simu yako.
Ongeza maisha ya betri
Kuokoa nishati:
1. Daima chaji betri kabisa.
2. Nyamazisha sauti zisizohitajika, kama vile sauti za mguso. Gusa Mipangilio >
Sauti > Mipangilio ya kina , na chini ya Sauti na mitetemo mingine , chagua ni
sauti gani za kuweka.
3. Tumia vifaa vya sauti vyenye waya, badala ya kipasa sauti.
4. Weka skrini ya simu ili kuzima baada ya muda mfupi. Gusa Mipangilio > Skrini > Mipangilio ya kina >
Muda wa kuisha wa skrini na uchague
muda.
5. Gusa Mipangilio > Skrini >
Hali ya mwangaza . Ili kurekebisha
mwangaza, kokota kitelezi cha hali ya mwangaza. Hakikisha kwamba
Mwangaza uliorekebishwa umezimwa.
6. Komesha programu zinazoendeshwa
kichini chini: gusa , telezesha kulia kwenye programu zote na uguse
FUTA ZOTE .
7. Tumia huduma za eneo kwa kuchagua: zima huduma za eneo wakati hauzihitaji. Gusa Mipangilio > Eneo , na ulemaze
Tumia eneo .
8. Tumia miunganisho ya mtandao kwa kuchagua: washa Bluetooth wakati inahitajika tu. Tumia muunganisho wa Wi-Fi ili uunganishe kwenye intaneti, badala ya muunganisho wa data ya
© 2020 HMD Global Oy. Haki Zote zimehifadhiwa. 18
Nokia 2.4 Mwongozo wa mtumiaji
simu. Komesha simu yako kutafuta mitandao inayopatikana ya pasi waya. Gusa Mipangilio > Mtandao na intaneti > Wi-Fi , na ulemaze Tumia Wi-Fi . Kama unasikiliza muziki au unatumia simu yako, lakini hutaki kupiga au kupokea simu,
washa hali ya ndege. Gusa Mipangilio >
Mtandao na Intaneti > Hali ya ndege . Hali ya ndege hufunga miunganisho kwenye mitandao ya simu za mkononi na huzima vipengele pasiwaya vya kifaa chako.

UFIKIAJI

Unaweza kubadilisha mipangilio mbalimbali ili kufanya kutumia simu yako kuwa rahisi.
Ongeza au upunguze ukubwa wa fonti
Ungependa kuwa na fonti kubwa kwenye simu yako?
1. Gusa Mipangilio > Ufikiaji .
2. Gusa Ukubwa wa maandishi . Ili kuongeza au kupunguza ukubwa wa fonti, kokota kitelezi cha kiwango cha ukubwa wa fonti.
Ongeza au upunguze ukubwa wa maandishi
Ungependa kufanya vipengee hivi kwenye skrini kuwa ndogo au kubwa?
1. Gusa Mipangilio > Ufikiaji .
2. Gusa Ukubwa wa skrini na urekebishe ukubwa wa mandishi, kokota kitelezi kiwango cha ukubwa wa skrini.

REDIO YA FM

Kusikiliza redio, unahitaji kuunganisha vifaa vinavyotangamana vya sauti kwenye simu. Vifaa vya sauti hufanya kazi kama antena. Kifaa cha kichwa kinaweza kuuzwa kando.
Sikiliza redio ya FM
Baada ya kuunganisha vifaa vya sauti, gusa Redio ya FM .
• Kuwasha redio, gusa
• Kupata vituo vya redio, gusa >
© 2020 HMD Global Oy. Haki Zote zimehifadhiwa. 19
Changanua .
• Kubadilisha kwenye kituo kingine,
Nokia 2.4 Mwongozo wa mtumiaji
telezesha mstari wa mawimbi ya idhaa upande wa kushoto au kulia.
• Kuhifadhi kituo, gusa .
Kidokezo cha utatuzi: Ikiwa redio haifanyi kazi, hakikisha kifaa cha kichwa kimeunganishwa vizuri.
• Kusikiliza kituo cha redio ukitumia spika
za simu, gusa . Hakikisha kifaa cha sauti kimeunganishwa.
• Kuzima redio, gusa
© 2020 HMD Global Oy. Haki Zote zimehifadhiwa. 20
Nokia 2.4 Mwongozo wa mtumiaji
5 Unganika na marafiki na familia yako

SIMU

Piga simu
1. Gusa .
2. Gusa na ucharaze nambari, au gusa na uchague jina unalotaka kupigia simu.
3. Gusa . Ikiwa umeingiza SIM kadi ya pili, gusa aikoni inayolingana ili kupiga simu kutoka kwa SIM hiyo.
Jibu simu
Wakati simu inaita, gusa JIBU .
Kataa simu
Ili kukataa simu inayoingia, gusa KATAA .

ANWANI

Hifadhi jina kutoka kwenye historia ya simu
1. Gusa > ili uone historia ya simu yako.
2. Gusa nambari unayotaka kuhifadhi.
3. Gusa Ongeza anwani . Ikiwa hii ni anwani mpya, charaza maelezo ya anwani, na uguse Hifadhi . Ikiwa anwani hii tayari iko kwenye orodha yako ya anwani, gusa
Ongeza kwa zilizopo , chagua anwani, na uguse Hifadhi .
Ongeza jina
1. Gusa Anwani > .
2. Jaza maelezo.
3. Gusa Hifadhi .

TUMA UJUMBE

Tuma ujumbe
© 2020 HMD Global Oy. Haki Zote zimehifadhiwa. 21
Nokia 2.4 Mwongozo wa mtumiaji
1. Gusa Barua pepe .
2. Gusa Anza soga .
3. Ili kuongeza mpokeaji, gusa , andika nambari yake, na uguse . Ili kuongeza mpokeaji kutoka kwenye orodha yako ya anwani, anza kuandika jina lake na uguse jina.
4. Ili kuongeza wapokeaji zaidi, gusa .
Baada ya kuchagua wapokeaji wote, gusa .
5. Andika ujumbe wako katika kisanduku cha ujumbe.
6. Gusa .

BARUA

Unaweza kutuma barua kwa kutumai simu yako ukiwa mahali popote.
Ongeza akaunti ya barua
Wakati unatumia programu ya Gmail kwa mara ya kwanza, utaulizwa usanidi akaunti yako ya barua pepe.
1. Gusa Gmail .
2. Unaweza kuchagua anwani iliyounganishwa na akaunti yako ya Google au gusa Ongeza anwani ya barua pepe .
3. Baada ya kuongeza akaunti zote, gusa NIPELEKE KWA GMAIL .
Tuma barua
1. Gusa Gmail .
2. Gusa .
3. Katika kisanduku cha Kwa ,
charaza anwani, au gusa >
Ongeza kutoka kwenye Anwani .
4. Charaza mada ya ujumbe na barua.
5. Gusa .
© 2020 HMD Global Oy. Haki Zote zimehifadhiwa. 22
Nokia 2.4 Mwongozo wa mtumiaji
6 Kamera

MISINGI YA KAMERA

Piga picha
Piga picha nzuri na maridadi – nasa nyakati bora katika albamu ya picha yako.
1. Gusa Kamera .
2. Lenga unachotaka kupiga picha.
3. Gusa .
Jipige picha
1. Gusa Kamera > ili ubadilishe kwa kamera ya mbele.
2. Gusa .
Piga picha za panorama
1. Gusa Kamera .
2. Gusa > Panorama .
3. Gusa na ufuate maagizo kwenye simu yako.

VIDEO

Rekodi video
1. Gusa Kamera .
2. Ili kubadilisha hali ya kurekodi video, gusa Video .
3. Gusa ili kuanza kurekodi.
4. Kukomesha kurekodi, gusa .
5. Kurudi kwenye hali ya kamera, gusa Picha .

TUMIA KAMERA YAKO KAMA MTAALAMU

Jifunze kuhusu mipangilio yako ya kamera
Katika programu ya Kamera, gusa ili kujifunza mengi kuhusu kila mpangilio.
© 2020 HMD Global Oy. Haki Zote zimehifadhiwa. 23
Nokia 2.4 Mwongozo wa mtumiaji
Weka ukungu nyuma ya picha yako
Ikiwa unataka kuweka ukungu kwenye mandharinyuma ya picha yako, chagua hali ya picha wima na ujaribu athari tofauti za kuweka ukungu katika mandharinyuma. Unaweza pia kutumia hali ya picha wima kupiga picha binafsi.
1. Gusa Kamera > Wima > .
2. Gusa hali na utumie kitelezi kuchagua jinsi unavyotaka sana kuweka athari hiyo.
3. Gusa .
Piga picha usiku
Ili kupiga picha zenye ubora wa juu usiku au katika hali ya mwangaza hafifu, washa hali ya usiku.
1. Gusa Kamera > Usiku .
2. Gusa .

PICHA NA VIDEO ZAKO

Tazama picha na video kwenye simu yako
Gusa Picha .
Nakili picha na video zako kwenye kompyuta yako
Ungependa kutazama picha na video zako kwenye skrini kubwa? Zisogeze kwenye kompyuta yako.
Unaweza kutumia kidhibiti faili cha kompyuta yako kunakili au kusogeza picha na video zako kwenye kompyuta.
Unganisha simu yako kwenye kompyuta na kebo ya USB inayotangamana. Ili kuweka aina ya muunganisho wa USB, fungua paneli ya taarifa, na uguse taarifa ya USB.
Shiriki picha na video zako
1. Gusa Picha , gusa picha unayotaka kushiriki na uguse .
2. Chagua jinsi unavyotaka kushiriki picha au video.
© 2020 HMD Global Oy. Haki Zote zimehifadhiwa. 24
Nokia 2.4 Mwongozo wa mtumiaji
7 Intaneti na miunganisho

AMILISHA WI-FI

Kutumia muunganisho wa Wi-Fi kwa kawaida huwa haraka na bei nafuu kuliko kutumia muunganisho wa data ya simu. Kama miunganisho yote ya Wi-Fi na data ya simu inapatikana, simu hutumia muunganisho wa Wi-Fi.
Washa Wi-Fi
1. Gusa Mipangilio > Mtandao na intaneti > Wi-Fi .
2. Washa Tumia Wi-Fi .
3. Chagua muunganisho unaotaka kutumia.
Muunganisho wako wa Wi-Fi unatumika wakati imeonyeshwa kwenye upau wa hali juu ya skrini.
Muhimu: Tumia usimbuaji ili kuongeza usalama wa muunganisho wako wa Wi-Fi. Kutumia usimbuaji hupunguza hatari ya wengine kufikia data yako.
Dokezo: Ikiwa unataka kufuatilia maeneo wakati mawimbi ya setileti hayapatikani, kwa mfano wakati uko ndani au kati ya majengo marefu, washa Wi-fi ili uboreshe usahihi wa mkao.
Kumbuka: Kutumia Wi-Fi huenda kumezuiwa katika nchi zingine. Kwa mfano, katika Ulaya, unaruhusiwa tu kutumia 5150-5350 MHz Wi-Fi ukiwa ndani tu, na nchini Marekani na Kanada, unaruhusiwa kutumia
5.15-5.25 GHz Wi-Fi ukiwa ndani tu. Kwa maelezo zaidi, wasiliana na utawala wa eneo lako.
Muhimu: Tumia usimbuaji ili kuongeza usalama wa muunganisho wako wa Wi-Fi. Kutumia usimbuaji hupunguza hatari ya wengine kufikia data yako.

VINJARI WAVUTI

Tumia simu yako kuunganisha kompyuta yako kwenye wavuti
Ni rahisi kutumia intaneti kwenye kompyuta yako ndogo mahali popote. Fanya simu yako iwe mtandao-hewa wa Wi-Fi, na utumie muunganisho wako wa data ya simu ili ufikie intaneti kwenye kompyuta yako ndogo au kifaa kingine.
1
1. Gusa Mipangilio > Mtandao na Intaneti > Kusambaza intaneti na kushiriki .
2. Washa Sambaza intaneti ya Wi-Fi ili ushiriki muunganisho wako wa data ya simu
kwenye Wi-Fi, Shiriki intaneti kwa USB ili kutumia muunganisho wa USB, au
Shiriki intaneti kwa Bluetooth ili utumie Bluetooth.
Kifaa kile kingine hutumia data kutoka kwa mpango wako wa data, ambayo inaweza kusababisha gharama ya matumizi ya data. Kwa maelezo kuhusu upatikanaji na gharama, wasiliana na mtoa huduma wa mtandao wako.
© 2020 HMD Global Oy. Haki Zote zimehifadhiwa. 25
Nokia 2.4 Mwongozo wa mtumiaji
Anza kuvinjari
Hakuna haja ya kompyuta – unaweza kuvinjari intaneti kwa urahisi kwenye simu yako. Jifahamishe juu ya habari, na tembelea tovuti zako uzipendazo. Unaweza kutumia kivinjari kwenye simu yako ili utazame kurasa za wavuti kwenye intaneti.
1. Gusa Chrome .
2. Charaza anwani ya wavuti na uguse .
Dokezo: Kama mtoa huduma wako wa mtandao hakulipishi ada moja kwa uhamishaji data, ili kuokoa gharama ya data, tumia mtandao wa Wi-Fi ili kuunganisha kwenye tovuti.
Tafuta wavuti
Chunguza wavuti na ulimwengu wa nje kwa kutumia Utafutaji wa Google. Unaweza kutumia kibodi kuandika maneno yako ya utafutaji.
Katika Chrome,
1. Gusa upau wa utafutaji.
2. Andika neno lako la utafutaji katika kisanduku cha utafutaji.
3. Gusa .
Unaweza pia kuchagua neno la kutafuta kutoka kwenye matokeo yanayopendekezwa.

BLUETOOTH®

Unaweza kuuunganisha pasi waya kwenye vifaa vingine vinavyotangamana, kama vile simu, kompyuta, vifaa vya sauti, na vifaa vya gari. Unaweza pia kutuma picha zako kwa simu zinazotangamana au kwenye kompyuta yako.
Unganisha kwa kifaa cha Bluetooth
Unaweza kuunganisha simu yako na vifaa vingi muhimu vya Bluetooth. Kwa mfano, na vifaa vya sauti vya pasi waya (kinauzwa kando), unaweza kuongea na simu bila kutumia mikono - unaweza kuendelea unachofanya, kama kufanya kazi kwenye kompyuta, wakati wa simu. Kuunganisha simu kwenye kifaa cha Bluetooth huitwa kuoanisha.
© 2020 HMD Global Oy. Haki Zote zimehifadhiwa. 26
Nokia 2.4 Mwongozo wa mtumiaji
1. Gusa Mipangilio > Vifaa vilivyounganishwa > Mapendeleo ya muunganisho > Bluetooth .
2. Badilisha Bluetooth kwa Washa .
3. Hakikisha kifaa kingine kimewashwa.
Huenda ukahitajika kuanzisha mchakato wa kuoanisha kutoka kwenye kifaa kingine. Kwa maelezo zaidi, angalia mwongozo wa
Kwa kuwa vifaa vyenye teknolojia pasi waya ya Bluetooth huwasiliana kwa kutumia mawimbi ya redio, havihitaji kuwa vinaangaliana. Hata hivyo, lazima vifaa vyako vya Bluetooth viwe mita 10 (futi 33) na kifaa kile kingine, ijapokuwa muunganisho unaweza kuathiriwa na vizuizi kama vile kuta au kutoka vifaa vingine vya elektroniki.
vifaa vilivyolinganishwa vinaweza bado kuunganishwa kwenye simu yako wakati Bluetooth imewashwa. Vifaa vingine vinaweza kugundua simu yako tu ikiwa mwonekano wa mipangilio ya Bluetooth imefunguliwa.
kifaa hicho kingine.
4. Gusa Oanisha kifaa kipya na uguse kifaa unachokata kuoanisha kutoka kwenye orodha ya vifaa vilivyogunduliwa vya Bluetooth.
5. Huenda ukahitaji kucharaza nenosiri. Kwa maelezo zaidi, angalia mwongozo wa kifaa hicho kingine.
Usilinganishe au kukubali maombi ya muunganisho kutoka kwa kifaa kisichojulikana. Hii husaidia kulinda simu yako dhidi ya maudhui mabaya.
Shiriki maudhui yako kwa kutumia Bluetooth
Ikiwa unataka kushiriki picha zako au maudhui mengine na rafiki, zitume kwenye simu ya rafiki yako kwa kutumia Bluetooth,
Unaweza kutumia zaidi ya muunganisho mmoja wa Bluetooth kwa wakati mmoja. Kwa mfano, wakati unatumia vifaa vya sauti vya Bluetooth, unaweza bado kutuma vitu vingine kwenye simu nyingine.
1. Gusa Mipangilio > Vifaa vilivyounganishwa > Mapendeleo ya muunganisho > Bluetooth .
2. Hakikisha Bluetooth imewashwa katika
simu zote na simu zinaonekana.
3. Nenda kwenye maudhui unayotaka
kutuma, na uguse > Bluetooth .
4. Kwenye orodha ya vifaa vilivyopatikana vya Bluetooth, gusa simu ya rafiki yako.
5. Ikiwa simu inahitaji msimbosiri, uuandike au kubali msimbosiri, na uguse Oanisha .
Msimbosiri hutumika tu wakati unaunganisha kifaa kwa mara ya kwanza.
Ondoa uoanishaji
Ikiwa huna kifaa ulichooanisha na simu yako, unaweza kuondoa uoanishaji huo.
© 2020 HMD Global Oy. Haki Zote zimehifadhiwa. 27
Nokia 2.4 Mwongozo wa mtumiaji
1. Gusa Mipangilio > Vifaa vilivyounganishwa > Vifaa vilivyounganishwa awali .
2. Gusa kando ya jina la kifaa.
3. Gusa SAHAU .
VPN
Huenda ukahitaji muunganisho wa mtandao pepe wa binafsi (VPN) ili kufikia rasilimali za kampuni yako, kama vile intraneti au barua ya kampuni, au utumie huduma ya VPN kwa malengo ya kibinafsi.
Wasiliana na msimamizi wa IT wa kampuni yako kwa maelezo ya usanidi wa VPN yako, au kukagua tovuti ya huduma ya VPN yako kwa maelezo zaidi.
Tumia muunganisho salama wa VPN
1. Gusa Mipangilio > Mtandao na Intaneti > Mipangilio ya kina > VPN .
2. Ili kuongeza wasifu wa VPN, gusa .
3. Charaza maelezo ya wasifu kama ilivyoagizwa na msimamizi wa IT wa kampuni yako au huduma ya VPN.
Hariri wasifu wa VPN
1. Gusa kando ya jina la wasifu.
2. Badilisha maelezo kama inavyohitajika.
Futa wasifu wa VPN
1. Gusa kando ya jina la wasifu.
2. Gusa SAHAU .
© 2020 HMD Global Oy. Haki Zote zimehifadhiwa. 28
Nokia 2.4 Mwongozo wa mtumiaji
8 Panga siku yako

TAREHE NA SAA

Weka tarehe na saa
Gusa Mipangilio > Mfumo > Tarehe na saa .
Sasisha saa na tarehe kiotomatiki
Unaweza kuweka simu yako kusasisha saa, tarehe, na ukanda wa saa kiotomatiki. Usasishaji otomatiki ni huduma ya mtandao na huenda usipatikane kulingana na eneo lako au mtoa huduma wa mtandao.
1. Gusa Mipangilio > Mfumo > Tarehe na saa .
2. Washa Tumia muda uliopeanwa wa mtandao .
3. Washa Saa za eneo, kiotomatiki .
Badilisha saa kuwa fomati ya saa 24
Gusa Mipangilio > Mfumo > Tarehe na Saa , na uwashe Tumia mpangilio wa saa 24 .

SAA YA KENGELE

Weka kengele
1. Gusa Saa > Kengele .
2. Ili kuongeza kengele, gusa .
3. Ili kurekebisha kengele, iguse. Ili kuweka kengele kujirudia katika tarehe maalum, weka tiki kwenye Rudia na uangazie siku za wiki.
Zima kengele
Wakati kengele inapotoa sauti, pitisha kengele kulia.
© 2020 HMD Global Oy. Haki Zote zimehifadhiwa. 29
Nokia 2.4 Mwongozo wa mtumiaji

KALENDA

Dhibiti kalenda
Gusa Kalenda > , na uchague aina ya kalenda unayotaka kuona.
Kalenda huongezwa kiotomatiki wakati unapoongeza akaunti kwenye simu yako. Ili kuongeza akaunti mpya na kalenda, nenda kwenye menyu ya programu na uguse Mipangilio > Akaunti >
Ongeza akaunti .
Ongeza tukio
1. Gusa Kalenda > .
2. Charaza maelezo unayotaka, na uweke saa.
3. Ili kufanya tukio lijirudie siku fulani, gusa
Isijirudie , na uchague ni mara ngapi tukio
Dokezo: Ili kuhariri tukio, gusa tukio na , na uhariri maelezo.
Futa miadi
1. Gusa tukio.
2. Gusa > Futa .
linapaswa kujirudia.
4. Ili kuweka ukumbusho, gusa Ongeza arifa , weka saa na uguse Imekamilika ,
5. Gusa Hifadhi .
© 2020 HMD Global Oy. Haki Zote zimehifadhiwa. 30
Nokia 2.4 Mwongozo wa mtumiaji
9 Ramani

TAFUTA MAENEO NA UPATE MAELEKEZO

Pata mahali
Ramani za Google hukusaidia kupata maeneo na biashara mahsusi.
1. Gusa Ramani .
2. Andika maneno ya kutafuta, kama vile anwani ya mtaa au jina la mahali, katika upau wa utafutaji.
3. Chagua kipengee kwenye orodha ya matokeo yanayopendekezwa unapokuwa ukiandika, au gusa ili kutafuta.
Eneo huonyeshwa kwenye ramani. Ikiwa hakuna matokeo ya utafutaji yatakayopatikana, hakikisha tahajia ya maneno yako ya utafutaji ni sahihi.
Angalia eneo lako la sasa
Gusa Ramani > .
Pata maelekezo ya mahali
1. Gusa Ramani na uingize unakoenda katika upau wa utafutaji.
2. Gusa Maelekezo . Ikoni iliyoangaziwa huonyesha hali ya usafiri, kwa mfano . Ili kubadilisha modi hii, chagua modi mpya chini ya upau wa utafutaji.
3. Kama hutaki mahali pa kuanza kuwa eneo lako la sasa, gusa Eneo lako , na utafute mahali pengine pa kuanza.
4. Gusa Anza ili kuanza urambazaji.
Njia huonyeshwa kwenye ramani, pamoja na makadirio ya muda unaochukua kufika hapo. Ili kuona maelekezo ya kina, gusa Hatua na zaidi .

PAKUA NA USASISHE RAMANI

Pakua ramani
Hifadhi ramani mpya kwenye simu yako kabla ya safari, ili uweze kuvinjari ramani bila muunganisho wa intaneti wakati unasafiri.
1. Gusa Ramani > > Ramani za nje ya mtandao > CHAGUA RAMANI YAKO MWENYEWE .
2. Chagua eneo kwenye ramani na uguse PAKUA .
© 2020 HMD Global Oy. Haki Zote zimehifadhiwa. 31
Nokia 2.4 Mwongozo wa mtumiaji
Sasisha ramani iliyopo
1. Gusa Ramani > > Ramani za nje ya mtandao na jina la ramani.
2. Gusa SASISHA .
Ikiwa ikoni haipatikani, gusa ikoni ya akaunti ya mtumiaji ya Google au picha yako ya akaunti ya mtumiaji ya Google.
Dokezo: Pia unaweza kuweka simu yako kusasisha ramani kiotomatiki. Gusa Ramani > >
Ramani za nje ya mtandao > na ubadilishe Sasisha ramani za nje ya mtandao kiotomatiki
na Pakua ramani za nje ya mtandao kiotomatiki kwa Washa .

TUMIA HUDUMA ZA ENEO

Tumia Ramani ili kujua uko wapi, na ambatisha eneo lako kwenye picha unazopiga. Maelezo ya eneo yanaweza kuambatishwa kwenye picha au video, kama eneo lako linaweza kubainishwa kwa kutumia teknolojia ya mtandao. Ukishiriki picha au video ambayo ina maelezo ya eneo, maelezo ya eneo yanaweza kuonyeshwa kwa wale wanaotazama picha au video. Baadhi ya programu zinaweza kutumia maelezo yako ya maeneo ili kutoa huduma mbalimbali.
Washa huduma za maeneo
Picha yako huonyesha eneo lako kwenye ramani kwa kutumia mfumo wa mkao wa setileti, Wi-Fi, au mkao wa mtandao (Cell ID).
Upatikanaji, usahihi na ukamilifu wa maelezo ya eneo hutegemea, kwa mfano, eneo lako, maeneo ya karibu, na vyanzo vya mhusika mwingine, na huenda ukazuiwa. Huenda maelezo ya eneo yasipatikane, kwa mfano, ndani ya majengo au chini ya ardhi. Kwa maelezo ya sera yanayohusiana na mbinu za mkao, angalia HMD Global Privacy Policy, available at http://www.nokia.com/phones/privacy.
Baadhi ya mifumo ya mkao wa setilaiti inaweza kuhitaji uhamishaji wa viwango vidogo vya data kwenye mtandao wa simu. Kama unataka kuepuka gharama ya data, kwa mfano wakati unasafiri, unaweza kuzima muunganisho wa data ya simu katika mipangilio ya simu yako.
Mkao wa Wi-Fi huboresha usahihi wa mkao wakati mawimbi ya setileti hayapatikani, hasa wakati uko ndani au kati ya majengo marefu. Ukiwa uko katika mahali matumizi ya Wi-Fi yamekatazwa, unaweza kuzima Wi-Fi katika mipangilio ya simu yako.
Gusa Mipangilio > Eneo , na uwashe Tumia Eneo .
© 2020 HMD Global Oy. Haki Zote zimehifadhiwa. 32
Nokia 2.4 Mwongozo wa mtumiaji
10 Programu, visasisho, na hifadhi nakala

PATA PROGRAMU KUTOKA KWENYE GOOGLE PLAY

Unahitaji kuongeza akaunti ya Google kwenye simu yako ili utumie huduma za Google Play. Mabadiliko yanaweza kutumika kwa baadhi ya maudhui yanayopatikana kwenye Google Play. Ili kuongeza mbinu ya malipo, gusa Play Store > > Mbinu za malipo . Hakikisha kila wakati una kibali kutoka kwa mmiliki wa mbinu ya malipo wakati unanunua maudhui kutoka Google Play.
Ongeza akaunti ya Google kwenye simu yako
1. Gusa Mipangilio > Akaunti > Ongeza akaunti > Google . Ukiulizwa, thibitisha mbinu ya kufunga kifaa chako.
2. Andika hati tambulishi za akaunti yako ya Google na uguse Ifuatayo , au, kuunda akaunti mpya, gusa Unda akaunti .
3. Fuata maagizo kwenye simu yako.
Pakua programu
1. Gusa Play Store .
2. Gusa upau wa utafutaji ili utafute programu, au chagua programu kutoka kwenye mapendekezo yako.
3. Katika ufafanuzi wa programu, gusa sakinisha ili upakue na usakinishe programu.
Ili kuona programu zako, nenda kwenye skrini ya mwanzo na utelezeshe juu kutoka chini ya skrini.

WEZESHA NAFASI KWENYE SIMU YAKO

Ikiwa kumbukumbu ya simu yako inajaa, hamisha faili kwenye kadi ya kumbukumbu au ufute faili zisizohitajika.
Hamisha faili kwenye kadi ya kumbukumbu
Ili kuhamisha picha kutoka kwenye kumbukumbu ya simu yako hadi kwenye kadi ya kumbukumbu, gusa Faili > Picha . Bonyeza na ushikilie picha unayotaka kuhamisha, na uguse > Hamisha kwenye > kadi ya SD .
Ili kuhamisha nyaraka na faili, gusa Faili > Nyaraka na Nyingine . Gusa kando ya jina la faili, na uguse Hamisha kwenye kadi ya SD .
© 2020 HMD Global Oy. Haki Zote zimehifadhiwa. 33
Nokia 2.4 Mwongozo wa mtumiaji

SASISHA PROGRAMU YA SIMU YAKO

Kuwa katika hali sawa na mdundo - sasisha programu ya simu yako pasi waya ili upate vipengee vipya na vilivyoboreshwa vya simu yako. Kusasisha programu kunaweza pia kuboresha utendakazi wa simu yako.
Sakinisha visasisho vinavyopatikana
Gusa Mipangilio > Mfumo > Mipangilio ya kina > Kisasisho cha mfumo > Kagua sasisho ili kukagua kama visasisho vinapatikana.
Wakati simu yako inapokuarifu kwamba sasisho linapatikana, fuata maagizo yaliyoonyeshwa kwenye simu yako. Ikiwa simu yako inaishiwa na kumbukumbu, huenda ukahitaji kusogeza programu, picha, na vitu vyako vingine kwenye kadi ya kumbukumbu.
Onyo: ukisakinisha kisasisho cha programu, huwezi kutumia kifaa hicho, hata kupiga simu za dharura, mpaka usasishaji ukamilike na kifaa kiwashwe upya.
Kabla ya kuanza kusasisha, unganisha chaja ua hakikisha betri ya kifaa ina nishati ya kutosha, na unganishe kwenye Wi-Fi, kwa kuwa vifurushi vya kusasisha vinaweza kutumia data nyingi ya simu.

HIFADHI NAKALA YA DATA YAKO

Ili kuhakikisha data yako ni salama, tumia kipengele cha kuhifadhi nakala kwenye simu yako. Data ya kifaa chako (kama vile manenosiri ya Wi-Fi na historia ya simu) na data ya simu (kama mipangilio na faili zilizohifadhiwa na programu) zitahifadhiwa kwa umbali.
Washa kuhifadhi nakala kiotomatiki
Gusa Mipangilio > Mfumo > Hifadhi nakala rudufu , na uwashe hifadhi nakala.

REJESHA MIPANGILIO HALISI NA UONDOE MAUDHUI BINAFSI KWENYE SIMU YAKO

Ajali zinaweza kutokea - Ikiwa simu yako haifanyi kazi vizuri, unaweza kurejesha mipangilio yake halisi. Au, ukinunua simu mpya, au uwe unataka kutupa au kuchakata upya simu yako, hivi ndivyo unavyoweza kuondoa maelezo na maudhui yako ya kibinafsi. Kumbuka kwamba ni wajibu wako kuondoa maudhui yote ya kibinafsi.
© 2020 HMD Global Oy. Haki Zote zimehifadhiwa. 34
Nokia 2.4 Mwongozo wa mtumiaji
Seti upya simu yako
1. Gusa Mipangilio > Mfumo > Mipangilio ya kina > Weka upya chaguo >
Futa data yote (rejesha data ya mwanzo) .
2. Fuata maagizo yaliyoonyeshwa kwenye simu yako.
© 2020 HMD Global Oy. Haki Zote zimehifadhiwa. 35
Nokia 2.4 Mwongozo wa mtumiaji
11 Linda simu yako

LINDA SIMU YAKO KWA KUFULI YA SKRINI

Unaweza kuweka simu yako kuhitaji uhalalishaji wakati unapofungua skrini.
Weka kufuli ya skrini
1. Gusa Mipangilio > Usalama > Kufuli ya skrini .
2. Chagua aina ya saa na ufuate maagizo kwenye simu yako.

LINDA SIMU YAKO KWA KUTUMIA ALAMA YA KIDOLE CHAKO

Ongeza alama ya kidole
1. Gusa Mipangilio > Usalama > Alama ya kidole .
2. Chagua ni mbinu gani ya hifadhi nakala ya kufungua unayotaka kutumia kwenye skrini ya kufunga na ufuate maagizo yaliyoonyeshwa kwenye simu yako.
Fungua simu yako kwa kutumia kidole chako
Weka kidole chako kilichosajiliwa kwenye sensa.
Ikiwa kuna hitilafu ya sensa ya alama ya kidole, na huwezi kutumia mbinu mbadala za kuingia ili kurejesha au kuweka upya simu kwa njia yoyote ile, simu yako itahitaji huduma kutoka kwa mtu aliyeidhinishwa. Huenda gharama ya ziada ikatumika, na data yote ya kibinafsi kwenye simu huenda ikafutwa. Kwa maelezo zaidi, wasiliana na care point iliyo karibu ya simu yako, au muuzaji wa simu yako.
© 2020 HMD Global Oy. Haki Zote zimehifadhiwa. 36
Nokia 2.4 Mwongozo wa mtumiaji

LINDA SIMU YAKO KWA KUTUMIA USO WAKO

Sanidi uhalalishaji wa uso
1. Gusa Mipangilio > Usalama > Fungua kwa kutumia uso .
2. Chagua ni mbinu gani ya hifadhi nakala ya kufungua unayotaka kutumia kwenye skrini ya kufunga na ufuate maagizo yaliyoonyeshwa kwenye simu yako.
Fungua macho yako na uhakikishe uso wako unaonekana kikamilifu na hujafunikwa na kitu chochote, kama vile kofia au miwani.
Kumbuka: Kutumia uso wako kufungua simu yako si salama kama kutumia alama ya kidole, ruwaza au nenosiri. Huenda simu yako imefunguliwa na mtu au kitu chenye mwonekano huo mmoja. Huenda kufungua kwa uso kusifanye kazi vizuri katika mazingira yenye mwangaza wa nyuma au wenye giza au mkali.
Fungua simu yako kwa kutumia uso wako
Ili kufungua simu yako, washa skrini yako na uangalie kamera.
Ikiwa kuna hitilafu ya kutambua uso, na huwezi kutumia mbinu mbadala za kuingia ili kurejesha au kuweka upya simu kwa njia yoyote ile, simu yako itahitaji huduma. Huenda gharama ya ziada ikatumika, na data yote ya kibinafsi kwenye simu huenda ikafutwa. Kwa maelezo zaidi, wasiliana na kituo cha huduma kilichoidhinishwa kilicho karibu cha simu yako, au muuzaji wa simu yako.

BADILISHA MSIMBO WAKO WA PIN YA SIM

Ikiwa SIM kadi yako ilikuja na msimbo wa kuweka upya PIN ya SIM, unaweza kuibadilisha ili kuwa salama zaidi. Sio watoa huduma wote wa mtandao wanakubali hii.
© 2020 HMD Global Oy. Haki Zote zimehifadhiwa. 37
Nokia 2.4 Mwongozo wa mtumiaji
Chagua PIN ya SIM yako
Unaweza kuchagua ni dijiti gani za kutumiza kwa PIN ya SIM. Msimbo wa PIN ya SIM unaweza kuwa wa dijiti 4-8.
1. Gusa Mipangilio > Usalama > Kufunga SIM kadi .
2. Chini ya kadi iliyoteuliwa ya SIM, gusa Badilisha nenosiri la kuzuia .

MISIMBO YA UFIKIAJI

Jifunze misimbo tofauti kwenye simu yako ni ya nini.
Msimbo wa PIN au PIN2
Misimbo ya PIN au PIN2 ina dijiti 4-8.
Misimbo hii hulinda SIM kadi yako dhidi ya matumizi yasioidhinishwa au huhitajika ili kufikia vipengee vingine. Unaweza kuweka simu yako kukuuliza msimbo wa PIN wakati unapoiwasha.
Ukisahau misimbo au iwe haijatolewa pamoja na kadi yako, wasiliana na mtoa huduma wa mtandao wako.
Ukicharaza msimbo vibaya mara 3 zikifuatana, unahitaji kufungua msimbo kwa kutumia msimbo wa PUK au PUK2.
Misimbo ya PUK au PUK2
Misimbo ya PUK au PUK2 zinahitajika ili kufungua msimbo wa PIN au PIN2.
Ikiwa misimbo haijatolewa na SIM kadi yako, wasiliana na mtoa huduma wako wa mtandao.
Msimbo wa kufunga
Msimbo wa kufunga unajulikana pia kama msimbo au nenosiri la usalama.
Msimbo wa kufunga hukusaidia kulinda simu yako dhidi ya matumizi yasiyoidhinishwa. Unaweza kuweka simu yako kukuuliza msimbo wa kufunga ambao unafasili. Weka msimbo kuwa siri na mahali salama, kando na simu yako.
Ukisahau msimbo na simu yako imefungwa, simu yako itahitaji huduma. Huenda gharama ya ziada ikatumika, na data yote ya kibinafsi kwenye simu huenda ikafutwa. Kwa maelezo zaidi, wasiliana na kituo cha huduma kilichoidhinishwa kilicho karibu cha simu yako, au muuzaji wa simu yako.
© 2020 HMD Global Oy. Haki Zote zimehifadhiwa. 38
Nokia 2.4 Mwongozo wa mtumiaji
Msimbo wa IMEI
Msimbo wa IMEI hutumiwa kutambua simu katika mtandao. Huenda pia ukahitaji kupeana nambari kwa kituo chako kilichoidhinishwa au muuzaji wa simu. Ili kuona msimbo wako wa IMEI:
• piga *#06#
• angalia kikasha halisi cha mauzo
Ikiwa msimbo wa IMEI umechapishwa kwenye simu yako, unaweza kuupata, kwa mfano, kwenye trei ya SIM au chini ya kifuniko cha nyuma, ikiwa simu yako ina kifuniko kinachoweza kuondolewa.
Tafuta au funga simu yako
Ukipoteza simu yako, unaweza kuitafuta, kuifunga, au kuifuta kwa mbali ikiwa umeingia kwenye Akaunti ya Google. Tafuta Kifaa Changu huwashwa kimsingi kwa simu zinazohusishwa na Akaunti ya Google.
Ili utumie Tafuta Kifaa Changu, lazima simu yako iwe:
• Imewashwa
• Umeingia kwenye Akaunti ya Google
• Imeunganishwa kwenye data ya simu au
• Inapatika kwenye Google Play
• Eneo limewashwa
• Tafuta Kifaa Changu imewashwa
Wi-Fi
Wakati Tafuta Kifaa Changu kinapounganishwa na simu yako, utaona eneo la simu, na simu itapata arifa.
1. Fungua android.com/find kwenye kompyuta, kompyuta kibao au simu iliyounganishwa kwenye intaneti na uingie kwenye Akaunti yako ya Google.
2. Ikiwa una zaidi ya simu moja, bofya simu iliyopotea juu ya skrini.
3. Kwenye ramani, angalia kuhusu mahali simu iko. Eneo huwa ukadiriaji na huenda lisiwe sahihi.
Iwapo kifaa chako hakiwezi kupatikana, Tafuta Kifaa Changu itaonyesha eneo la mwisho linalojulikana, ikiwa ipo. Ili kufunga au kufuta simu yako, fuata maagizo kwenye tovuti.
© 2020 HMD Global Oy. Haki Zote zimehifadhiwa. 39
Nokia 2.4 Mwongozo wa mtumiaji
12 Maelezo ya bidhaa na usalama

KWA USALAMA WAKO

Soma maelekezo haya rahisi. Kutoyafuata kunaweza kuwa hatari au kinyume cha sheria na masharti. Kwa maelezo zaidi, soma mwongozo kamili wa mtumiaji.
ZIMA KATIKA MAENEO YALIYOKATAZWA
Zima kifaa wakati matumizi ya simu za mkononi yamekatazwa au wakati yanaweza kusababisha mwingiliano au hatari, kwa mfano, ndani ya ndege au hospitalini, au karibu na vifaa vya matibabu, mafuta, kemikali, au maeneo yenye mlipuko. Tii maagizo yote katika maeneo yaliyozuiwa.
USALAMA BARABARANI HUJA KWANZA
Tii sheria zote za mahali ulipo. Daima iache mikono yako iwe huru wakati unaendesha gari. Kitu cha kuzingatia kwanza unapoendesha gari unapaswa kuwa usalama barabarani.
MWINGILIANO
© 2020 HMD Global Oy. Haki Zote zimehifadhiwa. 40
Nokia 2.4 Mwongozo wa mtumiaji
Vifaa vyote visivyotumia waya vina uwezekano wa kupata mwingiliano, ambao unaweza kuathiri utendaji kazi wake.
HUDUMA ILIYOIDHINISHWA
Watu walioidhinishwa tu ndio wanaweza kuweka au kukarabati bidhaa hii.
BETRI, CHAJA, NA VIFAA VINGINE VYA ZIADA
Tumia betri, chaja, na vifaa vya ziada ambavyo vimeidhinishwa na HMD Global Oy kwa ajili ya matumizi na kifaa hiki tu. Usiunganishe bidhaa ambazo haziendani pamoja.
WEKA KIFAA KIKIWA KIKAVU
Ikiwa kifaa chako kinaweza kuzuia maji, tafadhali rejelea ukadiriaji wake wa IP kwa mwongozo zaidi wa kina.
© 2020 HMD Global Oy. Haki Zote zimehifadhiwa. 41
Nokia 2.4 Mwongozo wa mtumiaji
SEHEMU ZA GLASI
Kifaa na/au skrini yake imetengenezwa kwa glasi. Glasi hii inaweza kuvunjika kifaa kikiangushwa mahali pagumu au kupokea mgongano mzito. Glasi ikivunjika, usiguse sehemu za glasi za kifaa au ujaribu kuondoa glasi iliyovunjika kutoka kwa kifaa. Acha kutumia kifaa hadi glasi ibadilishwe na mhudumu aliyeidhinishwa.
LINDA UWEZO WAKO WA KUSIKIA
Kuzuia madhara yanayowezekana ya kusikia, usisikilize katika viwango vya juu vya sauti kwa muda mrefu. Kuwa mwangalifu wakati unashikilia kifaa chako karibu na sikio wakati kipaza sauti kinatumika.
SAR
Kifaa hiki kinatimiza matakwa ya maelekezo ya ujiwekaji wazi kwa frikwensi za redio wakati kikitumika ama kwenye mkao wa kawaida kwenye sikio au wakati kikiwekwa angalau sentimita
1.5 (inchi 5/8) kutoka kwenye mwili. Thamani maalum za juu za SAR zinaweza kupatikana katika sehemu ya Maelezo ya Cheti ya (SAR) ya mwongozo huu wa mtumiaji. Kwa maelezo zaidi, angalia sehemu ya Maelezo ya Cheti (SAR) ya mwongozu huu wa mtumiaji au nenda kwenye
www.sar-tick.com.
© 2020 HMD Global Oy. Haki Zote zimehifadhiwa. 42
Nokia 2.4 Mwongozo wa mtumiaji

HUDUMA ZA MTANDAO NA GHARAMA

Kutumia baadhi ya vipengele na huduma, au kupakia maudhui, pamoja na vipengee visivyolipishwa, uhitaji muunganisho wa mtandao. Hii huenda ikasababisha uhamishaji wa viwango vikubwa vya data, ambayo inaweza kusababisha gharama ya data. Huenda pia ukahitajika kujisajili kwa baadhi ya vipengele.
Muhimu: Huenda 4G/LTE isikubaliwe na mtoa huduma wa mtandao wako au na mtoa huduma unayemtumia wakati unasafiri. Katika hali hizi, huenda usiweze kupiga au kupokea simu, kutuma au kupokea ujumbe au kutumia miunganisho ya data ya simu. Ili kuhakikisha kifaa chako kinafanya kazi vizuri wakati huduma ya 4G/LTE haipatikani, inapendekezwa kwamba ubadilishe kasi ya juu zaidi ya muunganisho kutoka 4G hadi 3G. Ili kufanya hivi, kwenye skrini ya mwanzo, gusa Mipangilio > Mtandao na Intaneti > Mtandao wa simu , na ubadilishe
Aina ya mtandao unaopendelewa kwa 3G .

SIMU ZA DHARURA

Muhimu: Miunganisho katika hali zote haiwezi kuhakikishwa. Kamwe usitegemee tu simu
pasiwaya kwa mawasiliano muhimu kama vile tiba za dharura.
Kabla ya kupiga simu:
• Washa simu.
• Kama skrini ya simu na vitufe vimefungwa, vifungue.
• Nenda eneo lenye mawimbi ya simu ya kutosha.
Kwenye skrini ya mwanzo, gusa
1. Charaza namba rasmi ya dharura ya eneo lako la sasa. Nambari za simu ya dharura hutofautiana kimaeneo.
2. Gusa .
3. Toa maelezo yanayofaa kwa usahihi kama iwezekanavyo. Usikate simu hadi upewe ruhusa ya kufanya hivyo.
Huenda pia ukahitajika kufanya yafuatayo:
• Weka SIM kadi ndani ya simu. Ikiwa huna SIM kadi, kwenye skrini ya kufunga, gusa Dharura .
• Ikiwa simu yako itakuuliza msimbo wa PIN, gusa Dharura .
• Zima vizuizi vya simu katika simu yako, kama vile uzuiaji simu, upigaji uliopangwa, au kikundi maalum cha watumiaji.
• Ikiwa mtandao wa simu haupatikani, unaweza pia kujaribu kupiga simu ya intaneti, ikiwa unaweza kufikia intaneti.
© 2020 HMD Global Oy. Haki Zote zimehifadhiwa. 43
Nokia 2.4 Mwongozo wa mtumiaji

KUHUDUMIA KIFAA CHAKO

Shughulikia kifaa chako, betri, chaja na vifaa vya ziada kwa uangalifu. Mapendekezo yafuatayo yatakusaidia kufanya kifaa chako kifanye kazi.
• Weka kifaa kikiwa kikavu. Taka za mtuamo, unyevu wa hewa, na aina zote za vimiminiko au unyevu zinaweza kuwa na madini yanayoweza kutia kutu saketi za elektroniki.
• Usitumie au kuhifadhi kifaa chako kwenye maeneo yenye vumbi au uchafu.
• Usihifadhi kifaa kwenye halijoto ya juu au ya chini. Halijoto ya juu huenda ikaharibu kifaa au betri.
• Usihifadhi kifaa kwenye halijoto baridi. Wakati kifaa kimerudi kwenye joto lake la kawaida, unyevunyevu unaweza kutengenezeka ndani ya kifaa.
• Usifungue kifaa kando na ilivyoagizwa katika kiongozi cha mtumiaji.
• Mabadiliko yasioidhinishwa yanaweza kuharibu kifaa hiki na kukiuka sheria zinazosimamia vifaa vya redio.
• Usiangushe, kugonga, au kutingisa kifaa au betri. Kukishika kiholela kunaweza kuivunja.
• Tumia kitambaa laini, kisafi na kikavu kusafisha uso wa kifaa hiki.
• Usipake rangi kifaa. Rangi inaweza kuzuia utendaji kazi wa kawaida.
• Weka kifaa chako mbali na sumaku au maeneo ya sumaku.
• Ili kuweka data yako muhimu salama, ihifadhi angalau katika maeneo mawili tofauti, kama vile kifaa chako, kadi ya kumbukumbu, au kompyuta au andika maelezo muhimu.
Wakati wa utendajikazi kwa muda mrefu, kifaa kinaweza kuwa na joto. Katika hali nyingi, hii ni kawaida. Kuepuka kupata joto sana, huenda kifaa kikapunguka kasi kiotomati, kikapunguza mwangaza wakati wa simu ya video, kikafunga programu, kikazima kuchaji, na ikiwezekana, kikajizima chenyewe. Kama kifaa hakifanyi kazi vizuri, kipeleke kwenye suhula iliyo karibu ya huduma iliyoidhinishwa.

UCHAKATAJI UPYA

Daima rudisha bidhaa zako za elektroniki, betri na nyezo za kifurushi zilizotumiwa kwa maeneo maalum ya ukusanyaji. Kwa njia hii utasaidia kuzuia utupaji taka usiodhibitiwa na kukuza uchakataji upya wa nyenzo. Bidhaa za umeme na elektroniki huwa na nyenzo nyingi za thamani, ikiwa ni pamoja na madini (kama vile shaba, aluminiamu, chuma, na magnesiamu) na madini ya
© 2020 HMD Global Oy. Haki Zote zimehifadhiwa. 44
Nokia 2.4 Mwongozo wa mtumiaji
thamani (kama vile dhahabu, fedha, na paladiamu) Nyenzo zote za kifaa zinaweza kufufuliwa kama nyenzo na nishati.

ALAMA YA PIPA ILIYO NA MKATO

Alama ya pipa iliyo na mkato
Alama ya pipa iliyo na mkato kwenye bidhaa, betri, maandishi, au kifurushi chako hukukumbusha kwamba bidhaa zote za elektroniki na betri lazima zipelekwe kwenye mkusanyiko tofauti wakati bidhaa inapokwisha. Usitupe bidhaa hizi kama takataka zisizochambuliwa za manispaa: zipeleke zichakatwe. Kwa maelezo juu ya eneo la uchakataji lililo karibu na wewe, wasiliana na mamlaka ya taka ya eneo lako.

MAELEZO YA BETRI NA CHAJA

Maelezo ya betri na chaja
Ili ukague ikiwa simu yako ina betri inayoweza kuondolewa au isiyoweza kuondolewa, angalia Mwongozo wa kuanza kutumia.
Vifaa vilivyo na beti inayoweza kuondolewa Tumia kifaa chako na betri halisi tu inayoweza kuchajiwa upya. Betri inaweza kuchajiwa na kuondolewa chaji hata mara mia, lakini hatimaye itachoka. Wakati muda wa kuongea na muda wa kusubiri unaonekana wazi kuwa mfupi kuliko kawaida, badilisha betri.
Vifaa vilivyo na betri isiyoweza kuondolewa Usijaribu kuitoa betri, kwa sababu unaweza kuharibu kifaa. Betri inaweza kuchajiwa na kuondolewa chaji hata mara mia, lakini hatimaye itachoka. Wakati muda wa kuongea na muda wa kusubiri unaonekana wazi kuwa mfupi kuliko kawaida, kubadilisha betri, peleka kifaa hicho kwenye kitengo cha mtengenezaji aliyeidhinishwa kilicho karibu.
Chaji kifaa chako na chapa uliyopewa. Aina ya plagi ya chaja huenda ikatofautiana. Muda wa kuchaji unaweza kutofautiana kulingana na uwezo wa kifaa.
© 2020 HMD Global Oy. Haki Zote zimehifadhiwa. 45
Nokia 2.4 Mwongozo wa mtumiaji
Maelezo ya usalama wa betri na chaja
Kifaa chako kikikamiliza kuchajiwa, chomoa chaja kutoka kwenye kifaa na soketi ya umeme. Tafadhali kumbuka kwamba kuchaji kwa mfululizo hakupaswi kuzidi saa 12. Ikiachwa bila kutumika, betri iliyokuwa imejaa chaji itapoteza chaji yake kadri muda unavyopita.
Halijoto ya juu sana hupunguza uwezo na maisha ya betri. Daima jaribu kuweka betri kwenye halijoto kati ya 15°C na 25°C (59°F na 77°F) kwa utendakazi bora. Kifaa chenye betri moto au baridi kinaweza kisifanye kazi kwa muda. Kumbuka kwamba huenda betri ikaisha haraka katika halijoto baridi na kupoteza nishati ya kutosha na kuzima simu katika dakika chache. Ukiwa nje katika halijoto baridi, weka simu yako ikiwa na joto kiasi.
Tii sheria za eneo lako. Peleka ichakatwe upya ikiwezekana. Usitupe kama takataka za kawaida za nyumbani.
Usiweke betri kwenye shinikizo la chini sana la hewa au kuiwacha kwenye halijoto ya juu sana, kwa mfano kuitupa kwenye moto, kwa kuwa hiyo inaweza kusababisha betri kulipuka au kuvuja kiowevu au gesi inayoweza kuwaka moto.
Usifungue, kukata, kuvunja, kukunja, kutoa, au kuharibu betri kwa njia yoyote ile. Kama betri itavuja, usiruhusu umaji uguse ngozi au macho. Hii ikifanyika, osha maeneo yaliyoathirika mara moja na maji, au tafuta msaada wa kitabibu. Usirekebishe, kujaribu kuingiza vitu vigeni kwenye betri, au kuizamisha au kuiweka kwenye maji au aina nyingine ya umaji. Betri zinaweza kulipuka kama zimeharibika.
Tumia betri na chaja kwa matumizi yaliyokusudiwa tu. Matumizi mabaya, au matumizi yasiyoidhinishwa au yasiyotangamana na betri au chaja huenda yakaleta hatari ya moto, mlipuko au hatari nyingine, na huenda ikabatilisha uhalali wowote ulioidhinishwa au waranti. Kama unaamini betri au chaja imeharibika, ipeleke kwa kituo cha huduma au muuza simu yako kabla ya kuendelea kuitumia. Kamwe usitumie betri au chaja yoyote iliyoharibika. Tumia chaja ndani ya nyumba tu. Usichaji kifaa chako wakati wa dhoruba ya radi.
Ili kuchopoa chaja au kifaa chochote cha ziada, kamata na uvute plagi na siyo waya.
Kwa kuongezea, zifuatazo hutumika ikiwa kifaa chako kina betri inayoweza kuondolewa:
• Daima zima na ung’oe chaja kabla ya kuondoa betri.
• Mkato wa umeme wa bahati mbaya unaweza kutokea kwa bahati mbaya kama kitu cha chuma kitagusa vipapi vya chuma kwenye betri. Huenda hii ikaharibu betri au kifaa kile kingine.

WATOTO WADOGO

Kifaa chako na viboreshaji vyake sio sesere. Vinaweza kuwa na sehemu ndogo ndogo. Viweke mbali na watoto wadogo.
© 2020 HMD Global Oy. Haki Zote zimehifadhiwa. 46
Nokia 2.4 Mwongozo wa mtumiaji

VIFAA VYA MATIBABU

Utendakazi wa kifaa cha kupitisha mawimbi ya redio, pamoja na simu pasiwaya, huenda zikaingiliana na utendakazi wa vifaa vya matibabu ambavyo havijakingwa vizuri. Wasiliana na daktari au mtengenezaji wa kifaa cha matibabu ili ubainishe kama kimekingwa vizuri dhidi ya nguvu ya nje ya redio.

VIFAA VYA MATIBABU VINAVYOPACHIKWA

Kuepuka mwingiliano unaowezekana, watengenezaji wa vifaa vilivyopachikwa vya matibabu wanapendekeza nafasi isiyopungua sentimita 15.3 (inchi 6) kati ya kifaa kisichotumia waya na kifaa cha matibabu. Watu ambao wana vifaa kama hivyo wanapaswa:
• Kila wakati weka kifaa pasiwaya umbali wa zaidi ya sentimita 15.3 (inchi 6) kutoka kwenye kifaa cha matibabu.
• Usibebe kifaa pasiwaya katika mfuko wa shati.
• Shikilia kifaa pasiwaya kwenye sikio kando
Ikiwa una maswali yoyote kuhusu kutumia kifaa chako pasiwaya na kifaa cha matibabu kilichopachikwa, wasiliana na mtoa huduma wako wa afya.
na kifaa cha matibabu.
• Zima kifaa pasiwaya kama kuna sababu yoyote ya kushuku kwamba mwingiliano unafanyika.
• Fuata maagizo ya mtengeneza kifaa cha matibabu kilichopachikwa.

VIFAA VYA KUSAIDIA KUSIKIA

Onyo: Wakati unatumia kifaa cha kuvaa kichwani, uwezo wako wa kusikiliza sauti za nje
unaweza kuathirika. Usitumie kifaa cha kuvaa kichwani mahali ambapo kinaweza kuhatarisha usalama wako.
Baadhi ya vifaa pasiwaya vinaweza kuingiliana na baadhi ya vifaa vya kusaidia kusikia.

LINDA MTOTO WAKO DHIDI YA VITU VYENYE MADHARA

Kifaa chako kinaweza kupata virusi na vitu vingine vyenye madhara. Chukua tahadhari zifuatazo:
• Kuwa mwangalifu wakati wa kufungua ujumbe. Huenda zikawa na programu mbaya au yenye kudhuru kifaa au kompyuta yako.
• Kuwa mwangalifu wakati unakubali maombi ya muunganisho, unapovinjari tovuti, au
© 2020 HMD Global Oy. Haki Zote zimehifadhiwa. 47
kupakua yaliyomo. Usikubali miunganisho ya Bluetooth kutoka kwenye vyanzo usivyoviamini.
• Sakinisha na tumia huduma na programu kutoka vyanzo ambavyo unaviamini tu na ambavyo vinatoa usalama na ulinzi.
Nokia 2.4 Mwongozo wa mtumiaji
• Sakinisha kizuia virusi na programu zingine za usalama kwenye kifaa chako na kompyuta yoyote iliyounganishwa. Tumia tu programu moja ya kinga virusi kwa wakati mmoja. Kutumia zaidi ya moja huenda kukaathiri utendakazi na utumizi
wa kifaa na/au kompyuta.
• Ikiwa unafikia vialamisho vilivyosakinishwa mapema na viungo kwa tovuti vya mhusika wa tatu, chukua tahadhari zinazohitajika. HMD Global haiidhinishi wala kuwajibika kwa tovuti hizo.

MAGARI

Huenda mawimbi ya redio yakaathiri vibaya mifumo ya elektroniki iliyowekwa vibaya au isiyokingwa vizuri katika magari. Kwa maelezo zaidi, wasiliana na mtengeneza gari lako au vifaa vyake. Watu walioidhinishwa tu ndio wanaweza kukarabati au kuweka kifaa ndani ya gari. Uwekaji wenye kasoro huenda ukawa hatari na ukabatilisha waranti yako. Hakikisha mara kwa mara kwamba vifaa vyote pasiwaya ndani ya gari vimefungwa vizuri na vinafanya kazi sawasawa. Usihifadhi au kubeba vifaa vinavyoweza kuchomeka au kulipuka katika eneo lile moja kama kifaa, sehemu zake, au vifaa vya ziada. Usiweke kifaa chako au viboreshaji kwenye eneo ambalo mfuko wa hewa hutumika.

MAZINGIRA YANAYOWEZA KULIPUKA

Zima kifaa chako katika eneo lolote lenya mazingira yanayoweza kulipika, kama vile karibu na pampu za mafuta katika vituo vya mafuta. Cheche zinaweza kusababisha mlipuko au moto unaoweza kuleta majeraha au kifo. Kumbuka vikwazo katika maeneo yenye mafuta; viwanda vya kemikali; au mahali ambapo shughuli za ulipuaji zinaendelea kufanyika. Maeneo yenye mazingira yenye uwezekano wa milipuko yanaweza kuwa na alama zisizo dhahiri. Haya kwa kawaida ni maeneo ambapo unaweza kushauriwa kuzima injini yako, chini ya sitaha kwenye boti, uhamishaji kemikali au suhula za kuhifadhi, na ambapo hewa ina kemikali au chembechembe kama vile nafaka, vumbi au poda ya chuma. Wasiliana na watengeneza magari yanayotumia mafuta aina ya gesi oevu ya petroli iliyoyeyushwa (kama vile propeni au buteni) ikiwa kifaa hiki kinaweza kutumiwa vizuri katika maeneo yao.

HABARI YA UTOAJI CHETI (SAR)

Kifaa hiki cha mkononi kinatimiza maelekezo yanayohusu ujiwekaji wazi kwa mawimbi ya redio.
Kifaa chako cha mkononi ni transmita na kipokezi cha redio. Kimeundwa kisizidishe viwango vya ufichuzi vya mawimbi ya redio (maeneo ya mawimbi ya redio ya sumaku ya umeme), vinavyopendekezwa na miongozo ya kimataifa kutoka kwa shirika huru la kisayansi ICNIRP. Maelekezo haya yanajumuisha viwango vya usalama vilivyoundwa kuhakikisha usalama wa watu wote, Haijalishi umri na afya. Maelekezo ya ufichuzi yanategemea Kiwango Maalum cha Ufyonzaji (SAR), ambacho ni onyesho la nguvu ya kiwango cha masafa ya redio (RF) ambayo inawekwa kichwani au mwilini wakati kifaa kinatumika. Kiwango cha SAR cha ICNIRP cha vifaa vya simu ni 2.0 W/kg kwa wastani wa gramu kumi za tishu.
© 2020 HMD Global Oy. Haki Zote zimehifadhiwa. 48
Nokia 2.4 Mwongozo wa mtumiaji
Vipimo vya SAR vinatekelezwa kwa kifaa katika mikao ya kawaida ya uendeshaji, wakati kifaa kinapitisha katika kiwango chake cha juu zaidi kilichoidhinishwa cha nishati, katika bendi zote zilizopimwa za masafa.
Tafadhali rejelea www.nokia.com/phones/sar kwa thamani ya juu ya SAR ya kifaa.
Kifaa hiki kinatimiza matakwa ya maelekezo ya ujiwekaji wazi kichwani au wakati kimewekwa angalau inchi 5/8 (sentimita 1.5) kutoka kwenye mwili. Wakati kikasha cha kubebea, kishikiza kwenye mkanda au aina nyingi ya kishikizi kikitumika kwa matumizi ya kuvaliwa mwilini, kinatakiwa kisiwe na chuma na kinatakiwa kuweka angalia umbali uliotajwa hapo juu kutoka kwenye mwili.
Kutuma data au ujumbe, muunganisho salama wa mtandao unahitajika. Utumaji unaweza kucheleweshwa hadi muunganisho huo upatikane. Fuata maagizo ya umbali wa kutenganisha hadi utumaji ukamilike.
Wakati wa matumizi ya kawaida, thamani za SAR kwa kawaida huwa chini ya thamani zilizotajwa hapa juu. Hii ni kwa sababu, kwa malengo ya ubora wa mfumo na kupunguza mwingiliano kwenye mtandao, nguvu ya kufanya kazi ya kifaa chako cha mkononi hupunguzwa kiotomati wakati nguvu kamili haihitajiki kwa simu. Nguvu towe inavyoendelea kuwa chini, ndivyo thamani ya SAR inavyokuwa chini.
Huenda modeli za vifaa zikawa na matoleo tofauti na zaidi ya thamani moja. Mabadiliko ya vijenzi na muundo yanaweza kufanyika baada ya muda na baadhi ya mabadiliko yanaweza kuathiri thamani za SAR.
Kwa maelezo zaidi, nenda kwenye www.sar-tick.com. Kumbuka kwamba vifaa vya mkononi huenda vikapitisha hata kama hupigi simu.
Shirika la Afya Duniani (WHO) limesema kwamba maelezo ya sasa ya kisayansi hayaashirii hitaji la tahadhari zozote maalum wakati wa kutumia vifaa vya mkononi. Ikiwa unavutiwa na kupunguza ufichuzi wako, wanapendekeza upunguze matumizi yako au utumie kifaa kisichotumia mikono ili kuweka kifaa mbali na kichwa na mwili wako. Kwa maelezo zaidi na ufafanuzi na majadiliano kuhusu ufichuzi wa RF, nenda kwenye tovuti ya WHO
www.who.int/peh-emf/en.

KUHUSU USIMAMIZI WA HAKI ZA DIJITALI

Unapokuwa ukitumia kifaa hiki, tii sheria zote na heshimu utamaduni wa wenyeji, uhuru binafsi wa mtu na haki halali za wengine, ikiwemo hakimiliki. Kinga za hakimiliki zinaweza kukuzuia dhidi ya kunakili, kurekebisha au kuhamisha picha, muziki na vitu vingine.

HAKIMILIKI NA ILANI NYINGINE

Hakimiliki na ilani nyingine
Upatikani wa baadhi ya bidhaa, vipengele, programu na huduma zilizofafanuliwa katika mwongozo huu zinaweza kutofautiana kulingana na eneo na uhitaji uamilishaji, kujisajili,
© 2020 HMD Global Oy. Haki Zote zimehifadhiwa. 49
Nokia 2.4 Mwongozo wa mtumiaji
mtandao na/au muunganisho wa intaneti na mpango unaofaa wa huduma. Kwa maelezo zaidi, wasiliana na mchuuzi au mtoa huduma wako. Kifaa hiki kinaweza kuwa na bidhaa, teknolojia au programu ambayo inaathiriwa na sheria na kanuni za usafirishaji nje ya nchi kutoka Marekani na nchi nyingine. Uchepushaji kinyume na sheria ni marufuku.
Yaliyomo katika waraka huu yametolewa ”kama yalivyo”. Isipokuwa kama inatakiwa hivyo na sheria husika, hakuna dhamana za aina yoyote, ama za moja kwa moja au zisizo bayana, pamoja na, lakini isiyokomea hapo, dhamana zisizo bayana za uuzikaji wa kibiashara na ufaaji kwa matumizi fulani, zinazotolewa kuhusiana na usahihi, uaminikaji au yaliyomo ndani ya waraka huu. HMD Global ina haki ya kupitia na kusahihisha waraka huu au kuuondoa wakati wowote bila kutoa taarifa kwanza.
Kwa kadiri inayohusiwa na sheria husika, hakuna wakati wowote ule HMD Global au wenye leseni wake watawajibika kwa upotevu wowote wa data au mapato au uharibifu wowote ule, uwe maalum, wa ajali, unatokana na, au usiokuwa wa moja kwa moja uliosababishwa.
Ni marufuku kutoa upya, kuhamisha au kusambaza sehemu ya yaliyomo au yote katika waraka huu katika hali yoyote ile bila ya kupewa kwanza idhini ya kuandikwa kutoka kwa HMD Global. HMD Global inaendesha sera ya kuendelea kubuni. HMD Global ina haki ya kufanya mabadiliko na kuboresha bidhaa yake yoyote iliyoelezwa katika waraka huu bila kutoa taarifa kwanza.
HMD Global haitoi wakilishi wowote, waranti au kuwajibika kwa utendaji kazi, maudhui, au usaidizi wa mtumiaji wa programu za mhusika wa tatu zilizotolewa na kifaa chako. Kwa kutumia programu, unakubali kwamba programu imetolewa kama ilivyo.
Upakuaji wa ramani, michezo, muziki na video na upakiaji taswira na video huenda ukajumuisha upitishaji wa viwango vikubwa vya data. Huenda mtoa huduma wako akatoza kwa upitishaji data. Upatikanaji wa bidhaa, huduma na vipengele fulani unaweza zikatofautiana kimaeneo. Tafadhali wasiliana na muuzaji wa eneo lako kwa maelezo zaidi na upatikanaji wa chaguo za lugha.
Vipengele, utendakazi na ainisho nyingine za bidhaa zinaweza kutegemea mtandao na hutegemea masharti, sheria, na gharama za ziada.
Ainisho, vipengele na maelezo mengine yote ya bidhaa yaliyotolewa yanaweza kubadilika bila ilani.
Sera ya Faragha ya HMD Global, inapatikana kwenye http://www.nokia.com/phones/privacy, hutumika kwa matumizi yako ya kifaa.
HMD Global Oy ndio wenye leseni ya kipekee ya rajamu ya Nokia ya simu na kompyuta kibao. Nokia ni alama ya biashara iliyosajiliwa ya Nokia Corporation.
Android, Google na alama na nembo zingine husika ni alama za biashara za Google LLC.
Alama ya neno na nembo za Bluetooth zinamilikiwa na Bluetooth SIG, Inc. na matumizi yoyote ya alama hizo na HMD Global yako chini ya leseni.
© 2020 HMD Global Oy. Haki Zote zimehifadhiwa. 50
Loading...