Muhimu: Kwa maelezo muhimu kuhusu matumizi salama ya kifaa na betri yako, soma maelezo
ya ”Kwa usalama wako” na ”Usalama wa Bidhaa” katika mwongozo uliochapishwa wa mtumiaji,
au kwenye www.nokia.com/support kabla utumie kifaa. Ili kujua jinsi ya kuanza kutumia kifaa
chako kipya, soma mwongozo uliochapishwa wa mtumiaji.
Usiunganishe kwenye bidhaa ambazo zinaunda ishara ya kutoa, kwa kuwa hii inaweza kuharibu
kifaa. Usiunganishe chanzo chochote cha stima kwenye kiunganisha cha sauti. Ukiunganisha
kifaa chochote cha nje au vifaa vyovyote vya sauti kando na vile vilivyoidhinishwa kutumiwa na
kifaa hiki, Kiunganishi cha sauti, kuwa makini sana na viwango vya sauti.
Sehemu nyingine za kifaa hiki zina sumaku. Vitu vya chuma vinaweza kuvutwa na kifaa. Usiweke
kadi za mkopo au kadi nyingine zenye mkanda wa sumaku karibu na kifaa kwa kipindi cha muda
mrefu, kwa kuwa kadi hizo zinaweza kuharibika.
INGIZA AU ONDOA SIM NA KADI YA KUMBUKUMBU
Ingiza SIM na kadi ya kumbukumbu
1. Simu ikiangalia chini, weka kucha ya kidole
kingine cha SIM.
chako katika sehemu ndogo iliyokatwa
kwenye kona ya chini.
4. Ikiwa una kadi ya kumbukumbu ya
microSD, telezesha kadi kwenye kipenyo
2. Kunja kifuniko ili ufungue na uiondoe.
3. Telezesha kadi ya nano-SIM kwenye
kipenyo cha SIM eneo la chuma likiangalia
chini hadi ijifunge mahali pake. Ikiwa una
SIM mbili, ingiza SIM ya pili kwenye kipenyo
Onyo: Usifungue kifuniko cha betri, kinaweza kuharibu kifaa chako.
Kumbuka: Zima kifaa na utenganishe chaja na kifaa kingine chochote kabla ya kuondoa
vifuniko vyovyote. Epuka kugusu vijenzi vya elektroniki unapokuwa ukichaji vifuniko vyovyote.
Daima hifadhi na utumie kifaa na vifuniko vyovyote vilivyoambatishwa.
cha kadi ya kumbukumbu.
5. Bonyeza kona ya juu ya kifuniko cha nyuma
dhidi ya kona ya juu ya simu yako, na kisha
ufinye kifuniko mahali pake, ukifunga
viopoo vyote kwenye kona za kifuniko.
1. Ondoa kifuniko cha nyuma kutoka kwenye simu. Simu ikiangalia chini, weka kucha ya kidole
chako katika sehemu ndogo iliyokatwa kwenye kona ya chini.
2. Kunja kifuniko ili ufungue na uiondoe.
3. Ondoa kadi. Ili kuondoa SIM kadi kwenye kipenyo cha SIM2, unahitaji kuisukuma polepole ili
kuiachilie mahali pake.
1
Tumia kadi halisi ya nano-SIM tu. Matumizi ya SIM kadi zisizotangamana huenda yakaharibu
kadi au kifaa, na huenda yakaharibu data iliyohifadhiwa kwenye kadi.
CHAJI SIMU YAKO
Chaji betri
1. Chomeka chaja inayotangamana kwenye soketi ya ukuta.
2. Unganisha kebo kwenye simu yako.
Simu yako inakubali kebo ya USB ya micro-B. Pia unaweza kuchaji simu yako kutoka kwenye
kompyuta kwa kutumia kebo ya USB, lakini inaweza kuchukua muda mrefu zaidi.
Kama betri imeisha moto kabisa, huenda ikachukua dakika kadhaa kabla ya kiashiria chaji
kuonyeshwa.
WASHA NA USANIDI SIMU YAKO
Wakati unapowasha simu yako kwa mara ya kwanza, simu yako hukuelekeza usanidi
miunganisho ya mtandao na mipangilio ya simu yako.
Washa simu yako
1. Kuwasha simu yako, bonyeza na ushikilie kitufe cha nishati hadi simu iteteme.
2. Wakati simu imewashwa, chagua lugha na eneo lako.
2. Chagua ni data gani unayotaka irejeshwe kwenye simu yako. Usawazishaji utaanza
kiotomatiki punde simu yako inapounganishwa kwenye intaneti.
Rejesha mipangilio ya programu kutoka kwenye simu yako ya awali ya Android
Ikiwa kifaa chako cha awali kilikuwa cha Android , na uhifadhi nakala ya akaunti ya Google
kwayo, unaweza kurejesha mipangilio ya programu na manenosiri ya Wi-Fi.
1. Gusa Mipangilio > Hifadhi nakala na weka upya .
2. Badilisha Onyesha upya otomatiki kwa Washa .
MIPANGILIO YA SIM MBILI
Ikiwa una toleo la SIM mbili, unaweza kuwa na SIM 2 kwenye simu yako, kwa mfano, moja ya kazi
yako na nyingine ya matumizi yako ya kibinafsi.
Kumbuka: Kwenye vifaa vyenye uwezo wa SIM mbili, vipenyo vya SIM1 na SIM2 hukubali
mitandao ya 4G. Hata hivyo, ikiwa SIM1 na SIM2 zako ni kadi za SIM za LTE, mitandao msingi
hukubali mitandao ya 4G/3G/2G, wakati SIM ya pili inaweza kukubati tu 3G/2G. Kwa maelezo
zaidi kuhusu SIM kadi zako, wasiliana na mtoa huduma wako.
Chagua ni SIM gani ya kutumia
Kwa mfano, wakati unapiga simu, unaweza kuchagua ni SIM gani ya kutumia kwa kugusa kitufe
kinacholingana cha SIM 1 au SIM 2 baada ya kupiga nambari hiyo.
Simu yako huonyesha hali ya mtandao ya SIM zako kitofauti. SIM kadi zote zinapatikana kwa
wakati mmoja wakati kifaa hakitumiki, lakini wakai SIM kadi moja inatumika, kwa mfano, wakati
wa kupiga simu, ile nyingine inawezakosa kupatikana.
Dhibiti SIM zako
Hutaki kazi iingiliane na muda wako huru? Au una muunganisho wa bei nafuu wa data kwenye
SIM moja? Unaweza kuamua ni SIM gani unayotaka kutumia.
Skrini huzunguka kiotomatiki wakati unapindua simu kwa digrii 90.
Ili kufunga skrini katika hali mkao wima, telezesha chini kutoka juu ya skrini, na uguse
Zungusha kiotomatiki ili ubadilishe kwa Wima .
Tumia vitufe vya urambazaji
Ili kuona ni programu gani ulizofungua, gusa kitufe cha muhtasari .
Ili kubadilisha kwa programu nyingine, gusa programu unayotaka. Ili kufunga programu, gusa
ikoni ya kando yake.
Ili kurejesha kwenye skrini ya awali uliyokuwa, gusa kitufe cha nyuma . simu yako hukumbuka
programu na tovuti zote ulizotembelea tangu wakati wa mwisho skrini yako ilipofungwa.
Ili kwenda kwenye skrini ya mwanzo, gusa kitufe cha mwanzo . Programu uliyokuwa ukitumia
hubakia imefunguliwa chinichini.
Jifunze jinsi ya kubinafsisha Skrini ya mwanzo na jinsi ya kubadilisha toni za mlio.
Badilisha mandhari yako
Gusa Mipangilio > Skrini > Mandhari .
Badilisha toni yako ya mlio ya simu yako
1. Gusa Mipangilio > Sauti .
2. Gusa Mlio wa simu wa SIM1 au Mlio wa simu wa SIM2 ili uchague mlio wa simu wa kila SIM.
Badilisha toni ya mlio ya taarifa ya ujumbe wako
1. Gusa Mipangilio .
2. Gusa Sauti .
3. Gusa Toni ya mlio ya chaguo-msingi ya arifa .
FUNGUA NA UFUNGE PROGRAMU
Fungua programu
Kwenye skrini ya mwanzo, gusa ikoni ya programu ili kuifungua. Ili kufungua mojawapo ya
programu zinazoendeshwa kichini chini, gusa , na uchague programu.
Fungua programu
Gusa , na uguse kwenye programu unayotaka kufunga.
Tafuta programu zako
Kwenye skrini ya mwanzo, telezesha juu kuanzia chini ya skrini ili uone programu zako zote.
Bonyeza , pitisha juu kwenye programu zote, na uguse ONDOA ZOTE .
ARIFA
Pata kujua kinachoendelea kwenye simu yako kwa kutumia arifa.
Tumia paneli ya taarifa
Unapopokea arifa mpya, kama vile ujumbe au simu zisizojibiwa, aikoni ya kiashiriaji huonekana
kwenye upau wa hali juu ya skrini. Ili kuona maelezo zaidi kuhusu aikoni, fungua paneli ya taarifa
na uangalie maelezo.
Ili kufungua paneli ya arifa, kokota upau wa hali kuelekea chini. Ili kufunga paneli ya arifa,
pitisha juu kwenye skrini.
Ili kubadilisha mipangilio ya taarifa ya programu, gusa Mipangilio > Arifa na uguse jina la
programu ili ufungue mipangilio ya programu.
Tumia ikoni za mpangilio wa haraka
Ili kuamilisha vipengele, gusa ikoni za mipangilio ya haraka kwenye paneli ya arifa. Ili kuona ikoni
zaidi, kokoa menyu chini.
Ili kupanga upya ikoni, gusa , gusa na ushikilie ikoni, na uikokote kwenye eneo lingine.
Ikiwa una tatizo la kusikia simu yako ikiita katika mazingira yenye kelele, au simu ina sauti ya
juu, unaweza kubadilisha sauti kama upendavyo kwa kutumia vitufe vya sauti upande wa simu
yako.
Usiunganishe kwenye bidhaa ambazo zinaunda ishara ya kutoa, kwa kuwa hii inaweza kuharibu
kifaa. Usiunganishe chanzo chochote cha stima kwenye kiunganisha cha sauti. Ukiunganisha
kifaa chochote cha nje au vifaa vyovyote vya sauti kando na vile vilivyoidhinishwa kutumiwa na
kifaa hiki, Kiunganishi cha sauti, kuwa makini sana na viwango vya sauti.
Badilisha sauti ya midia na programu
Bonyeza kitufe cha sauti upande wa simu yako ili uone upau wa hali ya sauti, gusa , na
ukokote kitelezi kwenye upau wa sauti kwa midia na programu kushoto au kulia.
Weka simu kimya
Bonyeza kitufe cha sauti kwenye upande wa simu yako, na uguse ili kuifanya iwe kimya.
Dokezo: Hutaki kuweka simu yako katika hali kimya, lakini huwezi kujibu sasa hivi? Ili
kunyamazisha simu inayoingia, bonyeza kitufe cha kupunguza sauti . Unaweza kuweka
simu yako kunyamazisha mlio wa simu ukiichukua: Gusa Mipangilio > Mwendo >
Nyamazisha ikichukuliwa .
Kama unataka kuweza kukataa simu kwa haraka, wezesha Mwendo. gusa Mipangilio >
Mwendo > Pindua ili ukatae simu . Wakati kuna simu inayoingia, pindua simu ili ukatae simu.
PICHA ZA SKRINI
Piga picha ya skrini
Ili kupiga picha ya skrini, fungua paneli ya arifa, na ukokote upau wa hali kuelekea chini. Gusa
Nasa skrini . Unaweza kutazama picha zilizonaswa katika Picha .
Haiwezekani kunasa picha ya skrini wakati unatumia baadhi ya programu na vipengele.
2. Chagua tu sauti ambazo unazihitaji:
Nyamazisha sauti zisizohitajika, kama vile
sauti za kubofya vitufe. Gusa Mipangilio >
Sauti , na chini ya Sauti nyingine , chagua
ni sauti gani za kuweka.
3. Tumia vifaa vya sauti vyenye waya, badala
ya kipasa sauti.
4. Badilisha mipangilio ya skrini ya simu:
Weka skrini ya simu ili kuzima baada ya
muda mfupi. Gusa Mipangilio > Skrini >
Lala na uchague muda.
5. Punguza mwangaza wa skrini:
Gusa Mipangilio > Skrini >
Hali ya mwangaza . Hakikisha kwamba
Mwangaza uliorekebishwa umewezeshwa.
Ili kurekebisha mwangaza, kokota kitelezi
cha Hali ya mwangaza .
6. Komesha programu zinazoendeshwa
kichini chini: Bonyeza , na ufunge
programu ambazo hauhitaji.
7. Wezesha Kidhibiti cha shughuli za
chinichini. Taarifa za baadhi ya programu
au barua pepe huenda zisiweze kuepuliwa
mara moja. Unaweza kudhibiti maisha
ya betri kwa kuongeza au kuondoa
programu kwenda au kutoka orodha ya
zilizoruhusiwa. Gusa Mipangilio > Betri >
Kidhibiti cha shughuli za chinichini .
8. Wezesha Kiokoa betri . Gusa Mipangilio
> Betri > Kiokoa betri , na ubadilishe kwa
Washa .
9. Tumia huduma za eneo kwa kuchagua:
Zima huduma za eneo wakati hauzihitaji.
Gusa Mipangilio > Eneo , na ubadilishe
kwa Zima .
10. Tumia miunganisho ya mtandao kwa
kuchagua: Washa Bluetooth wakati
inahitajika tu. Tumia muunganisho wa
Wi-Fi ili uunganishe kwenye intaneti,
badala ya muunganisho wa data ya simu
ya mkononi. Komesha simu yako kutafuta
mitandao inayopatikana ya pasi waya.
Gusa Mipangilio > Wi-Fi , na ubadilishe
kwa Zima . Kama unasikiliza muziki au
unatumia simu yako, lakini hutaki kupiga
au kupokea simu, washa hali ya Ndege.
Gusa Mipangilio > Zaidi > Hali ya ndege .
Hali ya ndege hufunga miunganisho kwenye mitandao ya simu za mkononi na huzima vipengele
pasiwaya vya kifaa chako.
OKOA GHARAMA YA UTUMIAJI DATA NJE YA MTANDAO WAKO WA KAWAIDA
Unaweza kupunguza gharama za utumiaji data nje ya mtandao wako wa kawaida na kuokoa
pesa kwenye bili ya simu yako kwa kubadilisha mipangilio ya data ya simu ya mkononi. Ili
kutumia mbinu bora ya muunganisho, badilisha mipangilio ya Wi-Fi na mitandao ya simu.
Utumiaji data nje ya mtandao wako wa kawaida humaanisha kutumia simu yako kupokea
data kwenye mitandao ambayo mtoa huduma wako wa mtandao hamiliki au kuendesha.
Kuunganisha kwenye intaneti wakati unatumia data ya nje ya mtandao wako wa kawaida, hasa
ukiwa ng’ambo, kunaweza kupandisha gharama ya data pakubwa. Kutumia muunganisho wa
Wi-Fi kwa kawaida huwa haraka na bei nafuu kuliko kutumia muunganisho wa data ya simu
ya mkononi. Kama miunganisho yote ya Wi-Fi na data ya simu ya mkononi inapatikana, simu
hutumia muunganisho wa Wi-Fi.
2. Hakikisha mtandao wa Wi-Fi umewekwa kwa Washa .
3. Chagua muunganisho unaotaka kutumia.
Funga muunganisho wa data ya simu ya mkononi
Telezesha chini kuanzia juu ya skrini, gusa na ubadilishe Data ya simu ya mkononi kwa
Zima .
Ili kufuata matumizi ya data yako, gusa Mipangilio > Matumizi ya data .
Komesha utumiaji data nje ya mtandao wako wa kawaida
Gusa Mipangilio > Zaidi > Mitandao ya simu za mkononi , na uzime
Utumiaji data nje ya mtandao wako wa kawaida .
ANDIKA MAANDISHI
Jifunze jinsi ya kuandika maandishi kwa haraka na vizuri kwa kutumia kibodi ya simu yako.
Tumia kibodi kwenye skrini
Kuandika kwa kutumia kibodi kwenye skrini ni rahisi. Unaweza kutumia kibodi ukiwa umeshikilia
simu yako katika hali wima au mlalo. Mpangilio wa kibodi unaweza kutofautiana katika
programu na lugha tofauti.
Ili kufungua kibodi kwenye skrini, gusa kisanduku cha maandishi.
Badilisha kati ya vibambo vikubwa na vidogo
Gusa kitufe cha shift. Ili kuwasha hali ya caps lock, gusa kitufe mara mbili. Ili kurejea hali ya
kawaida, gusa tena kitufe cha shift.
Charaza namba au kibambo maalum
Gusa nambari na Kitufe cha alama. Baadhi vitufe vya vibambo maalum huleta alama zaidi. Ili
kuona alama zaidi, gusa na ushikilie alama au kibambo maalum.
Gusa na ushikilie neno, kokota viweka alama kabla na baada ya neno ili kuangazia sehemu
unayotaka kunakili na uguse NAKILI . Ili kubandika maandishi, gusa ni wapi unataka kubandika
maandishi na uchague BANDIKA .
Ongeza lafudhi kwa kibambo
Gusa na ushikilie kibambo, na uguse lafudhi au kibambo cha lafushi, ikiwa inakubaliwa na kibodi
yako.
Futa kibambo
Gusa kitufe cha backspace.
Sogeza kasa
Ili kuhariri neno uliloandika, gusa neno, na uburute kasa mahali unapoitaka.
Tumia mapendekezo ya neno la kibodi
Simu yako hupendekeza maneno unapokuwa ukiandika, ili kukusaidia kuandika kwa haraka na
kwa usahihi zaidi. Mapendekezo ya maneno yanaweza kutopatikana katika lugha zote.
Wakati unapoanza kuandika neno, simu yako itapendekeza maneno yanayowezekana. Neno
unalotaka likionyeshwa kwenye upau wa mapendekezo, chagua neno. Ili kuona mapendekezo
zaidi, gusa na ushikilie pendekezo.
Ikiwa neno lililopendekezwa limewekwa alama ya koza, simu huitumia kiotomatiki ili
kubadilisha neno uliloandika. Ikiwa neno si sahihi, gusa na ushikilie ili kuona mapendekezo
mengine machache.
Ikiwa hutaki kibodi kupendekeza maneno unapokuwa ukicharaza, zima sahihisho za matini.
Gusa Mipangilio > Lugha na ingizo > Kibodi pepe . Teua kibodi unayotumia kwa kawaida.
Gusa Usahihishaji matini na uzime mbinu za kusahihisha matini ambayo hutaki kutumia.
Sahihisha neno
Ukigundua ya kwamba umekosea tahajia ya neno, gusa ili kuona mapendekezo ya kusahihisha
neno.