Muhimu: Kwa maelezo muhimu kuhusu matumizi salama ya kifaa na betri yako, soma maelezo
ya ”Kwa usalama wako” na ”Usalama wa Bidhaa” katika mwongozo uliochapishwa wa mtumiaji,
au kwenye www.nokia.com/support kabla utumie kifaa. Ili kujua jinsi ya kuanza kutumia kifaa
chako kipya, soma mwongozo uliochapishwa wa mtumiaji.
Usiunganishe kwenye bidhaa ambazo zinaunda wimbi la kutoa, kwa kuwa hii inaweza kuharibu
kifaa. Usiunganishe chanzo chochote cha stima kwenye kiunganisha cha sauti. Ukiunganisha
kifaa chochote cha nje au kifaa chochote cha kichwa kando na zile zilizoidhinishwa kutumiwa
na kifaa hiki, Kiunganishi cha sauti, kuwa makini sana na viwango vya sauti. Sehemu nyingine
za kifaa hiki zina sumaku. Vitu vya chuma vinaweza kuvutwa na kifaa. Usiweke kadi za karadha
au vitu vingine vyenye kutumia hifadhi ya sumaku karibu na kifaa hiki, kwa sababu maelezo
yaliyohifadhiwa kwenye vitu hivyo yanaweza kufutika.
Baadhi ya vifaa vya ziada vilivyotajwa katika mwongozo huu wa mtumiaji, kama vile chaja,
vipokea sauti vya kichwani, au waya wa data, vinaweza kuuzwa kando.
Dokezo: Unaweza kuweka mpangilio ili simu yako iombe msimbo wa usalama ili kulinda
faragha na data yako binafsi. Chagua Menyu > Mipangilio > Usalama > Kilinzi cha vitufe >
Msimbo wa usalama kisha uweke msimbo. Hata hivyo kumbuka kwamba unahitaji kukumbuka
msimbo huo, kwani HMD Global haiwezi kuufungua au kuuruka.
SANIDI NA UWASHE SIMU YAKO
Nano-SIM
Muhimu: Kifaa hiki kimeundwa ili kutumiwa na SIM kadi ya nano pekee (angalia mfano).
Matumizi ya kadi zisizotangamana za SIM zinaweza kuharibu kadi au kifaa, na zinaweza
kuharibu data iliyohifadhiwa kwenye kadi.
Kumbuka: Zima kifaa na usiiunganishe na chaja au kifaa kingine chochote kabla ya kubandua
vifuniko vyovyote. Epuka kugusa visehemu vya elektroniki wakati wa kubadilisha vifuniko
vyovyote. Daima hifadhi na kutumia kifaa kikiwa na vifuniko vyake vimewekwa.
Ikiwa una simu ya matundu mawili ya SIM, ingiza kadi yako ya SIM kwenye tundu la SIM1 na SIM
ya pili kwenye tundu la SIM2. Kadi zote mbili za SIM zinapatikana kwa wakati mmoja wakati kifaa
hakitumiki, lakini kadi moja ya SIM inapokuwa ikitumika, kwa mfano, wakati wa kupiga simu, ile
ya pili haipatikani.
Kidokezo: Ili kujua ikiwa simu yako inaweza kutumia SIM kadi 2, angalia lebo kwenye sanduku
la mauzo. Ikiwa kuna misimbo 2 ya IMEI kwenye lebo, una simu yenye SIM mbili.
Ingiza kadi ya kumbukumbu
1. Telezesha chini kishikizi cha kadi ya
kumbukumbu kisha ukifungue.
2. Weka kadi ya kumbukumbu kwenye tundu.
3. Funga kishikizi na ukitelezeshe juu ili
kukifunga.
Kidokezo: Tumia kadi ya kumbukumbu ya microSD yenye kasi, na ya hadi GB 32 kutoka kwa
mtengenezaji anayefahamika.
Washa simu yako
Bonyeza na ushikilie .
CHAJI SIMU YAKO
Betri yako imechajiwa nusu kiwandani, lakini utahitajika kuichaji upya kabla uweze kutumia simu
yako.
Chaji betri
1. Chomeka chaja kwenye soketi ya ukuta.
2. Unganisha chaja kwenye simu. Ukimaliza, chomoa chaja kwenye simu, kisha kwenye soketi
ya ukuta.
Kama betri imeisha moto kabisa, huenda ikachukua dakika kadhaa kabla ya kiashiria chaji
kuonyeshwa.
Kidokezo: Unaweza kuchaji kwa kutumia USB wakati umeme wa ukutani haupatikani. Ubora
wa nishati ya kuchaji kwa USB hutofautiana, na huenda ikachukua muda mrefu kuchaji kuanza
na kifaa kuanza kufanya kazi.
VITUFE
Tumia vitufe vya simu
• Ili kuona programu na vipengele vya simu yako, kwenye skrini ya mwanzo, chagua Menyu .
• Ili kwenda kwenye programu au kipengele, bonyeza kitufe cha kutambaza juu, chini,
kushoto, au kulia. Ili kufungua programu au kipengele, bonyeza kitufe cha kutambaza.
• Kurudi kwa skrini ya mwanzo, bonyeza kitufe cha kukata simu.
• Ili kubadilisha sauti ya simu yako wakati unaongea kwenye simu au unaposikiliza redio,
bonyeza vitufe vya sauti.
Funga kicharazio
Ili kufunga vitufe, funga tundu. Ili kufungua vitufe, bonyeza kitufe cha kutelezesha kisha
uchague Fungua > * .
Ili kuchagua jinsi menyu ya programu inavyoonyeshwa kwenye skrini, chagua Menyu >
Mipangilio > Mfumo > Mwonekano mkuu wa menyu kisha uchague 3x3 ili kuona programu
9 katika menyu kwa wakati mmoja au 1x1 kuona programu 1 kwa wakati. Ukichagua 1x1 ,
telezesha juu au chini ili kuvinjari kati ya programu.
Ongeza maelezo yako ya ICE
Ili kuweza kupiga simu za DHARURA, unahitaji kuongeza maelezo yako ya DHARURA (Katika Hali
ya Dharura).
1. Ongeza maelezo yako binafsi: chagua Menyu > Mipangilio > Kifaa > taarifa ya ICE >
Taarifa ya msingi na Taarifa muhimu .
2. Chagua waasiliani ambao wanapigiwa simu ya DHARURA: chagua Menyu > Mipangilio
> Kifaa > SOS > Wawasiliani wa ICE , kisha uchague wawasiliani wa ICE kutoka kwenye
orodha yako ya wawasiliani. Kumbuka kwamba huwezi kutumia nambari rasmi za dharura
kama majina yako ya ICE.
3. Kabla ya kupiga simu za SOS, unahitaji kuziwezesha. Chagua Menyu > Mipangilio > Kifaa
> SOS > Mipangilio ya SOS , kisha uwashe simu ya SOS .
Bonyeza na ushikilie kitufe cha simu ya SOS kwa sekunde chache. Simu inampigia mwasiliani
wako wa kwanza wa ICE. Mwasiliani asipojibu ndani ya sekunde 25, simu itapiga simu kwa
mwasiliani anayefuata, na itaendelea kupigia wawasiliani wako hadi mmoja wao ajibu simu, au
ubonyeze . Kumbuka: Wakati simu ya SOS imejibiwa, simu inaenda katika hali isiyotumia
mikono. Usiweke simu karibu na sikio lako, kwani sauti inaweza kuwa kubwa sana.
Unaweza kurejesha mipangilio halisi ya kiwandani, lakini kuwa makini, kwa kuwa uwekaji huu
upya huondoa data yote uliyohifadhi kwenye kumbukumbu ya simu na ubinafsishaji wako wote.
Kama unatuma simu yako, kumbuka kwamba unawajibika kuondoa maudhui yote ya kibinafsi.
Ili kuweka upya simu yako kwa mipangilio yake halisi na kuondoa data yako yote, kwenye skrini
ya mwanzo, andika *#7370#. Ukiulizwa, ingiza msimbo wako wa usalama.
Soma maelekezo haya rahisi. Kutoyafuata kunaweza kuwa hatari au kinyume cha sheria na
masharti. Kwa maelezo zaidi, soma mwongozo kamili wa mtumiaji.
ZIMA KATIKA MAENEO YALIYOKATAZWA
Zima kifaa wakati matumizi ya kifaa cha mkononi yamekatazwa au wakati yanaweza
kusababisha mwingiliano au hatari, kwa mfano, ndani ya ndege au hospitalini, au karibu na vifaa
vya matibabu, mafuta, kemikali, au maeneo yenye mlipuko. Tii maagizo yote katika maeneo
yaliyozuiwa.
USALAMA BARABARANI HUJA KWANZA
Tii sheria zote za mahali ulipo. Daima iache mikono yako iwe huru kuendesha gari. Kitu cha
kuzingatia kwanza unapoendesha gari unapaswa kuwa usalama barabarani.
Vifaa vyote visivyotumia waya vina uwezekano wa kupata mwingiliano, ambao unaweza kuathiri
utendaji kazi wake.
HUDUMU ILIYOIDHINISHWA
Watu walioidhinishwa tu ndio wanaweza kuweka au kukarabati bidhaa hii.
BETRI, CHAJA, NA VIFAA VINGINE VYA ZIADA
Tumia betri, chaja, na vifaa vya ziada ambavyo vimeidhinishwa na HMD Global Oy kwa ajili ya
matumizi na kifaa hiki tu. Usiunganishe bidhaa ambazo hazitangamani.
WEKA KIFAA KIKIWA KIKAVU
Ikiwa kifaa chako kinazuia maji, angalia ukadiriaji wake wa IP katika ainisho za kiufundi za kifaa
kwa maelekezo zaidi tondoti.
Kuzuia madhara yanayowezekana ya kusikia, usisikilize katika viwango vya juu vya sauti kwa
muda mrefu. Kuwa mwangalifu wakati unashikilia kifaa chako karibu na sikio wakati kipaza sauti
kinatumika.
SAR
Kifaa hiki kinatimiza matakwa ya maelekezo ya ujiwekaji wazi kwa frikwensi za redio wakati
kikitumika ama kwenye mkao wa kawaida kwenye sikio au wakati kikiwekwa angalau sentimita
1.5 (inchi 5/8) kutoka kwenye mwili. Thamani maalum za juu za SAR zinaweza kupatikana
katika sehemu ya Maelezo ya Cheti ya (SAR) ya mwongozo huu wa mtumiaji. Kwa maelezo zaidi,
angalia sehemu ya Maelezo ya Cheti (SAR) ya mwongozu huu wa mtumiaji au nenda kwenye
www.sar-tick.com.
SIMU ZA DHARURA
Muhimu: Miunganisho katika hali zote haiwezi kuhakikishwa. Kamwe usitegemee tu simu
pasiwaya kwa mawasiliano muhimu kama vile tiba za dharura.
Kabla ya kupiga simu:
• Washa simu.
• Kama skrini na vitufe vya simu vimefungwa, vifungue.
• Nenda eneo lenye mawimbi ya simu ya kutosha.
1. Bonyeza kitufe cha kukata simu kwa kurudia, hadi skrini ya mwanzo ionyeshwe.
2. Charaza namba rasmi ya dharura ya eneo lako la sasa. Nambari za simu ya dharura
hutofautiana kimaeneo.
3. Bonyeza kitufe cha simu.
4. Toa maelezo yanayofaa kwa usahihi kama iwezekanavyo. Usikate simu hadi upewe ruhusa ya
kufanya hivyo.
Huenda pia ukahitajika kufanya yafuatayo:
• Weka SIM kadi ndani ya simu.
• Ikiwa simu yako itakuuliza msimbo wa PIN, charaza nambari rasmi ya dharura ya eneo lako la
sasa, na ubonyeze kitufe cha simu.
• Zima vizuizi vya simu katika simu yako, kama vile uzuiaji simu, upigaji uliopangwa, au kikundi
maalum cha watumiaji.
KUHUDUMIA KIFAA CHAKO
Shughulikia kifaa chako, betri, chaja na vifaa vya ziada kwa uangalifu. Mapendekezo yafuatayo
yatakusaidia kufanya kifaa chako kifanye kazi.
• Weka kifaa kikiwa kikavu. Taka za
mtuamo, unyevu wa hewa, na aina zote
za vimiminiko au unyevu zinaweza kuwa
na madini yanayoweza kutia kutu saketi za
elektroniki.
• Usitumie au kuhifadhi kifaa chako kwenye
maeneo yenye vumbi au uchafu.
• Usihifadhi kifaa kwenye halijoto ya juu au
ya chini. Halijoto ya juu huenda ikaharibu
kifaa au betri.
• Usihifadhi kifaa kwenye halijoto baridi.
Wakati kifaa kimerudi kwenye joto
lake la kawaida, unyevunyevu unaweza
kutengenezeka ndani ya kifaa.
• Usifungue kifaa kando na ilivyoagizwa
katika kiongozi cha mtumiaji.
• Mabadiliko yasioidhinishwa yanaweza
kuharibu kifaa hiki na kukiuka sheria
zinazosimamia vifaa vya redio.
• Usiangushe, kugonga, au kutingisa kifaa
au betri. Kukishika kiholela kunaweza
kuivunja.
• Tumia kitambaa laini, kisafi na kikavu
kusafisha uso wa kifaa hiki.
• Usipake rangi kifaa. Rangi inaweza kuzuia
utendaji kazi wa kawaida.
• Weka kifaa chako mbali na sumaku au
maeneo ya sumaku.
• Ili kuweka data yako muhimu salama,
ihifadhi angalau katika maeneo mawili
tofauti, kama vile kifaa chako, kadi ya
kumbukumbu, au kompyuta au andika
maelezo muhimu.
Wakati wa utendajikazi kwa muda mrefu, kifaa kinaweza kuwa na joto. Katika hali nyingi, hii
ni kawaida. Kuepuka kupata joto sana, huenda kifaa kikapunguza kasi kiotomatiki, kikafunga
programu, kikazima kuchaji, na ikiwezekana, kikajizima. Kama kifaa hakifanyi kazi sawasawa,
kipeleke kwenye kitengo cha mtengenezaji aliyeidhinishwa kilicho karibu.
Daima rudisha bidhaa zako za elektroniki, betri na nyezo za kifurushi zilizotumiwa kwa maeneo
maalum ya ukusanyaji. Kwa njia hii utasaidia kuzuia utupaji taka usiodhibitiwa na kukuza
uchakataji upya wa nyenzo. Bidhaa za umeme na elektroniki huwa na nyenzo nyingi za thamani,
ikiwa ni pamoja na madini (kama vile shaba, aluminiamu, chuma, na magnesiamu) na madini ya
thamani (kama vile dhahabu, fedha, na paladiamu) Nyenzo zote za kifaa zinaweza kufufuliwa
kama nyenzo na nishati.
ALAMA YA PIPA ILIYO NA MKATO
Alama ya pipa iliyo na mkato
Alama ya pipa iliyo na mkato kwenye bidhaa, betri, maandishi, au kifurushi chako
hukukumbusha kwamba bidhaa zote za elektroniki na betri lazima zipelekwe kwenye
mkusanyiko tofauti wakati bidhaa inapokwisha. Usitupe bidhaa hizi kama takataka
zisizochambuliwa za manispaa: zipeleke zichakatwe. Kwa maelezo juu ya eneo la uchakataji lililo
karibu na wewe, wasiliana na mamlaka ya taka ya eneo lako.
MAELEZO YA BETRI NA CHAJA
Maelezo ya betri na chaja
Ili ukague ikiwa simu yako ina betri inayoweza kuondolewa au isiyoweza kuondolewa, angalia
Mwongozo wa kuanza kutumia.
Vifaa vilivyo na beti inayoweza kuondolewa Tumia kifaa chako na betri halisi tu inayoweza
kuchajiwa upya. Betri inaweza kuchajiwa na kuondolewa chaji hata mara mia, lakini hatimaye
itachoka. Wakati muda wa kuongea na muda wa kusubiri unaonekana wazi kuwa mfupi kuliko
kawaida, badilisha betri.
Vifaa vilivyo na betri isiyoweza kuondolewa Usijaribu kuitoa betri, kwa sababu unaweza
kuharibu kifaa. Betri inaweza kuchajiwa na kuondolewa chaji hata mara mia, lakini hatimaye
itachoka. Wakati muda wa kuongea na muda wa kusubiri unaonekana wazi kuwa mfupi kuliko
kawaida, kubadilisha betri, peleka kifaa hicho kwenye kitengo cha mtengenezaji aliyeidhinishwa
kilicho karibu.
Chaji kifaa chako na chapa inayotangamana. Aina ya plagi ya chaja huenda ikatofautiana. Muda
wa kuchaji unaweza kutofautiana kulingana na uwezo wa kifaa.
Maelezo ya usalama wa betri na chaja
Kifaa chako kikikamiliza kuchajiwa, chomoa chaja kutoka kwenye kifaa na soketi ya umeme.
Tafadhali kumbuka kwamba kuchaji kwa mfululizo hakupaswi kuzidi saa 12. Ikiachwa bila
kutumika, betri iliyokuwa imejaa chaji itapoteza chaji yake kadri muda unavyopita.
Halijoto ya juu sana hupunguza uwezo na maisha ya betri. Daima jaribu kuweka betri kwenye
halijoto kati ya 15°C na 25°C (59°F na 77°F) kwa utendakazi bora. Kifaa chenye betri moto au
baridi kinaweza kisifanye kazi kwa muda. Kumbuka kwamba huenda betri ikaisha haraka katika
halijoto baridi na kupoteza nishati ya kutosha na kuzima simu katika dakika chache. Ukiwa nje
katika halijoto baridi, weka simu yako ikiwa na joto kiasi.
Tii sheria za eneo lako. Peleka ichakatwe upya ikiwezekana. Usitupe kama takataka za kawaida
za nyumbani.
Usiweke betri kwenye shinikizo la chini sana la hewa au kuiwacha kwenye halijoto ya juu sana,
kwa mfano kuitupa kwenye moto, kwa kuwa hiyo inaweza kusababisha betri kulipuka au kuvuja
kiowevu au gesi inayoweza kuwaka moto.
Usifungue, kukata, kuvunja, kukunja, kutoa, au kuharibu betri kwa njia yoyote ile. Kama betri
itavuja, usiruhusu umaji uguse ngozi au macho. Hii ikifanyika, osha maeneo yaliyoathirika mara
moja na maji, au tafuta msaada wa kitabibu. Usirekebishe, kujaribu kuingiza vitu vigeni kwenye
betri, au kuizamisha au kuiweka kwenye maji au aina nyingine ya umaji. Betri zinaweza kulipuka
kama zimeharibika.
Tumia betri na chaja kwa matumizi yaliyokusudiwa tu. Matumizi mabaya, au matumizi
yasiyoidhinishwa au yasiyotangamana na betri au chaja huenda yakaleta hatari ya moto,
mlipuko au hatari nyingine, na huenda ikabatilisha uhalali wowote ulioidhinishwa au waranti.
Kama unaamini betri au chaja imeharibika, ipeleke kwa kituo cha huduma au muuza simu
yako kabla ya kuendelea kuitumia. Kamwe usitumie betri au chaja yoyote iliyoharibika.
Tumia chaja ndani ya nyumba tu. Usichaji kifaa chako wakati wa dhoruba ya radi. Wakati
chaja haijajumuishwa katika furushi la mauzo, chaji kifaa chako kwa kutumia kebo ya data
(iliyojumuishwa) na adapta ya nishati ya USB (inaweza kuuzwa kando). Unaweza kuchaji kifaa
chako na kebo za wahusika wengine na adapta za nishati ambazo zinatangamana na USB 2.0
au baadaye na kanuni husika za nchi na viwango vya usalama vya kimataifa na mkoa. Huenda
adapta nyingine zisitimize viwango husika vya usalama, na kuchaji kwa kutumia adapta hizo
kunaweza kusababisha hatari ya kupoteza mali au majeraha ya kibinafsi.
Ili kuchopoa chaja au kifaa chochote cha ziada, kamata na uvute plagi na siyo waya.
Kwa kuongezea, zifuatazo hutumika ikiwa kifaa chako kina betri inayoweza kuondolewa:
• Daima zima na ung’oe chaja kabla ya kuondoa betri.
• Mkato wa umeme wa bahati mbaya unaweza kutokea kwa bahati mbaya kama kitu cha
chuma kitagusa vipapi vya chuma kwenye betri. Huenda hii ikaharibu betri au kifaa kile
kingine.
WATOTO WADOGO
Kifaa chako na viboreshaji vyake sio sesere. Vinaweza kuwa na sehemu ndogo ndogo. Viweke
mbali na watoto wadogo.
VIFAA VYA MATIBABU
Utendajikazi wa kifaa cha kupitisha mawimbi ya redio, pamoja na simu zisizotumia waya, huenda
zikaingiliana na utendaji wa vifaa vya matibabu visivyokingwa vizuri. Wasiliana na daktari au
mtengenezaji wa kifaa cha matibabu ili ubainishe kama kimekingwa vizuri dhidi ya nguvu ya nje
ya radio.
VIFAA VYA MATIBABU VINAVYOPACHIKWA
Kuepuka mwingiliano unaowezekana, watengenezaji wa vifaa vilivyopachikwa vya matibabu
(kama vile vipima mapigo ya moyo, pampu za insulini, na yurostimuleta wanapendekeza nafasi
isiyopungua sentimita 15.3 (inchi 6) kati ya kifaa kisichotumia waya na kifaa cha matibabu.
Watu ambao wana vifaa kama hivyo wanapaswa:
• Daima weka kifaa kisichotumia waya kwa
umbali wa sentimita 15.3 (inchi 6) kutoka
kwa kifaa cha matibabu.
• Usibebe kifaa pasiwaya katika mfuko wa
shati.
• Shikilia kifaa pasiwaya kwenye sikio kando
Ikiwa una maswali yoyote kuhusu kutumia kifaa chako pasiwaya na kifaa cha matibabu
kilichopachikwa, wasiliana na mtoa huduma wako wa afya.
na kifaa cha matibabu.
• Zima kifaa pasiwaya kama kuna sababu
yoyote ya kushuku kwamba mwingiliano
unafanyika.
• Fuata maagizo ya mtengeneza kifaa cha
matibabu kilichopachikwa.
VIFAA VYA KUSAIDIA KUSIKIA
Onyo: Wakati unatumia vifaa vya sauti, uwezo wako wa kusikiliza sauti za nje unaweza
kuathirika. Usitumie vifaa vya sauti mahali ambapo kinaweza kuhatarisha usalama wako.
Baadhi ya vifaa pasiwaya vinaweza kuingiliana na baadhi ya vifaa vya kusaidia kusikia.
Huenda kifaa chako kikakumbana na virusi na maudhui mengine mabaya. Chukua tahadhari
zifuatazo:
• Kuwa mwangalifu wakati unafungua ujumbe. Huenda zikawa na programu mbaya au
zikaharibu kifaa au kompyuta yako.
• Kuwa mwangalifu wakati unakubali maombi ya muunganisho au unapovinjari intaneti.
Usikubali maombi ya miunganisho ya Bluetooth kutoka vyanzo usivyoviamini.
• Sakinisha kingavirusi na programu nyingine za usalama kwenye kompyuta yoyote
iliyounganishwa.
• Ukifikia vialamisho na viungo vilivyosakinishwa mapema vya tovuti nyingine za intaneti, kuwa
mwangalifu. HMD Global haiidhinishi au kuwajibika kwa tovuti kama hizo.
MAGARI
Huenda mawimbi ya redio yakaathiri vibaya mifumo ya elektroniki iliyowekwa vibaya au
isiyokingwa vizuri katika magari. Kwa maelezo zaidi, wasiliana na mtengeneza gari lako au vifaa
vyake. Watu walioidhinishwa tu ndio wanapaswa kuweka kifaa ndani ya gari. Usakinishaji wenye
kasoro huenda wa hatari na ukabatilisha waranti yako. Hakikisha mara kwa mara kwamba vifaa
vyote visivyotumia waya ndani ya gari vimefungwa vizuri na vinafanya kazi sawasawa. Usihifadhi
au kubeba vifaa vinavyoweza kuchomeka au kulipuka katika eneo sawa kama kifaa, sehemu
zake, au vifaa vya ziada. Usiweke kifaa chako au viboreshaji kwenye eneo ambalo mfuko wa
hewa hutumika.
MAZINGIRA YANAYOWEZA KULIPUKA
Zima kifaa chako katika eneo lolote lenya mazingira yanayoweza kulipika, kama vile karibu na
pampu za mafuta katika vituo vya mafuta. Cheche zinaweza kusababisha mlipuko au moto
unaoweza kuleta majeraha au kifo. Kumbuka vikwazo katika maeneo yenye mafuta; viwanda
vya kemikali; au mahali ambapo shughuli za ulipuaji zinaendelea kufanyika. Maeneo yenye
mazingira yenye uwezekano wa milipuko yanaweza kuwa na alama zisizo dhahiri. Haya kwa
kawaida ni maeneo ambapo unaweza kushauriwa kuzima injini yako, chini ya sitaha kwenye boti,
uhamishaji kemikali au suhula za kuhifadhi, na ambapo hewa ina kemikali au chembechembe
kama vile nafaka, vumbi au poda ya chuma. Wasiliana na watengenezaji wa magari yanayotumia
mafuta aina ya gesi oevu ya petroli iliyoyeyushwa (kama vile propeni au buteni) ikiwa kifaa hiki
kinaweza kutumiwa vizuri katika maeneo yao.
HABARI YA UTOAJI CHETI (SAR)
Kifaa hiki cha mkononi kinatimiza maelekezo yanayohusu ujiwekaji wazi kwa mawimbi ya
redio.
Kifaa chako cha mkononi ni transmita na kipokezi cha redio. Kimeundwa kutozidi kikomo cha
ufichuzi kwa mawimbi ya redio (nyuga za sumaku za masafa ya redio), yanayopendekezwa
na maelekezo ya kimataifa kutoka kwa shirika huru la kisanyansi ICNIRP. Maelekezo haya
yanajumuisha viwango vya tahadhari ya ziada iliyowekwa kuhakikisha usalama wa watu wote,
bila kujali umri wala afya. Maelekezo ya ufichuzi yanategemea Kiwango Maalum cha Ufyonzaji
(SAR), ambacho ni onyesho la nguvu za kiwango cha masafa ya redio (RF) zinazowekwa kichwani
au mwilini wakati kifaa kinapitisha. Kikomo cha ICNIRP SAR kwa vifaa vya mkononi ni 2.0
wati/kilogramu (W/kg) kilichotokana na wastani wa gramu 10 za tishu.
Vipimo vya SAR hutekelezwa na kifaa katika mikao wastani ya matumizi, kwa hivyo kupitisha
kwa kiwango chake cha juu zaidi kilichoidhinishwa, katika bendi zake zote za masafa.
Tafadhali rejelea www.nokia.com/phones/sar for the maximum SAR value of the device.
Kifaa hiki kinatimiza matakwa ya maelekezo ya ujiwekaji wazi wa RF wakati kinatumiwa karibu
na kichwa au kikiwekwa angalau inchi 5/8 (sentimita 1.5) mbali na mwili. Wakati kikasha cha
kubebea, kishikiza kwenye mkanda au aina nyingi ya kishikizi kikitumika kwa matumizi ya
kuvaliwa mwilini, kinatakiwa kisiwe na chuma na kinatakiwa kuweka angalia umbali uliotajwa
hapo juu kutoka kwenye mwili.
Kutuma data au ujumbe, muunganisho salama wa mtandao unahitajika. Utumaji unaweza
kucheleweshwa hadi muunganisho huo upatikane. Fuata maagizo ya umbali wa kutenganisha
hadi utumaji ukamilike.
Wakati wa matumizi ya kawaida, thamani za SAR kwa kawaida huwa chini ya thamani zilizotajwa
hapa juu. Hii ni kwa sababu, kwa malengo ya ubora wa mfumo na kupunguza mwingiliano
kwenye mtandao, nguvu ya kufanya kazi ya kifaa chako cha mkononi hupunguzwa kiotomati
wakati nguvu kamili haihitajiki kwa simu. Nguvu towe inavyoendelea kuwa chini, ndivyo thamani
ya SAR inavyokuwa chini.
Huenda modeli za vifaa zikawa na matoleo tofauti na zaidi ya thamani moja. Mabadiliko ya
vijenzi na muundo yanaweza kufanyika baada ya muda na baadhi ya mabadiliko yanaweza
kuathiri thamani za SAR.
Kwa maelezo zaidi, nenda kwenye www.sar-tick.com. Kumbuka kwamba vifaa vya mkononi
huenda vikapitisha hata kama hupigi simu.
Shirika la Afya Duniani (WHO) limesema kwamba maelezo ya sasa ya kisayansi hayaashirii
hitaji la tahadhari zozote maalum wakati wa kutumia vifaa vya mkononi. Ikiwa unavutiwa
na kupunguza ufichuzi wako, wanapendekeza upunguze matumizi yako au utumie kifaa
kisichotumia mikono ili kuweka kifaa mbali na kichwa na mwili wako. Kwa maelezo zaidi
na ufafanuzi na majadiliano kuhusu ufichuzi wa RF, nenda kwenye tovuti ya WHO kwenye
Unapokuwa ukitumia kifaa hiki, tii sheria zote na heshimu utamaduni wa wenyeji, uhuru binafsi
wa mtu na haki halali za wengine, ikiwemo hakimiliki. Kinga za hakimiliki zinaweza kukuzuia dhidi
ya kunakili, kurekebisha au kuhamisha picha, muziki na maudhui mengine.
Upatikanaji wa bidhaa, vipengele, programu na huduma unaweza kutofautiana kimaeneo.
Kwa maelezo zaidi, wasiliana na mchuuzi au mtoa huduma wako. Kifaa hiki kinaweza kuwa na
bidhaa, teknolojia au programu ambayo inategemea sheria na masharti ya usafirishaji nje ya
nchi kutoka Marekani na nchi nyingine. Uchepushaji kinyume na sheria ni marufuku.
Yaliyomo katika waraka huu yametolewa ”kama yalivyo”. Isipokuwa kama inatakiwa hivyo na
sheria husika, hakuna dhamana za aina yoyote, ama za moja kwa moja au zisizo bayana, pamoja
na, lakini isiyokomea hapo, dhamana zisizo bayana za uuzikaji wa kibiashara na ufaaji kwa
matumizi fulani, zinazotolewa kuhusiana na usahihi, uaminikaji au yaliyomo ndani ya waraka
huu. HMD Global ina haki ya kupitia na kusahihisha waraka huu au kuuondoa wakati wowote bila
kutoa taarifa kwanza.
Kwa kadiri inayohusiwa na sheria husika, hakuna wakati wowote ule HMD Global au wenye leseni
wake watawajibika kwa upotevu wowote wa data au mapato au uharibifu wowote ule, uwe
maalum, wa ajali, unatokana na, au usiokuwa wa moja kwa moja uliosababishwa.
Ni marufuku kutoa upya, kuhamisha au kusambaza sehemu ya yaliyomo au yote katika waraka
huu katika hali yoyote ile bila ya kupewa kwanza idhini ya kuandikwa kutoka kwa HMD Global.
HMD Global inaendesha sera ya kuendelea kubuni. HMD Global ina haki ya kufanya mabadiliko
na kuboresha bidhaa yake yoyote iliyoelezwa katika waraka huu bila kutoa taarifa kwanza.
HMD Global haitoi uhakikisho wowote, waranti au kuwajibika kwa utendakazi, maudhui, au
usaidizi wa mtumiaji wa programu za mhusika mwingine zilizotolewa na kifaa chako. Kwa
kutumia programu, unakubali kwamba programu imetolewa kama ilivyo.
Upakuaji wa ramani, michezo, muziki na video na upakiaji wa picha na video huenda
ukajumuisha upitishaji wa viwango vikubwa vya data. Huenda mtoa huduma wako akatoza kwa
upitishaji data. Upatikanaji wa bidhaa, huduma na vipengele fulani unaweza zikatofautiana
kimaeneo. Tafadhali wasiliana na muuzaji wa eneo lako kwa maelezo zaidi na upatikanaji wa
chaguo za lugha.
Vipengele, utendakazi na ainisho nyingine za bidhaa zinaweza kutegemea mtandao na
hutegemea masharti, sheria, na gharama za ziada.
Ainisho, vipengele na maelezo mengine yote ya bidhaa yaliyotolewa yanaweza kubadilika bila
ilani.
Sera ya Faragha ya HMD Global, inapatikana kwenye http://www.nokia.com/phones/privacy,
hutumika kwa matumizi yako ya kifaa.
HMD Global Oy ndio ina leseni ya kipekee ya chapa ya Nokia ya simu na kompyuta kibao. Nokia
ni alama ya biashara iliyosajiliwa ya Nokia Corporation.
Alama ya neno na nembo za Bluetooth zinamilikiwa na Bluetooth SIG, Inc. na matumizi yoyote
ya alama hizo na HMD Global yako chini ya leseni.
Bidhaa hii inajumuisha programu huria. Kwa hakimiliki husika na ilani, vibali, na ukubalifu
mwingine, chagua *#6774# kwenye skrini ya mwanzo.