Muhimu: Kwa maelezo muhimu kuhusu matumizi salama ya kifaa na betri yako, soma maelezo
ya ”Kwa usalama wako” na ”Usalama wa Bidhaa” katika mwongozo uliochapishwa wa mtumiaji,
au kwenye www.nokia.com/support kabla utumie kifaa. Ili kujua jinsi ya kuanza kutumia kifaa
chako kipya, soma mwongozo uliochapishwa wa mtumiaji.
Sasisha simu yako na ukubali visasisho vinavyopatikana vya programu ili upate vipengee vipya
na vilivyoboreshwa vya simu yako. Kusasisha programu kunaweza pia kuboresha utendakazi wa
simu yako.
VITUFE NA SEHEMU
Simu yako
Mwongozo huu wa mtumiaji hutumika kwa modeli zifuatazo: TA-1479, TA-1490, TA-1481, TA-
11. Kitufe cha Nishati/Kufunga, Sensa ya
alama ya kidole
Baadhi ya vifaa vya ziada vilivyotajwa katika mwongozo huu wa mtumiaji, kama vile chaja, kifaa
cha kichwani, au kebo ya data, huenda vikauzwa kando.
Sehemu na viunganishaji, hali ya sumaku
Usiunganishe kwenye bidhaa ambazo zinaunda ishara ya kutoa, kwa kuwa hii inaweza kuharibu
kifaa. Usiunganishe chanzo chochote cha stima kwenye kiunganisha cha sauti. Ukiunganisha
kifaa chochote cha nje au vifaa vyovyote vya sauti kando na vile vilivyoidhinishwa kutumiwa na
kifaa hiki, Kiunganishi cha sauti, kuwa makini sana na viwango vya sauti.
Sehemu nyingine za kifaa hiki zina sumaku. Vitu vya chuma vinaweza kuvutwa na kifaa. Usiweke
kadi za mkopo au kadi nyingine zenye mkanda wa sumaku karibu na kifaa kwa kipindi cha muda
mrefu, kwa kuwa kadi hizo zinaweza kuharibika.
12. Kiunganisha USB
INGIZA SIM NA KADI ZA KUMBUKUMBU
Ingiza kadi
1. Fungua trei ya SIM kadi: sukuma pini ya kufungua trei ndani ya shimo la trei na uondoe trei.
2. Ikiwa una simu ya SIM moja, weka kadi ya nano-SIM kwenye kipenyo 1 na kadi ya
kumbukumbu kwenye kipenyo 2 kwenye trei eneo la mguso likiangalia chini. Ikiwa una
simu ya SIM mbili, weka SIM kadi ya nano kwenye kipenyo 1 na aidha SIM ya pili au kadi ya
kumbukumbu kwenye kipenyo 2 kwenye trei eneo la mguso likiangalia chini.
Ikiwa una eSIM kadi badala ya SIM kadi halisi, washa simu yako na ufuate maagizo kwenye simu.
Kuweza kuamilisha eSIM yako, unahitaji muunganisho wa Wi-Fi. Kumbuka kwamba ikiwa una
simu ya SIM-moja, unaweza kuwa na SIM kadi moja tu, ya halisi au eSIM, inayotumika kwa wakati
mmmoja. Kumbuka kwamba ikiwa una simu ya SIM-mbili, unaweza kuwa na SIM kadi mbili halisi
au SIM halisi na eSIM inayotumika kwa wakati mmmoja. Kwa maelezo zaidi kuhusu eSIM kadi,
wasiliana na mtoa huduma wako wa mtandao.
Ikiwa una eSIM kadi
Ikiwa una eSIM kadi badala ya SIM kadi halisi, washa simu yako na ufuate maagizo kwenye simu.
Kuweza kuamilisha eSIM yako, unahitaji muunganisho wa Wi-Fi. Ili kununua eSIM kadi, wasiliana
na mtoa huduma wako wa mtandao. Kumbuka kwamba ikiwa una simu ya SIM-moja, unaweza
kuwa na SIM kadi moja tu, ya halisi au eSIM, inayotumika kwa wakati mmmoja. Kumbuka
kwamba ikiwa una simu ya SIM-mbili, unaweza kuwa na SIM kadi mbili halisi au SIM halisi na
eSIM inayotumika kwa wakati mmmoja. Kwa maelezo zaidi kuhusu eSIM kadi, wasiliana na mtoa
huduma wako wa mtandao.
Kidokezo: Ili kujua ikiwa simu yako inaweza kutumia SIM kadi 2, angalia lebo kwenye sanduku
la mauzo. Ikiwa kuna misimbo 2 ya IMEI kwenye lebo, una simu yenye SIM mbili.
Muhimu: Usiondoe kadi ya kumbukumbu wakati programu inaitumia. Kufanya hivyo kunaweza
kuharibu kadi ya kumbukumbu na kuharibu data iliyohifadhiwa kwenye kadi.
Kidokezo: Tumia kadi ya kumbukumbu ya microSD yenye kasi, na ya hadi TB 1 kutoka kwa
mtengenezaji anayefahamika.
CHAJI SIMU YAKO
Chaji betri
1. Chomeka chaja inayotangamana kwenye soketi ya ukuta.
2. Unganisha kebo kwenye simu yako.
Simu yako inakubali kebo ya USB ya C. Pia unaweza kuchaji simu yako kutoka kwenye kompyuta
kwa kutumia kebo ya USB, lakini inaweza kuchukua muda mrefu zaidi.
Kama betri imeisha moto kabisa, huenda ikachukua dakika kadhaa kabla ya kiashiria chaji
kuonyeshwa.
WASHA NA USANIDI SIMU YAKO
Washa simu yako
Wakati unapowasha simu yako kwa mara ya kwanza, simu yako hukuelekeza usanidi
miunganisho ya mtandao na mipangilio ya simu yako.
1. Bonyeza na ushikilie kitufe cha nishati.
2. Chagua lugha na eneo lako.
3. Fuata maagizo yaliyoonyeshwa kwenye simu yako.
Hamisha data kutoka kwenye simu yako ya awali
Huwezi kuhamisha data kutoka kwenye simu yako ya zamani hadi kwenye simu yako mpya kwa
kutumia akaunti ya Google
Ili kuhifadhi nakala ya data kwenye simu yako ya zamani kwenye akaunti yako ya Google, rejelea
mwongozo wa mtumiaji wa simu yako ya zamani.
Rejesha mipangilio ya programu kutoka kwenye simu yako ya awali ya Android™
Ikiwa simu yako ya awali ilikuwa ya Android, na ulikuwa umeiweka kuhifadhi nakala ya
data kwenye akaunti yako ya Google, unaweza kurejesha mipangilio ya programu yako na
manenosiri.
1. Gusa Mipangilio > Nenosiri na akaunti > Ongeza akaunti > Google .
2. Chagua ni data gani unayotaka irejeshwe kwenye simu yako mpya. Usawazishaji huanza
kiotomatiki punde simu yako inapounganishwa kwenye intaneti.
Zima simu yako
Ili kuzima simu yako, bonyeza kitufe cha nishati na kitufe cha kuongeza sauti kwa wakati
mmoja, na uchague Zima nishati .
Kidokezo: Ikiwa unataka kuzima simu yako kwa kubonyeza na kushikilia kitufe cha nishati,
gusa Mipangilio > Mfumo > Ishara > Bonyeza na ushikilie kitufe cha nishati na uzime
Weka vidole 2 kwenye kipengee, kama vile ramani, picha, au ukurasa wavuti, na utelezeshe
vidole vako vikiwa kando au pamoja.
Funga mwelekeo wa skrini
Skrini huzunguka kiotomatiki wakati unapindua simu kwa digrii 90.
Kufunga skrini katika hali ya wima, telezesha chini kutoka upande wa juu wa skrini, na uguse
Zungusha kiotomatiki > Zima .
Rambaza kwa kutumia ishara
Kuwasha kwa kutumia urambazaji wa ishara, gusa Mipangilio > Mfumo > Ishara >
Urambazaji wa mfumo > Urambazaji wa ishara .
• Ili kuona programu zako zote, kwenye skrini ya mwanzo, telezesha juu kwenye skrini.
• Ili kwenda kwenye skrini ya mwanzo, telezesha juu kutoka chini ya skrini. Programu
uliyokuwa ukitumia hubakia imefunguliwa chinichini.
• Kuona programu gani umefungua, telezesha juu kutoka chini ya skrini bila kutoa kidole
chako hadi uone programu, kisha uondoe kidole chako. Ili kubadilisha kwa programu
nyingine iliyofunguliwa, gusa programu. Ili kufunga programu zote zilizofunguliwa, telezesha
kulia kupitia programu zote na uguse FUTA ZOTE .
• Ili urudi kwenye skrini ya awali ambayo ulikuwa unatumia, telezesha kutoka upande wa kulia
au kushoto ya skrini. simu yako hukumbuka programu na tovuti zote ulizotembelea tangu
wakati wa mwisho skrini yako ilipofungwa.
Kuwasha vitufe vya urambazaji, gusa Mipangilio > Mfumo > Ishara > Urambazaji wa mfumo
> Urambazaji wa vitufe 3 .
• Ili kuona programu zako zote, kwenye skrini ya mwanzo, telezesha juu kuanzia chini ya
skrini.
• Ili kwenda kwenye skrini ya mwanzo, gusa . Programu uliyokuwa ukitumia hubakia
imefunguliwa chinichini.
• Ili kuona ni programu gani ulizofungua, gusa . Ili kubadilisha kwa programu nyingine
iliyofunguliwa, telezesha kulia na uguse programu. Ili kufunga programu zote
zilizofunguliwa, telezesha kulia kupitia programu zote na uguse FUTA ZOTE .
• Ili kurejesha kwenye skrini ya awali uliyokuwa, gusa . simu yako hukumbuka programu na
tovuti zote ulizotembelea tangu wakati wa mwisho skrini yako ilipofungwa.
TUMIA ESIM YAKO
Wezesha eSIM yako
Ikiwa hukuwasha eSIM kadi yako ulipowasha simu yako kwa mara ya kwanza, unaweza
kuiwasha katika mipangilio. Ikiwa huna SIM kadi halisi iliyowekwa kwenye simu yako, unahitaji
muunganisho wa Wi-Fi ili kuweza kuwasha eSIM yako: gusa Mipangilio > Mtandao na intaneti ,
na uwashe Wi-Fi .
1. Gusa Mipangilio > Mtandao na intaneti >
SIM .
2. Ikiwa huna SIM kadi halisi
iliyowekwa kwenye simu yako, gusa
Pakua eSIM badala yake? . Ikiwa tayari
una SIM kadi halisi iliyowekwa, gusa
Ongeza eSIM .
3. Ikiwa una msimbo wa QR kutoka kwa
mtoa huduma wako wa mtandao,
ichanganue kwa kutumia simu
yako au gusa Unahitaji msaada? >
iweke wewe mwenyewe , na uweke
msimbo ulioupokea kutoka kwa mtoa
huduma wako wa mtandao.
4. Gusa Endelea > Pakua , na usubiri hadi
eSIM ipakuliwe kwenye simu yako.
5. Gusa Mipangilio na eSIM, na uwashe
Tumia eSIM .
Unaweza kuwa na hadi eSIM kadi 10 kwenye simu hii, kulingana na ukubwa wa eSIM zako. Ikiwa
huna nafasi ya kutosha ya eSIM zako, uondoa eSIM katika Mipangilio .
Badilisha kati ya eSIM
Ikiwa una eSIM kadi kadhaa na unataka kubadilisha utumie eSIM nyingine, gusa Mipangilio >
Mtandao na intaneti > SIM , gusa eSIM unayotaka kutumia, na uwashe Tumia eSIM .
2. Simu hutenganishwa kwenye mtandao wa eSIM. Gusa Sawa ili kuendelea.
3. Mara tu simu ikisoma SIM kadi, gusa SIM kadi na uwashe Tumia SIM .
Ondoa eSIM kutoka kwenye simu yako
Ili uondoe eSIM kadi kwenye simu yako, gusa Mipangilio > Mtandao na intaneti > SIM , gusa
eSIM unayotaka kuondoa na uguse Futa eSIM . Hata hivyo, kumbuka, kwamba hii haisitishi
usajili wako kutoka kwa mtoa huduma wako wa mtandao. Ikiwa unataka kutumia baadaye eSIM
iliyondolewa kwenye simu yako, wasiliana na mtoa huduma wako wa mtandao.