Muhimu: Kwa maelezo muhimu kuhusu matumizi salama ya kifaa na betri yako, soma maelezo
ya ”Kwa usalama wako” na ”Usalama wa Bidhaa” katika mwongozo uliochapishwa wa mtumiaji,
au kwenye www.nokia.com/support kabla utumie kifaa. Ili kujua jinsi ya kuanza kutumia kifaa
chako kipya, soma mwongozo uliochapishwa wa mtumiaji.
Sasisha simu yako na ukubali visasisho vinavyopatikana vya programu ili upate vipengee vipya
na vilivyoboreshwa vya simu yako. Kusasisha programu kunaweza pia kuboresha utendakazi wa
simu yako.
VITUFE NA SEHEMU
Simu yako
Mwongozo huu wa mtumiaji hutumika kwa modeli zifuatazo: TA-1361, TA-1358, TA-1370, TA1367, TA-1390.
6. Kisaidizi cha Google/Kitufe cha Utafutaji
wa Google*
7. Kamera ya mbele
8. Maikrofoni
9. Kiunganisha kifaa cha kichwani
Nokia G50 Mwongozo wa mtumiaji
10. Kifaa cha sikioni
12. Kitufe cha Nishati/Kufunga/Sensa ya
alama ya kidole
11. Vitufe vya sauti
13. Kiunganisha USB
Baadhi ya vifaa vya ziada vilivyotajwa katika mwongozo huu wa mtumiaji, kama vile chaja, kifaa
cha kichwani, au kebo ya data, huenda vikauzwa kando.
*Kisaidizi cha Google hakipatikani katika lugha na nchi zingine. Ambapo hakipatikani,
Kisaidizi cha Google hubadilishwa kwa Utafutaji wa Google. Angalia upatikanaji katika
https://support.google.com/assistant.
Sehemu na viunganishaji, hali ya sumaku
Usiunganishe kwenye bidhaa ambazo zinaunda ishara ya kutoa, kwa kuwa hii inaweza kuharibu
kifaa. Usiunganishe chanzo chochote cha stima kwenye kiunganisha cha sauti. Ukiunganisha
kifaa chochote cha nje au vifaa vyovyote vya sauti kando na vile vilivyoidhinishwa kutumiwa na
kifaa hiki, Kiunganishi cha sauti, kuwa makini sana na viwango vya sauti.
Sehemu nyingine za kifaa hiki zina sumaku. Vitu vya chuma vinaweza kuvutwa na kifaa. Usiweke
kadi za mkopo au kadi nyingine zenye mkanda wa sumaku karibu na kifaa kwa kipindi cha muda
mrefu, kwa kuwa kadi hizo zinaweza kuharibika.
1. Fungua trei ya SIM kadi: sukuma pini ya kufungua trei ndani ya shimo la trei na uondoe trei.
2. Ikiwa una simu ya SIM moja, weka kadi ya nano-SIM kwenye kipenyo 1 na kadi ya
kumbukumbu kwenye kipenyo 2 kwenye trei eneo la mguso likiangalia chini. Ikiwa una
simu ya SIM mbili, weka SIM kadi ya nano kwenye kipenyo 1 na aidha SIM ya pili au kadi ya
kumbukumbu kwenye kipenyo 2 kwenye trei eneo la mguso likiangalia chini.
3. Telezesha trei ndani.
Kidokezo: Ili kujua ikiwa simu yako inaweza kutumia SIM kadi 2, angalia lebo kwenye sanduku
la mauzo. Ikiwa kuna misimbo 2 ya IMEI kwenye lebo, una simu yenye SIM mbili.
Muhimu: Usiondoe kadi ya kumbukumbu wakati programu inaitumia. Kufanya hivyo kunaweza
kuharibu kadi ya kumbukumbu na kuharibu data iliyohifadhiwa kwenye kadi.
Kidokezo: Tumia kadi ya kumbukumbu ya microSD yenye kasi, na ya hadi GB 512 kutoka kwa
mtengenezaji anayefahamika.
1. Chomeka chaja inayotangamana kwenye soketi ya ukuta.
2. Unganisha kebo kwenye simu yako.
Simu yako inakubali kebo ya USB ya C. Pia unaweza kuchaji simu yako kutoka kwenye kompyuta
kwa kutumia kebo ya USB, lakini inaweza kuchukua muda mrefu zaidi.
Kama betri imeisha moto kabisa, huenda ikachukua dakika kadhaa kabla ya kiashiria chaji
kuonyeshwa.
WASHA NA USANIDI SIMU YAKO
Wakati unapowasha simu yako kwa mara ya kwanza, simu yako hukuelekeza usanidi
miunganisho ya mtandao na mipangilio ya simu yako.
Washa simu yako
1. Kuwasha simu yako, bonyeza na ushikilie kitufe cha nishati hadi simu iteteme.
2. Wakati simu imewashwa, chagua lugha na eneo lako.
3. Fuata maagizo yaliyoonyeshwa kwenye simu yako.
Hamisha data kutoka kwenye simu yako ya awali
Huwezi kuhamisha data kutoka kwenye simu yako ya zamani hadi kwenye simu yako mpya kwa
kutumia akaunti ya Google
Ili kuhifadhi nakala ya data kwenye simu yako ya zamani kwenye akaunti yako ya Google, rejelea
mwongozo wa mtumiaji wa simu yako ya zamani.
Rejesha mipangilio ya programu kutoka kwenye simu yako ya awali ya Android™
Ikiwa simu yako ya awali ilikuwa ya Android, na uhifadhi nakala ya akaunti ya Google kwayo,
unaweza kurejesha mipangilio ya programu yako na manenosiri ya Wi-Fi.
1. Gusa Mipangilio > Mfumo > Hifadhi nakala rudufu .
2. Badilisha Hifadhi nakala kwenye Google Drive kwa Washa .
MIPANGILIO YA SIM MBILI
Ikiwa una simu ya SIM mbili, unaweza kuwa na SIM 2 kwenye simu yako, kwa mfano, moja ya kazi
yako na nyingine ya matumizi yako ya kibinafsi.
Chagua ni SIM gani ya kutumia
Kwa mfano, wakati unapiga simu, unaweza kuchagua ni SIM gani ya kutumia kwa kugusa kitufe
kinacholingana cha SIM 1 au SIM 2 baada ya kupiga nambari hiyo.
Simu yako huonyesha hali ya mtandao ya SIM zako kitofauti. SIM kadi zote zinapatikana kwa
wakati mmoja wakati kifaa hakitumiki, lakini wakai SIM kadi moja inatumika, kwa mfano, wakati
wa kupiga simu, ile nyingine inawezakosa kupatikana.
Dhibiti SIM zako
Hutaki kazi iingiliane na muda wako huru? Au una muunganisho wa bei nafuu wa data kwenye
SIM moja? Unaweza kuamua ni SIM gani unayotaka kutumia.
Gusa Mipangilio > Mtandao na intaneti > Mtandao wa simu , na uguse SIM kadi.
Badili jina la SIM kadi
Gusa SIM unayotaka kubadilisha jina, na uandike jina unalotaka.
Chagua ni SIM gani ya kutumia kwa simu au muunganisho wa data
Chini ya SIM unayopendelea ya , gusa mpangilio unaotaka kubadilisha na uchague SIM.
Gusa Mipangilio > Skrini > Mipangilio ya Kina > Mandhari .
Badilisha toni ya mlio wa simu yako
Gusa Mipangilio > Sauti > Toni ya mlio wa Simu (SIM1) au Mipangilio ya Kina >
Toni ya mlio wa Simu (SIM2) , na uchague toni.
Badilisha sauti ya taarifa ya ujumbe wako
Gusa Mipangilio > Sauti > Mipangilio ya kina > Sauti chaguo-msingi ya arifa .
ARIFA
Tumia paneli ya taarifa
Unapopokea arifa mpya, kama vile ujumbe au simu zisizojibiwa, aikoni huonekana juu ya skrini.
Ili kuona maelezo zaidi kuhusu arifa, telezesha chini kuanzia juu ya skrini. Ili kufunga
mwonekano, pitisha juu kwenye skrini.
Ili kubadilisha mipangilio ya taarifa ya programu, gusa Mipangilio > Programu na taarifa , gusa
jina la programu na Arifa .
Arifa za ujumbe
Unaweza kuyapatia kipaumbele mazungumzo yako muhimu sana. Unapopokea arifa kuhusu
ujumbe mpya, telezesha chini kuanzia juu ya skrini. Gusa na ushikilie ujumbe na uguse
Kipaumbele > Tekeleza . Mazungumzo hukaa juu ya orodha ya mazungumzo, na skrini ya
kufuli huonyesha iwapo kuna jumbe mpya katika mazungumzo yaliyopatiwa kipaumbele.
Ili kuamilisha vipengele, gusa ikoni za mipangilio ya haraka kwenye paneli ya arifa. Ili kuona ikoni
zaidi, kokoa menyu chini.
Ili kupanga upya ikoni, gusa , gusa na ushikilie ikoni, na uikokote kwenye eneo lingine.
DHIBITI SAUTI
Badilisha sauti
Ikiwa una tatizo la kusikia simu yako ikiita katika mazingira yenye kelele, au simu ina sauti ya
juu, unaweza kubadilisha sauti kama upendavyo kwa kutumia vitufe vya sauti upande wa simu
yako.
Usiunganishe kwenye bidhaa ambazo zinaunda ishara ya kutoa, kwa kuwa hii inaweza kuharibu
kifaa. Usiunganishe chanzo chochote cha stima kwenye kiunganisha cha sauti. Ukiunganisha
kifaa chochote cha nje au vifaa vyovyote vya sauti kando na vile vilivyoidhinishwa kutumiwa na
kifaa hiki, Kiunganishi cha sauti, kuwa makini sana na viwango vya sauti.
Badilisha sauti ya midia na programu
Bonyeza kitufe cha sauti upande wa simu yako ili uone upau wa hali ya sauti, gusa , na
ukokote kitelezi kwenye upau wa sauti kwa midia na programu kushoto au kulia.
Weka simu kimya
Ili kuweka simu kuwa kimya, bonyeza kitufe cha kupunguza zaidi, gusa ili uweke simu yako
kutetema pekee na uguse ili kuiweka kimya.