Muhimu: Kwa maelezo muhimu kuhusu matumizi salama ya kifaa na betri yako, soma maelezo
ya ”Kwa usalama wako” na ”Usalama wa Bidhaa” katika mwongozo uliochapishwa wa mtumiaji,
au kwenye www.nokia.com/support kabla utumie kifaa. Ili kujua jinsi ya kuanza kutumia kifaa
chako kipya, soma mwongozo uliochapishwa wa mtumiaji.
Sasisha simu yako na ukubali visasisho vinavyopatikana vya programu ili upate vipengee vipya
na vilivyoboreshwa vya simu yako. Kusasisha programu kunaweza pia kuboresha utendakazi wa
simu yako.
VITUFE NA SEHEMU
Chunguza vitufe na sehemu kwenye simu yako mpya.
Simu yako
Mwongozo huu wa mtumiaji hutumika kwa modeli zifuatazo: TA-1157, TA-1150, TA-1133, TA1149, na TA-1152.
6. Kisaidizi cha Google/Kitufe cha utafutaji
wa Google*
7. Kamera ya mbele
8. Kifaa cha sikioni
9. Vitufe vya sauti
Baadhi ya vifaa vya ziada vilivyotajwa katika mwongozo huu wa mtumiaji, kama vile chaja, kifaa
cha kichwa, au kebo ya data, huenda vikauzwa kando.
*Kisaidizi cha Google hupatikana katika masoko na lugha zilizoteuliwa. Ambapo hakipatikani,
Kisaidizi cha Google hubadilishwa kwa Utafutaji wa Google.
Sehemu na viunganishaji, hali ya sumaku
Usiunganishe kwenye bidhaa ambazo zinaunda ishara ya kutoa, kwa kuwa hii inaweza kuharibu
kifaa. Usiunganishe chanzo chochote cha stima kwenye kiunganisha cha sauti. Ukiunganisha
kifaa chochote cha nje au vifaa vyovyote vya sauti kando na vile vilivyoidhinishwa kutumiwa na
kifaa hiki, Kiunganishi cha sauti, kuwa makini sana na viwango vya sauti.
10. Kitufe cha Nishati/Kufunga
11. Kiunganisha USB
12. Maikrofoni
13. Kipaza sauti
Sehemu nyingine za kifaa hiki zina sumaku. Vitu vya chuma vinaweza kuvutwa na kifaa. Usiweke
kadi za mkopo au kadi nyingine zenye mkanda wa sumaku karibu na kifaa kwa kipindi cha muda
mrefu, kwa kuwa kadi hizo zinaweza kuharibika.
1. Fungua trei ya SIM na kadi ya kumbukumbu: sukuma pini ya kufungua trei ndani ya shimo la
trei na uondoe trei.
2. Weka nano-SIM kwenye kipenyo cha 1 kwenye trei na eneo la mguso likiangalia chini. Ikiwa
una SIM ya pili, ingiza kwenye kipenyo cha 2.
3. Weka kadi ya kumbukumbu kwenye kipenyo cha kadi ya kumbukumbu.
4. Telezesha trei ndani.
Tumia kadi halisi ya nano-SIM tu. Matumizi ya SIM kadi zisizotangamana huenda yakaharibu
kadi au kifaa, na huenda yakaharibu data iliyohifadhiwa kwenye kadi.
Tumia tu kadi za kumbukumbu zinazotangamana zilizoidhinishwa kutumiwa na kifaa hiki. Kadi
zisizotangamana zinaweza kuharibu kadi na kifaa na kuharibu data iliyohifadhiwa kwenye kadi.
Muhimu: Usiondoe kadi ya kumbukumbu wakati programu inaitumia. Kufanya hivyo kunaweza
kuharibu kadi ya kumbukumbu na kuharibu data iliyohifadhiwa kwenye kadi.
CHAJI SIMU YAKO
Chaji betri
1. Chomeka chaja inayotangamana kwenye soketi ya ukuta.
2. Unganisha kebo kwenye simu yako.
Simu yako inakubali kebo ya USB ya micro-B. Pia unaweza kuchaji simu yako kutoka kwenye
kompyuta kwa kutumia kebo ya USB, lakini inaweza kuchukua muda mrefu zaidi.
Kama betri imeisha moto kabisa, huenda ikachukua dakika kadhaa kabla ya kiashiria chaji
kuonyeshwa.
WASHA NA USANIDI SIMU YAKO
Wakati unapowasha simu yako kwa mara ya kwanza, simu yako hukuelekeza usanidi
miunganisho ya mtandao na mipangilio ya simu yako.
2. Chagua ni data gani unayotaka irejeshwe kwenye simu yako mpya. Usawazishaji huanza
kiotomatiki punde simu yako inapounganishwa kwenye intaneti.
Rejesha mipangilio ya programu kutoka kwenye simu yako ya awali ya Android™
Ikiwa simu yako ya awali ilikuwa ya Android, na uhifadhi nakala ya akaunti ya Google kwayo,
unaweza kurejesha mipangilio ya programu yako na manenosiri ya Wi-Fi.
1. Gusa Mipangilio > Mfumo > Mipangilio ya kina > Hifadhi nakala rudufu .
2. Badilisha Hifadhi nakala kwenye Google Drive kwa Washa .
MIPANGILIO YA SIM MBILI
Ikiwa una toleo la SIM mbili, unaweza kuwa na SIM 2 kwenye simu yako, kwa mfano, moja ya kazi
yako na nyingine ya matumizi yako ya kibinafsi.
Chagua ni SIM gani ya kutumia
Kwa mfano, wakati unapiga simu, unaweza kuchagua ni SIM gani ya kutumia kwa kugusa kitufe
kinacholingana cha SIM 1 au SIM 2 baada ya kupiga nambari hiyo.
Simu yako huonyesha hali ya mtandao ya SIM zako kitofauti. SIM kadi zote zinapatikana kwa
wakati mmoja wakati kifaa hakitumiki, lakini wakai SIM kadi moja inatumika, kwa mfano, wakati
wa kupiga simu, ile nyingine inawezakosa kupatikana.
Skrini huzunguka kiotomatiki wakati unapindua simu kwa digrii 90.
Kufunga skrini katika hali ya wima, telezesha chini kutoka upande wa juu wa skrini, na uguse
Zungusha kiotomatiki .
Tumia vitufe vya urambazaji
Ili kuona ni programu gani ulizofungua, pitisha juu kwenye kitufe cha mwanzo .
Ili kubadilisha kwa programu nyingine, pitisha kulia.
Ili kufunga programu, ipitishe juu.
Ili kurejesha kwenye skrini ya awali uliyokuwa, gusa kitufe cha nyuma . simu yako hukumbuka
programu na tovuti zote ulizotembelea tangu wakati wa mwisho skrini yako ilipofungwa.
Ili kwenda kwenye skrini ya mwanzo, gusa kitufe cha mwanzo . Programu uliyokuwa ukitumia
hubakia imefunguliwa chinichini.
Fungua programu mbili kwa wakati mmoja
1. Ili kuabiri kwa urahisi kati ya programu, pitisha juu kwenye kitufe cha mwanzo .
2. Gusa ikoni ya programu juu ya programu na uguse ikoni ya .
3. Gusa programu nyingine kwenye orodha ya programu ili ugawanye skrini kati ya programu
mbili.
Ili kurudi kwenye mwonekano wa kawaida, gusa programu na upitishe juu.
Kwenye skrini ya mwanzo, gusa ikoni ya programu ili kuifungua. Ili kufungua mojawapo ya
programu zinazoendeshwa kichini chini, telezesha kitufe cha nyumbani kisha telezesha kulia
na uchague programu.
Fungua programu
Telezesha juu kitufe cha nyumbani na utelezeshe juu programu unayotaka kufunga.
Tafuta programu zako
Telezesha juu kitufe cha nyumbani na utelezeshe juu tena ili kuona programu zako zote.
Funga programu zote zinazoendeshwa
Telezesha juu kitufe cha nyumbani , telezesha kulia kwenye programu zote, na uguse
FUTA ZOTE .
BINAFSISHA SIMU YAKO
Jifunze jinsi ya kubinafsisha skrini ya mwanzo na jinsi ya kubadilisha mlio wa simu.
Badilisha mandhari yako
Gusa Mipangilio > Skrini > Mandhari .
Badilisha mlio wa simu yako
Gusa Mipangilio > Sauti > Mlio wa simu wa SIM1 or Mlio wa simu wa SIM2 .
Badilisha sauti ya taarifa ya ujumbe wako
Gusa Mipangilio > Sauti > Mipangilio ya kina > Sauti chaguo-msingi ya arifa .
Pata kujua kinachoendelea kwenye simu yako kwa kutumia arifa.
Tumia paneli ya taarifa
Unapopokea arifa mpya, kama vile ujumbe au simu zisizojibiwa, aikoni ya kiashiriaji huonekana
kwenye upau wa hali juu ya skrini. Ili kuona maelezo zaidi kuhusu arifa, kokota chini upau wa
hali. Ili kufunga mwonekano, pitisha juu kwenye skrini.
Ili kufungua paneli ya arifa, kokota upau wa hali chini. Ili kufunga paneli ya arifa, pitisha juu
kwenye skrini.
Ili kubadilisha mipangilio ya taarifa ya programu, gusa Mipangilio > Programu na arifa > na
uguse jina la programu ili ufungue mipangilio ya programu. Gusa Arifa . Unaweza kuzima au
kuwasha arifa kwa kila programu kivyake.
Kidokezo: Ili kuona nukta za arifa, gusa Mipangilio > Programu na arifa > Arifa na
ubadilishe Ruhusu nukta za arifa kwa washa. Nukta ndogo itaonekana kwenye ikoni ya
programu, ikiwa una arifa, lakini bado hatujaishughulikia. Gusa na ushikilie ikoni ili kuona
chaguo zinazopatikana, Unaweza kugusa arifa ili kuifungua, au telezesha ili kupuuza.
Tumia ikoni za mpangilio wa haraka
Ili kuamilisha vipengele, gusa ikoni za mipangilio ya haraka kwenye paneli ya arifa. Ili kuona ikoni
zaidi, kokoa menyu chini.
Ili kupanga upya ikoni, gusa , gusa na ushikilie ikoni, na uikokote kwenye eneo lingine.
Ikiwa una tatizo la kusikia simu yako ikiita katika mazingira yenye kelele, au simu ina sauti ya
juu, unaweza kubadilisha sauti kama upendavyo kwa kutumia vitufe vya sauti upande wa simu
yako.
Usiunganishe kwenye bidhaa ambazo zinaunda ishara ya kutoa, kwa kuwa hii inaweza kuharibu
kifaa. Usiunganishe chanzo chochote cha stima kwenye kiunganisha cha sauti. Ukiunganisha
kifaa chochote cha nje au vifaa vyovyote vya sauti kando na vile vilivyoidhinishwa kutumiwa na
kifaa hiki, Kiunganishi cha sauti, kuwa makini sana na viwango vya sauti.
Badilisha mipangilio ya sauti
Bonyeza kitufe cha sauti upande wa simu yako ili uone upau wa hali ya sauti, gusa , na
ukokote vitelezi kwenye pau za sauti upande wa kushoto au kulia.
Weka simu kimya
Ili kuweka simu kimya, bonyeza kitufe cha sauti, gusa ili kuweka simu yako iteteme pekee na
uguse ili kuiweka kimya.
KISAIDIZI CHA GOOGLE
Kisaidizi cha Google hupatikana katika masoko na lugha zilizoteuliwa pekee. Ambapo
hakipatikani, Kisaidizi cha Google hubadilishwa kwa Utafutaji wa Google. Kisaidizi cha Google
kinaweza kukusaidia kwa mfano, kutafuta maelezo mtandaoni, kutafsiri maneno na sentensi,
kuandika vidokezo na uteuzi wa kalenda. Unaweza kutumia Kisaidizi cha Google hata wakati
simu yako imefungwa. Hata hivyo, Kisaidizi cha Google hukuomba ufungue simu yako kabla ya
kufikia data yako ya kibinafsi.
Tumia kitufe cha Kisaidizi cha Google
Ili kufikia huduma za Kisaidizi cha Google, tumia kitufe cha Kisaidizi cha Google upande wa simu
yako:
• Bonyeza kitufe mara moja ili kuanzisha Kisaidizi cha Google. Unapobonyeza kitufe mara ya
kwanza, unaulizwa kuingia kwa kutumia akaunti yako ya Google au kuunda akaunti mpya.
• Bonyeza kitufe mara mbili ili kuona muhtasari wa siku yako, kupata mapendekezo na
maelezo yaliyobinafsishwa
• Bonyeza na ushikilie kitufe mara moja ili kuzungumza na Kisaidizi cha Google. Uliza swali
lako na uachilie kitufe. Utaona jibu la Kisaidizi cha Google kwenye skrini ya simu yako.
Ikiwa nchi au eneo lako halikubali Kisaidizi cha Google, bado unaweza kutumia kitufe cha
Kisaidizi cha Google:
• Bonyeza kitufe mara moja ili kufungua utafutaji wa Google
• Bonyeza kitufe mara mbili ili kuanzisha picha ya Google inayoonyesha ajenda yako ya leo
• Bonyeza na ushikilie kitufe ili kutumia utafutaji wa sauti ya Google. Uliza swali lako na
uachilie kitufe. Utaona jibu la Google kwenye skrini ya simu yako.
Zima kitufe cha Kisaidizi cha Google
Kuzima kitufe cha Kisaidizi cha Google, gusa Mipangilio > Mfumo > Ishara >
Kitufe cha Kisaidizi cha Google , na uzime Kitufe cha Kisaidizi cha Google .
MAISHA YA BETRI
Pata mengi kutoka kwa simu yako ukipata maisha ya betri unayotaka. Kuna hatua unazoweza
kuchukua kuokoa nishati kwenye simu yako.
Ongeza maisha ya betri
Kuokoa nishati:
• Daima chaji betri kikamilifu.
• Kunyamazisha sauti zisizohitajika, kama
vile sauti za kugusa. Gusa Mipangilio
> Sauti > Mipangilio ya kina , na katika
sehemu ya Sauti na mitetemo mingine ,
chagua ni sauti gani za kuweka.
• Tumia vifaa vya masikio, badala ya kipaza
sauti.
• Weka skrini ya simu kuzima baada ya
muda mfupi. Gusa Mipangilio > Skrini
> Mipangilio ya kina > Lala na uchague
muda.
• Gusa Mipangilio > Onyesho >
Hali ya mwangaza . Ili kurekebisha
mwangaza, kokota kitelezi cha hali
ya mwangaza. Hakikisha kwamba
Mwangaza uliorekebishwa umezimwa.
• Komesha programu kufanya kazi
kichinichini: telezesha juu kitufe cha
nyumbani na utelezeshe juu programu
unayotaka kufunga.
• Wezesha betri inayofaa. Zuia betri kwa
programu ambazo hutumii mara kwa
mara. Huenda arifa zikacheleweshwa kwa
programu hizi. Gusa Mipangilio > Betri >
• Tumia huduma za eneo kwa uangalifu:
zima huduma za eneo wakati hauzihitaji.
Gusa Mipangilio > Usalama na eneo >
Eneo , na ulemaze Tumia eneo .
• Tumia miunganisho ya mtandao kwa
uangalifu: washa Bluetooth wakati
inahitajika tu. Tumia muunganisho wa WiFi kuunganisha kwenye intaneti, badala ya
munganisho wa data ya simu.
• Komesha simu yako kuchanganua
mitandao ya pasiwaya inayopatikana.
Gusa Mipangilio > Mtandao na intaneti
> Wi-Fi , na ulemaze Tumia Wi-Fi .
• Ikiwa unasikiliza muziki au vinginevyo
unatumia simu yako, lakini hutaki kupiga
au kupokea simu, washa hali ya ndege.
Gusa Mipangilio > Mtandao na intaneti
> Mipangilio ya kina > Hali ya ndege . Hali
ya ndege hufunga miunganisho kwenye
mitandao ya simu za mkononi na huzima
vipengele pasiwaya vya kifaa chako.
ANDIKA MAANDISHI
Jifunze jinsi ya kuandika maandishi kwa haraka na vizuri kwa kutumia kibodi ya simu yako.
Tumia kibodi kwenye skrini
Kuandika kwa kutumia kibodi kwenye skrini ni rahisi. Unaweza kutumia kibodi ukiwa umeshikilia
simu yako katika hali wima au mlalo. Mpangilio wa kibodi unaweza kutofautiana katika
programu na lugha tofauti.
Ili kufungua kibodi kwenye skrini, gusa kisanduku cha maandishi.
Badilisha kati ya vibambo vikubwa na vidogo
Gusa kitufe cha shift. Ili kuwasha hali ya caps lock, gusa kitufe mara mbili. Ili kurejea hali ya
kawaida, gusa tena kitufe cha shift.
Charaza namba au kibambo maalum
Gusa nambari na Kitufe cha alama. Baadhi vitufe vya vibambo maalum huleta alama zaidi. Ili
kuona alama zaidi, gusa na ushikilie alama au kibambo maalum.
Ingiza emoji
Gusa kitufe cha emoji, na uchague emoji.
Nakili au bandika maandishi
Gusa na ushikilie neno, kokota viweka alama kabla na baada ya neno ili kuangazia sehemu
unayotaka kunakili na uguse Nakili . Ili kubandika maandishi, gusa ni wapi unataka kubandika
maandishi na uchague Bandika .