Muhimu: Kwa maelezo muhimu kuhusu matumizi salama ya kifaa na betri yako, soma maelezo
ya ”Kwa usalama wako” na ”Usalama wa Bidhaa” katika mwongozo uliochapishwa wa mtumiaji,
au kwenye www.nokia.com/support kabla utumie kifaa. Ili kujua jinsi ya kuanza kutumia kifaa
chako kipya, soma mwongozo uliochapishwa wa mtumiaji.
Sasisha simu yako na ukubali visasisho vinavyopatikana vya programu ili upate vipengee vipya
na vilivyoboreshwa vya simu yako. Kusasisha programu kunaweza pia kuboresha utendakazi wa
simu yako.
VITUFE NA SEHEMU
Simu yako
Mwongozo huu wa mtumiaji hutumika kwa modeli zifuatazo: TA-1206, TA-1211, TA-1214, TA1194, TA-1209.
1. Mweko
2. Kamera
3. Kipenyo cha SIM na kadi ya kumbukumbu
4. Kisaidizi cha Google/Kitufe cha Utafutaji
wa Google*
Baadhi ya vifaa vya ziada vilivyotajwa katika mwongozo huu wa mtumiaji, kama vile chaja, kifaa
cha kichwa, au kebo ya data, huenda vikauzwa kando.
*Kisaidizi cha Google hupatikana katika masoko na lugha zilizoteuliwa. Ambapo hakipatikani,
Kisaidizi cha Google hubadilishwa kwa Utafutaji wa Google. Angalia upatikanaji katika
https://support.google.com/assistant.
Sehemu na viunganishaji, hali ya sumaku
Usiunganishe kwenye bidhaa ambazo zinaunda ishara ya kutoa, kwa kuwa hii inaweza kuharibu
kifaa. Usiunganishe chanzo chochote cha stima kwenye kiunganisha cha sauti. Ukiunganisha
kifaa chochote cha nje au vifaa vyovyote vya sauti kando na vile vilivyoidhinishwa kutumiwa na
kifaa hiki, Kiunganishi cha sauti, kuwa makini sana na viwango vya sauti.
Sehemu nyingine za kifaa hiki zina sumaku. Vitu vya chuma vinaweza kuvutwa na kifaa. Usiweke
kadi za mkopo au kadi nyingine zenye mkanda wa sumaku karibu na kifaa kwa kipindi cha muda
mrefu, kwa kuwa kadi hizo zinaweza kuharibika.
12. Kipaza sauti
INGIZA SIM NA KADI ZA KUMBUKUMBU
Ingiza kadi
1. Fungua trei ya SIM kadi: sukuma pini ya kufungua trei ndani ya shimo la trei na uondoe trei.
2. Weka nano-SIM kwenye kipenyo cha 1 kwenye trei na eneo la mguso likiangalia chini. Ikiwa
una simu ya SIM mbili, ingiza SIM ya pili kwenye kipenyo cha 2.
3. Ikiwa una kadi ya kumbukumbu, iingize kwenye kipenyo cha kadi ya kumbukumbu.
4. Telezesha trei ndani.
Tumia kadi halisi ya nano-SIM tu. Matumizi ya SIM kadi zisizotangamana huenda yakaharibu
kadi au kifaa, na huenda yakaharibu data iliyohifadhiwa kwenye kadi.
Tumia tu kadi za kumbukumbu zinazotangamana zilizoidhinishwa kutumiwa na kifaa hiki. Kadi
zisizotangamana zinaweza kuharibu kadi na kifaa na kuharibu data iliyohifadhiwa kwenye kadi.
CHAJI SIMU YAKO
Chaji betri
1. Chomeka chaja inayotangamana kwenye soketi ya ukuta.
2. Unganisha kebo kwenye simu yako.
Simu yako inakubali kebo ya USB ya micro-B. Pia unaweza kuchaji simu yako kutoka kwenye
kompyuta kwa kutumia kebo ya USB, lakini inaweza kuchukua muda mrefu zaidi.
Kama betri imeisha moto kabisa, huenda ikachukua dakika kadhaa kabla ya kiashiria chaji
kuonyeshwa.
WASHA NA USANIDI SIMU YAKO
Wakati unapowasha simu yako kwa mara ya kwanza, simu yako hukuelekeza usanidi
miunganisho ya mtandao na mipangilio ya simu yako.
Washa simu yako
1. Kuwasha simu yako, bonyeza na ushikilie kitufe cha nishati hadi simu iteteme.
2. Wakati simu imewashwa, chagua lugha na eneo lako.
2. Chagua ni data gani unayotaka irejeshwe kwenye simu yako mpya. Usawazishaji huanza
kiotomatiki punde simu yako inapounganishwa kwenye intaneti.
Rejesha mipangilio ya programu kutoka kwenye simu yako ya awali ya Android™
Ikiwa simu yako ya awali ilikuwa ya Android, na uhifadhi nakala ya akaunti ya Google kwayo,
unaweza kurejesha mipangilio ya programu yako na manenosiri ya Wi-Fi.
1. Gusa Mipangilio > Mfumo > Hifadhi nakala rudufu .
2. Badilisha Hifadhi nakala kwenye Google Drive kwa Washa .
MIPANGILIO YA SIM MBILI
Ikiwa una toleo la SIM mbili, unaweza kuwa na SIM 2 kwenye simu yako, kwa mfano, moja ya kazi
yako na nyingine ya matumizi yako ya kibinafsi.
Kumbuka: Kwenye vifaa vyenye uwezo wa SIM mbili, vipenyo vya SIM1 na SIM2 hukubali
mitandao ya 4G. Hata hivyo, ikiwa SIM1 na SIM2 zako ni kadi za SIM za LTE, mitandao msingi
hukubali mitandao ya 4G/3G/2G, wakati SIM ya pili inaweza kukubati tu 3G/2G. Kwa maelezo
zaidi kuhusu SIM kadi zako, wasiliana na mtoa huduma wako.
Chagua ni SIM gani ya kutumia
Kwa mfano, wakati unapiga simu, unaweza kuchagua ni SIM gani ya kutumia kwa kugusa kitufe
kinacholingana cha SIM 1 au SIM 2 baada ya kupiga nambari hiyo.
Simu yako huonyesha hali ya mtandao ya SIM zako kitofauti. SIM kadi zote zinapatikana kwa
wakati mmoja wakati kifaa hakitumiki, lakini wakai SIM kadi moja inatumika, kwa mfano, wakati
wa kupiga simu, ile nyingine inawezakosa kupatikana.
Dhibiti SIM zako
Hutaki kazi iingiliane na muda wako huru? Au una muunganisho wa bei nafuu wa data kwenye
SIM moja? Unaweza kuamua ni SIM gani unayotaka kutumia.
Gusa Mipangilio > Mtandao na Intaneti > SIM Kadi .
Skrini huzunguka kiotomatiki wakati unapindua simu kwa digrii 90.
Kufunga skrini katika hali ya wima, telezesha chini kutoka upande wa juu wa skrini, na uguse
Zungusha kiotomatiki .
Tumia vitufe vya urambazaji
• Ili kuona programu zote za programu,
telezesha juu kitufe cha nyumbani na
kisha ukitelezeshe juu tena.
• IIi kwenda kwenye skrini ya mwanzo, gusa
kitufe cha mwanzo. Programu uliyokuwa
ukitumia hubakia imefunguliwa chinichini.
• Ili kuona ni programu gani ulizofungua,
pitisha juu kwenye kitufe cha mwanzo.
• Ili kubadilisha kwa programu nyingine
iliyofunguliwa, pitisha kulia.
• Ili kufunga programu, ipitishe juu.
• Ili kufunga programu zote zilizofunguliwa,
telezesha kulia kupitia programu zote, na
uguse FUTA ZOTE .
• Ili kurejesha kwenye skrini ya awali
uliyokuwa, gusa kitufe cha nyuma . simu
yako hukumbuka programu na tovuti zote
ulizotembelea tangu wakati wa mwisho
skrini yako ilipofungwa.
2. Gusa Mlio wa simu wa SIM1 au > Mlio wa simu wa SIM2 ili uchague mlio wa simu wa kila
SIM.
Badilisha sauti ya taarifa ya ujumbe wako
Gusa Mipangilio > Sauti > Sauti chaguo-msingi ya arifa .
ARIFA
Pata kujua kinachoendelea kwenye simu yako kwa kutumia arifa.
Tumia paneli ya taarifa
Unapopokea arifa mpya, kama vile ujumbe au simu zisizojibiwa, aikoni ya kiashiriaji huonekana
kwenye upau wa hali juu ya skrini. Ili kuona maelezo zaidi kuhusu arifa, kokota chini upau wa
hali. Ili kufunga mwonekano, pitisha juu kwenye skrini.
Ili kufungua paneli ya arifa, kokota upau wa hali chini. Ili kufunga paneli ya arifa, pitisha juu
kwenye skrini.
Ili kubadilisha mipangilio ya taarifa ya programu, gusa Mipangilio > Programu na arifa > na
uguse jina la programu ili ufungue mipangilio ya programu. Gusa Arifa . Unaweza kuzima au
kuwasha arifa kwa kila programu kivyake.
Kidokezo: Ili kuona nukta za arifa, gusa Mipangilio > Programu na arifa > Arifa na
ubadilishe Ruhusu nukta za arifa kwa washa. Nukta ndogo itaonekana kwenye ikoni ya
programu, ikiwa una arifa, lakini bado hatujaishughulikia. Gusa na ushikilie ikoni ili kuona
chaguo zinazopatikana, Unaweza kugusa arifa ili kuifungua, au telezesha ili kupuuza.
Ili kuamilisha vipengele, gusa ikoni za mipangilio ya haraka kwenye paneli ya arifa. Ili kuona ikoni
zaidi, kokoa menyu chini.
Ili kupanga upya ikoni, gusa , gusa na ushikilie ikoni, na uikokote kwenye eneo lingine.
DHIBITI SAUTI
Badilisha sauti
Ikiwa una tatizo la kusikia simu yako ikiita katika mazingira yenye kelele, au simu ina sauti ya
juu, unaweza kubadilisha sauti kama upendavyo kwa kutumia vitufe vya sauti upande wa simu
yako.
Usiunganishe kwenye bidhaa ambazo zinaunda ishara ya kutoa, kwa kuwa hii inaweza kuharibu
kifaa. Usiunganishe chanzo chochote cha stima kwenye kiunganisha cha sauti. Ukiunganisha
kifaa chochote cha nje au vifaa vyovyote vya sauti kando na vile vilivyoidhinishwa kutumiwa na
kifaa hiki, Kiunganishi cha sauti, kuwa makini sana na viwango vya sauti.
Badilisha sauti ya midia na programu
Bonyeza kitufe cha sauti upande wa simu yako ili uone upau wa hali ya sauti, gusa , na
ukokote kitelezi kwenye upau wa sauti kwa midia na programu kushoto au kulia.
Weka simu kimya
Ili kuweka simu kuwa kimya, bonyeza kitufe cha kupunguza zaidi, gusa ili uweke simu yako
kutetema pekee na uguse ili kuiweka kimya.
Dokezo: Hutaki kuweka simu yako katika hali kimya, lakini huwezi kujibu sasa hivi? Ili
kunyamazisha simu inayoingia, bonyeza kitufe cha kupunguza sauti. Pia unaweza kuweka simu
yako kunyamazisha mlio wakati unapochukua simu: gusa Mipangilio > Mfumo > Ishara >
Nyamazisha ikichukuliwa , na uwashe.
Ikiwa unataka kuweza kukataa simu inayoingia kwa kupindua simu, gusa Mipangilio > Mfumo
> Ishara > Pindua ili ukatae simu , na uwashe.
USAHIHISHAJI MATINI KIOTOMATIKI
Jifunze jinsi ya kuandika maandishi kwa haraka na vizuri kwa kutumia usahihishaji matini wa
kibodi.
Tumia mapendekezo ya neno la kibodi
Simu yako hupendekeza maneno unapokuwa ukiandika, ili kukusaidia kuandika kwa haraka na
kwa usahihi zaidi. Mapendekezo ya maneno yanaweza kutopatikana katika lugha zote.
Wakati unapoanza kuandika neno, simu yako itapendekeza maneno yanayowezekana. Neno
unalotaka likionyeshwa kwenye upau wa mapendekezo, chagua neno. Ili kuona mapendekezo
zaidi, gusa na ushikilie pendekezo.
Dokezo: Ikiwa neno lililopendekezwa limewekwa alama ya koza, simu huitumia kiotomatiki
ili kubadilisha neno uliloandika. Ikiwa neno si sahihi, gusa na ushikilie ili kuona mapendekezo
mengine machache.
Ikiwa hutaki kibodi kupendekeza maneno unapokuwa ukicharaza, zima sahihisho za matini.
Gusa Mipangilio > Mfumo > Lugha na ingizo > Kibodi pepe . Teua kibodi unayotumia kwa
kawaida. Gusa Usahihishaji matini na uzime mbinu za kusahihisha matini ambayo hutaki
kutumia.
Sahihisha neno
Ukigundua ya kwamba umekosea tahajia ya neno, gusa ili kuona mapendekezo ya kusahihisha
neno.
Zima kikagua tahajia
Gusa Mipangilio > Mfumo > Lugha na ingizo > Mipangilio ya kina > Kikagua tahajia , na
uzime Tumia kikagua tahajia .
KISAIDIZI CHA GOOGLE
Kisaidizi cha Google hupatikana katika masoko na lugha zilizoteuliwa pekee. Ambapo
hakipatikani, Kisaidizi cha Google hubadilishwa kwa Utafutaji wa Google. Kisaidizi cha Google
kinaweza kukusaidia kwa mfano, kutafuta maelezo mtandaoni, kutafsiri maneno na sentensi,