Muhimu: Kwa maelezo muhimu kuhusu matumizi salama ya kifaa na betri yako, soma maelezo
ya ”Kwa usalama wako” na ”Usalama wa Bidhaa” katika mwongozo uliochapishwa wa mtumiaji,
au kwenye www.nokia.com/support kabla utumie kifaa. Ili kujua jinsi ya kuanza kutumia kifaa
chako kipya, soma mwongozo uliochapishwa wa mtumiaji.
Jiepushe kugusa eneo la antena bila sababu wakati antena inatumika. Ugusaji antena huathiri
ubora wa mawasiliano na unaweza kupunguza maisha ya betri kwa sababu ya kiwango cha juu
Usiunganishe kwenye bidhaa ambazo zinaunda ishara ya kutoa, kwa kuwa hii inaweza kuharibu
kifaa. Usiunganishe chanzo chochote cha stima kwenye kiunganisha cha sauti. Ukiunganisha
kifaa chochote cha nje au vifaa vyovyote vya sauti kando na vile vilivyoidhinishwa kutumiwa na
kifaa hiki, Kiunganishi cha sauti, kuwa makini sana na viwango vya sauti.
Sehemu nyingine za kifaa hiki zina sumaku. Vitu vya chuma vinaweza kuvutwa na kifaa. Usiweke
kadi za mkopo au kadi nyingine zenye mkanda wa sumaku karibu na kifaa kwa kipindi cha muda
mrefu, kwa kuwa kadi hizo zinaweza kuharibika.
INGIZA AU ONDOA SIM NA KADI YA KUMBUKUMBU
Ingiza SIM na kadi ya kumbukumbu
1. Fungua trei ya SIM na trei ya kadi ya kumbukumbu kwa kuweka kifungua trei kilichomo
kwenye mashimo kando ya trei.
2. Weka nano-SIM kwenye kipengo cha 1 kilicho kwenye trei eneo la mguso likiangalia chini.
Ikiwa una SIM mbili na SIM ya pili, unaweza kuingiza SIM au kadi ya kumbukumbu kwenye
kipenyo cha 2. Ikiwa una SIM moja, unaweza kuweka tu kadi ya kumbukumbu kwenye
kipenyo cha 2.
3. Telezesha trei ya SIM na kadi ya kumbukumbu mahali pake.
Kumbuka: Ikiwa una SIM Mbili yenye trei moja pekee ya SIM, huwezi kutumia SIM kadi mbili na
kadi ya kumbukumbu kwa wakati mmoja.
Fungua trei za SIM na kadi ya kumbukumbu, ondoa kadi, na utelezeshe trei ndani ya vipenyo
vyake.
1
Tumia kadi halisi ya nano-SIM tu. Matumizi ya SIM kadi zisizotangamana huenda yakaharibu kadi au
kifaa, na huenda yakaharibu data iliyohifadhiwa kwenye kadi.
CHAJI SIMU YAKO
Chaji betri
1. Chomeka chaja inayotangamana kwenye soketi ya ukuta.
2. Unganisha kebo kwenye simu yako.
Simu yako inakubali kebo ya USB ya micro-B. Pia unaweza kuchaji simu yako kutoka kwenye
kompyuta kwa kutumia kebo ya USB, lakini inaweza kuchukua muda mrefu zaidi.
2. Chagua ni data gani unayotaka irejeshwe kwenye simu yako. Usawazishaji utaanza
kiotomatiki punde simu yako inapounganishwa kwenye intaneti.
Rejesha mipangilio ya programu kutoka kwenye simu yako ya awali ya Android
Ikiwa kifaa chako cha awali kilikuwa cha Android , na uhifadhi nakala ya akaunti ya Google
kwayo, unaweza kurejesha mipangilio ya programu na manenosiri ya Wi-Fi.
1. Gusa Mipangilio > Hifadhi nakala na weka upya .
2. Badilisha Onyesha upya otomatiki kwa Washa .
MIPANGILIO YA SIM MBILI
Ikiwa una toleo la SIM mbili, unaweza kuwa na SIM 2 kwenye simu yako, kwa mfano, moja ya kazi
yako na nyingine ya matumizi yako ya kibinafsi.
Kumbuka: Kwenye vifaa vyenye uwezo wa SIM mbili, vipenyo vya SIM1 na SIM2 hukubali
mitandao ya 4G. Hata hivyo, ikiwa SIM1 na SIM2 zako ni kadi za SIM za LTE, mitandao msingi
hukubali mitandao ya 4G/3G/2G, wakati SIM ya pili inaweza kukubati tu 3G/2G. Kwa maelezo
zaidi kuhusu SIM kadi zako, wasiliana na mtoa huduma wako.
Kwa mfano, wakati unapiga simu, unaweza kuchagua ni SIM gani ya kutumia kwa kugusa kitufe
kinacholingana cha SIM 1 au SIM 2 baada ya kupiga nambari hiyo.
Simu yako huonyesha hali ya mtandao ya SIM zako kitofauti. SIM kadi zote zinapatikana kwa
wakati mmoja wakati kifaa hakitumiki, lakini wakai SIM kadi moja inatumika, kwa mfano, wakati
wa kupiga simu, ile nyingine inawezakosa kupatikana.
Dhibiti SIM zako
Hutaki kazi iingiliane na muda wako huru? Au una muunganisho wa bei nafuu wa data kwenye
SIM moja? Unaweza kuamua ni SIM gani unayotaka kutumia.
Gusa Mipangilio > SIM Kadi .
Badili jina la SIM kadi
Gusa SIM unayotaka kubadilisha jina, na uandike jina unalotaka.
Chagua ni SIM gani ya kutumia kwa simu au muunganisho wa data
Chini ya SIM unayopendelea ya , gusa mpangilio unaotaka kubadilisha na uchague SIM.
FUNGA AU FUNGUA SIMU YAKO
Funga simu yako
Kiwa unataka kuepuka kupiga simu kwa makosa wakati simu yako iko kwenye mfuko au begi
lako, unaweza kufunga vitufe na skrini yako.
Ili kufunga vitufe na skrini yako, bonyeza kitufe cha nishati.
Fungua vitufe na skrini
Bonyeza kitufe cha nishati, na utelezeshe juu kwenye skrini. Ukiulizwa, toa hati tambulishi za
ziada.
TUMIA SKRINI YA MGUSO
Muhimu: Epuka kugwara skrini ya mguso. Usitumie kamwe kalamu, penseli halisi, au kitu
Skrini huzunguka kiotomatiki wakati unapindua simu kwa digrii 90.
Ili kufunga skrini katika hali mkao wima, telezesha chini kutoka juu ya skrini, na uguse
Zungusha kiotomatiki ili ubadilishe kwa Wima .
Tumia vitufe vya urambazaji
Ili kuona ni programu gani ulizofungua, gusa kitufe cha muhtasari .
Ili kubadilisha kwa programu nyingine, gusa programu unayotaka. Ili kufunga programu, gusa
ikoni ya kando yake.
Ili kurejesha kwenye skrini ya awali uliyokuwa, gusa kitufe cha nyuma . simu yako hukumbuka
programu na tovuti zote ulizotembelea tangu wakati wa mwisho skrini yako ilipofungwa.
Ili kwenda kwenye skrini ya mwanzo, gusa kitufe cha mwanzo . Programu uliyokuwa ukitumia
hubakia imefunguliwa chinichini.
Fungua programu mbili kwa wakati mmoja
Kwa urambazaji rahisi kati ya programu, bonyeza na ushikilie kitufe cha muhtasari cha ili
kugawanya skrini kati ya programu mbili. Kurudi kwenye mwonekano wa kawaida, bonyeza na
ushikilie cha muhtasari.
Jifunze jinsi ya kubinafsisha Skrini ya mwanzo na jinsi ya kubadilisha toni za mlio.
Badilisha mandhari yako
Gusa Mipangilio > Skrini > Mandhari .
Badilisha toni yako ya mlio ya simu yako
1. Gusa Mipangilio > Sauti .
2. Gusa Mlio wa simu wa SIM1 au Mlio wa simu wa SIM2 ili uchague mlio wa simu wa kila SIM.
Badilisha toni ya mlio ya taarifa ya ujumbe wako
1. Gusa Mipangilio .
2. Gusa Sauti .
3. Gusa Toni ya mlio ya chaguo-msingi ya arifa .
FUNGUA NA UFUNGE PROGRAMU
Fungua programu
Kwenye skrini ya mwanzo, gusa ikoni ya programu ili kuifungua. Ili kufungua mojawapo ya
programu zinazoendeshwa kichini chini, gusa , na uchague programu.
Fungua programu
Gusa , na uguse kwenye programu unayotaka kufunga.
Tafuta programu zako
Kwenye skrini ya mwanzo, telezesha juu kuanzia chini ya skrini ili uone programu zako zote.
Bonyeza , pitisha juu kwenye programu zote, na uguse ONDOA ZOTE .
ARIFA
Pata kujua kinachoendelea kwenye simu yako kwa kutumia arifa.
Tumia paneli ya taarifa
Unapopokea arifa mpya, kama vile ujumbe au simu zisizojibiwa, aikoni ya kiashiriaji huonekana
kwenye upau wa hali juu ya skrini. Ili kuona maelezo zaidi kuhusu aikoni, fungua paneli ya taarifa
na uangalie maelezo.
Ili kufungua paneli ya arifa, kokota upau wa hali kuelekea chini. Ili kufunga paneli ya arifa,
pitisha juu kwenye skrini.
Ili kubadilisha mipangilio ya taarifa ya programu, gusa Mipangilio > Arifa na uguse jina la
programu ili ufungue mipangilio ya programu.
Tumia ikoni za mpangilio wa haraka
Ili kuamilisha vipengele, gusa ikoni za mipangilio ya haraka kwenye paneli ya arifa. Ili kuona ikoni
zaidi, kokoa menyu chini.
Ili kupanga upya ikoni, gusa , gusa na ushikilie ikoni, na uikokote kwenye eneo lingine.
Ikiwa una tatizo la kusikia simu yako ikiita katika mazingira yenye kelele, au simu ina sauti ya
juu, unaweza kubadilisha sauti kama upendavyo kwa kutumia vitufe vya sauti upande wa simu
yako.
Usiunganishe kwenye bidhaa ambazo zinaunda ishara ya kutoa, kwa kuwa hii inaweza kuharibu
kifaa. Usiunganishe chanzo chochote cha stima kwenye kiunganisha cha sauti. Ukiunganisha
kifaa chochote cha nje au vifaa vyovyote vya sauti kando na vile vilivyoidhinishwa kutumiwa na
kifaa hiki, Kiunganishi cha sauti, kuwa makini sana na viwango vya sauti.
Badilisha sauti ya midia na programu
Bonyeza kitufe cha sauti upande wa simu yako ili uone upau wa hali ya sauti, gusa , na
ukokote kitelezi kwenye upau wa sauti kwa midia na programu kushoto au kulia.
Weka simu kimya
Bonyeza kitufe cha sauti kwenye upande wa simu yako, na uguse ili kuifanya iwe kimya.
Dokezo: Hutaki kuweka simu yako katika hali kimya, lakini huwezi kujibu sasa hivi? Ili
kunyamazisha simu inayoingia, bonyeza kitufe cha kupunguza sauti . Unaweza kuweka
simu yako kunyamazisha mlio wa simu ukiichukua: Gusa Mipangilio > Mwendo >
Nyamazisha ikichukuliwa .
Kama unataka kuweza kukataa simu kwa haraka, wezesha Mwendo. gusa Mipangilio >
Mwendo > Pindua ili ukatae simu . Wakati kuna simu inayoingia, pindua simu ili ukatae simu.
PICHA ZA SKRINI
Piga picha ya skrini
Ili kupiga picha ya skrini, fungua paneli ya arifa, na ukokote upau wa hali kuelekea chini. Gusa
Nasa skrini . Unaweza kutazama picha zilizonaswa katika Picha .
Haiwezekani kunasa picha ya skrini wakati unatumia baadhi ya programu na vipengele.
MAISHA YA BETRI
Pata mengi kutoka kwa simu yako ukipata maisha ya betri unayotaka. Kuna hatua unazoweza
kuchukua kuokoa nishati kwenye simu yako.
2. Chagua tu sauti ambazo unazihitaji:
Nyamazisha sauti zisizohitajika, kama vile
sauti za kubofya vitufe. Gusa Mipangilio >
Sauti , na chini ya Sauti nyingine , chagua
ni sauti gani za kuweka.
3. Tumia vifaa vya sauti vyenye waya, badala
ya kipasa sauti.
4. Badilisha mipangilio ya skrini ya simu:
Weka skrini ya simu ili kuzima baada ya
muda mfupi. Gusa Mipangilio > Skrini >
Lala na uchague muda.
5. Punguza mwangaza wa skrini:
Gusa Mipangilio > Skrini >
Hali ya mwangaza . Hakikisha kwamba
Mwangaza wa kiotomatiki haujawekwa
tiki. Ili kurekebisha mwangaza, kokota
kitelezi cha Hali ya mwangaza .
6. Komesha programu zinazoendeshwa
kichini chini: Bonyeza , na ufunge
programu ambazo hauhitaji.
7. Tumia huduma za eneo kwa kuchagua:
Zima huduma za eneo wakati hauzihitaji.
Gusa Mipangilio > Eneo , na ubadilishe
kwa Zima .
8. Tumia miunganisho ya mtandao kwa
kuchagua: Washa Bluetooth wakati
inahitajika tu. Tumia muunganisho wa
Wi-Fi ili uunganishe kwenye intaneti,
badala ya muunganisho wa data ya
simu. Komesha simu yako kutafuta
mitandao inayopatikana ya pasi waya.
Gusa Mipangilio > Wi-Fi , na ubadilishe
kwa Zima . Kama unasikiliza muziki au
unatumia simu yako, lakini hutaki kupiga
au kupokea simu, washa hali ya Ndege.
Gusa Mipangilio > Zaidi > Hali ya ndege .
OKOA GHARAMA YA UTUMIAJI DATA NJE YA MTANDAO WAKO WA KAWAIDA
Unaweza kupunguza gharama za utumiaji data nje ya mtandao wako wa kawaida na kuokoa
pesa kwenye bili ya simu yako kwa kubadilisha mipangilio ya data ya simu ya mkononi. Ili
kutumia mbinu bora ya muunganisho, badilisha mipangilio ya Wi-Fi na mitandao ya simu.
Utumiaji data nje ya mtandao wako wa kawaida humaanisha kutumia simu yako kupokea
data kwenye mitandao ambayo mtoa huduma wako wa mtandao hamiliki au kuendesha.
Kuunganisha kwenye intaneti wakati unatumia data ya nje ya mtandao wako wa kawaida, hasa
ukiwa ng’ambo, kunaweza kupandisha gharama ya data pakubwa. Kutumia muunganisho wa
Wi-Fi kwa kawaida huwa haraka na bei nafuu kuliko kutumia muunganisho wa data ya simu
ya mkononi. Kama miunganisho yote ya Wi-Fi na data ya simu ya mkononi inapatikana, simu
hutumia muunganisho wa Wi-Fi.
Unganisha kwenye mtandao wa Wi-Fi
1. Gusa Mipangilio > Wi-Fi .
2. Hakikisha mtandao wa Wi-Fi umewekwa kwa Washa .
3. Chagua muunganisho unaotaka kutumia.
Funga muunganisho wa data ya simu ya mkononi
Telezesha chini kuanzia juu ya skrini, gusa na ubadilishe Data ya simu ya mkononi kwa
Ili kufuata matumizi ya data yako, gusa Mipangilio > Matumizi ya data .
Komesha utumiaji data nje ya mtandao wako wa kawaida
Gusa Mipangilio > Zaidi > Mitandao ya simu za mkononi , na uzime
Utumiaji data nje ya mtandao wako wa kawaida .
ANDIKA MAANDISHI
Jifunze jinsi ya kuandika maandishi kwa haraka na vizuri kwa kutumia kibodi ya simu yako.
Tumia kibodi kwenye skrini
Kuandika kwa kutumia kibodi kwenye skrini ni rahisi. Unaweza kutumia kibodi ukiwa umeshikilia
simu yako katika hali wima au mlalo. Mpangilio wa kibodi unaweza kutofautiana katika
programu na lugha tofauti.
Ili kufungua kibodi kwenye skrini, gusa kisanduku cha maandishi.
Badilisha kati ya vibambo vikubwa na vidogo
Gusa kitufe cha shift. Ili kuwasha hali ya caps lock, gusa kitufe mara mbili. Ili kurejea hali ya
kawaida, gusa tena kitufe cha shift.
Charaza namba au kibambo maalum
Gusa nambari na Kitufe cha alama. Baadhi vitufe vya vibambo maalum huleta alama zaidi. Ili
kuona alama zaidi, gusa na ushikilie alama au kibambo maalum.
Ingiza emoji
Gusa kitufe cha emoji, na uchague emoji.
Nakili au bandika maandishi
Gusa na ushikilie neno, kokota viweka alama kabla na baada ya neno ili kuangazia sehemu
unayotaka kunakili na uguse NAKILI . Ili kubandika maandishi, gusa ni wapi unataka kubandika
maandishi na uchague BANDIKA .
Gusa na ushikilie kibambo, na uguse lafudhi au kibambo cha lafushi, ikiwa inakubaliwa na kibodi
yako.
Futa kibambo
Gusa kitufe cha backspace.
Sogeza kasa
Ili kuhariri neno uliloandika, gusa neno, na uburute kasa mahali unapoitaka.
Tumia mapendekezo ya neno la kibodi
Simu yako hupendekeza maneno unapokuwa ukiandika, ili kukusaidia kuandika kwa haraka na
kwa usahihi zaidi. Mapendekezo ya maneno yanaweza kutopatikana katika lugha zote.
Wakati unapoanza kuandika neno, simu yako itapendekeza maneno yanayowezekana. Neno
unalotaka likionyeshwa kwenye upau wa mapendekezo, chagua neno. Ili kuona mapendekezo
zaidi, gusa na ushikilie pendekezo.
Ikiwa neno lililopendekezwa limewekwa alama ya koza, simu huitumia kiotomatiki ili
kubadilisha neno uliloandika. Ikiwa neno si sahihi, gusa na ushikilie ili kuona mapendekezo
mengine machache.
Ikiwa hutaki kibodi kupendekeza maneno unapokuwa ukicharaza, zima sahihisho za matini.
Gusa Mipangilio > Lugha na ingizo > Kibodi pepe . Teua kibodi unayotumia kwa kawaida.
Gusa Usahihishaji matini na uzime mbinu za kusahihisha matini ambayo hutaki kutumia.
Sahihisha neno
Ukigundua ya kwamba umekosea tahajia ya neno, gusa ili kuona mapendekezo ya kusahihisha
neno.
Zima kikagua tahajia
Gusa Mipangilio > Lugha na ingizo > Kikagua tahajia , na ubadilishe Kikagua tahajia kwa
Zima .
TAREHE NA SAA
Fuatilia muda – jifunze jinsi ya kutumia simu yako kama saa, na hata pia saa ya kengele, na jinsi
ya kusasisha miadi, kazi, na ratiba zako.
Unaweza kuweka simu yako kusasisha saa, tarehe, na ukanda wa saa kiotomatiki. Usasishaji
otomatiki ni huduma ya mtandao na huenda usipatikane kulingana na eneo lako au mtoa
huduma wa mtandao.
1. Gusa Mipangilio > Tarehe na saa .
2. Gusa Tarehe na saa otomatiki > tumia saa inayotolewa na mtandao .
3. Washa Ukanda otomatiki wa saa .
Badilisha saa kuwa fomati ya saa 24
Gusa Mipangilio > Tarehe na Saa , na uwashe Tumia fomati ya saa 24 .
SAA NA KENGELE
Saa yako sio ya kengele tu – jifunze ni nini kingine unachoweza kufanya.
Tumia kipima saa
Hakuna kuunguza chakula tena – tumia kipima saa ili kupima saa zako za upishi.
1. Gusa Saa > KIPIMA SAA .
2. Weka muda wa kipima saa.
Tumia saa ya michezo
Tumia saa ya michezo ili kuona jinsi unavyoweza kuimarika kwa mbio.
3. Ili kurekebisha kengele, iguse. Ili kuweka kengele kujirudia katika tarehe maalum, weka tiki
kwenye Rudia na uangazie siku za wiki.
Sinzisha kengele
Ikiwa bado hutaki kuamka, wakati kengele inapotoa sauti, pitisha kengele kushoto. Ili
kurekebisha muda wa kusinzisha, gusa Saa > > Mipangilio > Muda wa kusinzisha na
uchague urefu kama upendavyo.
Zima kengele
Wakati kengele inapotoa sauti, pitisha kengele kulia.
Futa kengele
Gusa Saa > KENGELE . Chagua kengele, na uguse Futa .
KIKOKOTOO
Umesahau kikokotoo chako cha mfukoni – kuna kikokotoo kwenye simu yako.
Tumia kikokotoo
Gusa Kikokotoo .
Ili kutumia kikokotoo mahiri, telezesha upau kuanzia ukingo wa kulia mwa skrini hadi kushoto.
UFIKIAJI
Unaweza kubadilisha mipangilio mbalimbali ili kufanya kutumia simu yako kuwa rahisi.
3. Ili kujibu ujumbe, gusa , au gusa > Jibu zote .
Futa barua
1. Gusa Gmail .
2. Gusa ujumbe unaotaka kufuta na kugusa .
4. Charaza mada ya ujumbe na barua.
5. Gusa .
Ongeza kutoka kwenye Anwani .
3. Ili kufuta ujumbe anuwai, gusa mviringo wenye herufi za wapokeaji ili kuchagua ujumbe na
uguse .
TANGAMANA NA WATU
Je, unataka kuunganika na kushiriki vitu na watu katika maisha yako? Ukiwa na programu ya
jamii, unaweza kupashwa ni nini kinachofanyikia marafiki wako.
Programu za jamii
Ili kuendelea kuwasiliana na marafiki na familia yako, ingia katika huduma zako za utumaji
ujumbe, kushiriki, na mitandao ya jamii. Chagua huduma unayotaka kutumia kutoka kwenye
skrini yako ya Mwanzo. Programu za jamii zinapatikana kwenye Duka la Google Play . Huduma
zinazopatikana huenda zikatofautiana.
Je, kwanini ubebe kamera ya kando kama simu yako ina kila kitu unachohitaji ili kunasa
kumbukumbu? Kwa kutumia kamera ya simu yako, unaweza kupiga picha au kurekodi video kwa
urahisi.
Piga picha
Piga picha nzuri na maridadi – nasa nyakati bora katika albamu ya picha yako.
1. Gusa Kamera .
2. Lenga unachotaka kupiga picha.
3. Gusa kitufe cha kilago .
Jipige picha
Unahitaji kujipiga picha nzuri? Tumia kamera ya mbele ya simu ili kupiga picha hiyo.
1. Gusa Kamera .
2. Badilisha kwa kamera ya mbele.
3. Lenga unachotaka kupiga picha.
4. Gusa kitufe cha kilago .
TUMIA KAMERA YAKO KAMA MTAALAMU
Ili kuhakikisha kuwa umedhibiti kila hali ya picha yako, weka kamera yako kwenye Hali ya mkono.
Unataka kuwa na muda wa kuingia kwenye picha pia? Jaribu kutumia kipima saa.
1. Gusa Kamera .
2. Gusa . Kitufe huonyesha mpangilio wa kipima saa. Ili kuibadilisha, iguse tena.
Teua ufichuzi bora
Ili kubadilisha mipangilio ya ufichuzi, katika Hali ya mkono, gusa , na uchague mpangilio.
Piga picha zenye ubora wa juu
Katika programu ya Kamera, gusa > Mwonekano , na uweke mwonekano ambao unataka.
HIFADHI PICHA NA VIDEO ZAKO KWENYE KADI YA KUMBUKUMBU
Ikiwa kuna kadi ya kumbukumbu kwenye simu yako, na kumbukumbu ya simu inajaa, hifadhi
picha na video ulizorekodi kwenye kadi ya kumbukumbu.
Dokezo: Kwa video ya ubora wa juu, rekodi video kwenye kumbukumbu ya simu yako.
Ukirekodi video kwenye kadi ya kumbukumbu, inapendekezwa kwamba kadi ya microSD
unayotumia iwe kadi ya 4–128GB kutoka kwa mtengenezaji anayejulikana vizuri.
Badilisha eneo la picha na video zilizohifadhiwa
1. Gusa Kamera .
2. Gusa > Mipangilio > Hifadhi ya data .
PICHA NA VIDEO ZAKO
Tazama picha na video kwenye simu yako
Je, unataka kukumbuka nyakati hizo muhimu? Tazama picha na video kwenye simu yako.
Ungependa kutazama picha na video zako kwenye skrini kubwa? Zisogeze kwenye kompyuta
yako.
Unaweza kutumia kidhibiti faili cha kompyuta yako kunakili au kusogeza picha na video zako
kwenye kompyuta.
Unganisha simu yako kwenye kompyuta na kebo ya USB inayotangamana. Ili kuweka aina ya
muunganisho wa USB, fungua paneli ya taarifa, na uguse taarifa ya USB.
Shiriki picha na video zako
Unaweza kushiriki picha na video zako kwa haraka na kwa urahisi ili marafiki na familia yako
wazione.
1. Katika Picha , gusa picha unayotaka kushiriki na uguse .
2. Chagua jinsi unavyotaka kushiriki picha au video.
Kutumia muunganisho wa Wi-Fi kwa kawaida huwa haraka na bei nafuu kuliko kutumia
muunganisho wa data ya simu. Kama miunganisho yote ya Wi-Fi na data ya simu inapatikana,
simu hutumia muunganisho wa Wi-Fi.
Washa Wi-Fi
1. Gusa Mipangilio > Wi-Fi .
2. Badilisha Wi-Fi kwa Washa .
3. Chagua muunganisho unaotaka kutumia.
Muunganisho wako wa Wi-Fi unatumika wakati imeonyeshwa kwenye upau wa hali juu ya
skrini.
Kumbuka: Kutumia Wi-Fi huenda kumezuiwa katika nchi zingine. Kwa mfano, katika Ulaya, unaruhusiwa
tu kutumia 5150-5350 MHz Wi-Fi ukiwa ndani tu, na nchini Marekani na Kanada, unaruhusiwa kutumia
5.15-5.25 GHz Wi-Fi ukiwa ndani tu. Kwa maelezo zaidi, wasiliana na utawala wa eneo lako.
Muhimu: Tumia usimbuaji ili kuongeza usalama wa muunganisho wako wa Wi-Fi. Kutumia usimbuaji
hupunguza hatari ya wengine kufikia data yako.
1
Dokezo: Ikiwa unataka kufuatilia maeneo wakati mawimbi ya setileti hayapatikani, kwa mfano
wakati uko ndani au kati ya majengo marefu, washa Wi-fi ili uboreshe usahihi wa mkao.
TUMIA MUUNGANISHO WA DATA YA SIMU YA MKONONI
Washa muunganisho wa data ya simu ya mkononi
Telezesha chini kuanzia juu ya skrini, gusa na ubadilishe Data ya simu ya mkononi kwa
Washa .
1
Tumia muunganisho wa data ya simu ya mkononi wakati unaranda
Gusa Mipangilio > Zaidi > Mitandao ya simu za mkononi , na uweke
Utumiaji data nje ya mtandao wako wa kawaida kwa Washa .
Dokezo: Ili kufuata matumizi ya data yako, gusa Mipangilio > Matumizi ya data .
1
Kuunganisha kwenye intaneti wakati unatumia data ya nje ya mtandao wako wa kawaida, hasa ukiwa
ng’ambo, kunaweza kupandisha gharama ya data pakubwa.
Tumia simu yako kuunganisha kompyuta yako kwenye wavuti
Ni rahisi kutumia intaneti kwenye kompyuta yako ndogo mahali popote. Fanya simu yako
iwe mtandao-hewa wa Wi-Fi, na utumie muunganisho wako wa data ya simu ili ufikie intaneti
kwenye kompyuta yako ndogo au kifaa kingine.
1. Gusa Mipangilio > Zaidi > Kushiriki na kusambaza intaneti .
2. Washa Sambaza intaneti ya Wi-Fi ili ushiriki muunganisho wako wa data ya simu kwenye Wi-
Fi, au unganisha Bluetooth ili utumie Bluetooth.
Kifaa kile kingine hutumia data kutoka kwa mpango wako wa data, ambayo inaweza
kusababisha gharama ya matumizi ya data. Kwa maelezo kuhusu upatikanaji na gharama,
wasiliana na mtoa huduma wa mtandao wako.
Anzisha kivinjari
Jifahamishe juu ya habari, na tembelea tovuti zako uzipendazo. Unaweza kutumia
Google Chrome kwenye simu yako ili utazame kurasa za wavuti kwenye intaneti. Chrome
inaweza pia kukusaidia kukuonya dhidi ya vitisho vya usalama.
Ili kuvinjari wavuti, lazima uunganishwe kwenye intaneti.
Gusa Chrome .
Anza kuvinjari
Hakuna haja ya kompyuta – unaweza kuvinjari intaneti kwa urahisi kwenye simu yako.
1. Gusa Chrome .
2. Charaza anwani ya wavuti na uguse .
Dokezo: Kama mtoa huduma wako wa mtandao hakulipishi ada moja kwa uhamishaji data, ili
kuokoa gharama ya data, tumia mtandao wa Wi-Fi ili kuunganisha kwenye tovuti.
Fungua kichupo kipya
Wakati unataka kutembelea tovuti kadhaa kwa wakati mmoja, unaweza kufungua vichupo vipya
vya kuvinjari na uvitumie vyote kwa wakati mmoja.
Katika Chrome,
1. Gusa kisanduku kinachofuata kwenye upau wa anwani.
1. Gusa kisanduku kinachofuata kwenye upau wa anwani.
2. Gusa kichupo unachotaka.
Funga kichupo
Katika Chrome,
1. Gusa kisanduku kinachofuata kwenye upau wa anwani.
2. Gusa X kwenye kichupo unachotaka kufunga.
Tafuta wavuti
Chunguza wavuti na ulimwengu wa nje kwa kutumia Utafutaji wa Google. Unaweza kutumia
kibodi kuandika maneno yako ya utafutaji.
Katika Chrome,
1. Gusa upau wa utafutaji.
2. Andika neno lako la utafutaji katika kisanduku cha utafutaji.
3. Gusa .
Unaweza pia kuchagua neno la kutafuta kutoka kwenye matokeo yanayopendekezwa.
Tumia mpango wako wa data vizuri
Ikiwa una wasiwasi kuhusu gharama ya matumizi yako ya data, simu yako itakusaidia kuzuia
baadhi ya programu dhidi ya kutuma au kupokea data wakati zinaendeshwa chini chini.
1. Gusa Mipangilio > Matumizi ya data > Kiokoa data .
Okoa betri yako kwa kufunga miunganisho ya intaneti ambayo imefunguka chini chini. Unaweza
kuifanya bila kufunga programu zozote.
1. Gusa Mipangilio > Wi-Fi .
2. Badilisha Wi-Fi kwa Zima .
Funga muunganisho wa data ya simu ya mkononi
1. Pitisha chini kutoka juu ya skrini.
2. Gusa .
3. Badilisha Data ya simu ya mkononi kwa Zima .
Washa hali ya ndege
1. Gusa Mipangilio > Zaidi .
2. Washa Hali ya ndege .
Hali ya ndege hufunga miunganisho kwenye mitandao ya simu za mkononi na huzima vipengele
pasiwaya vya kifaa chako. Fuata maagizo na mahitaji ya usalama yanayotolewa na, kwa mfano,
ndege, na sheria na masharti yoyote husika. Inaporuhusiwa, unaweza kuunganisha kwenye
mtandao wa Wi-Fi ili, kwa mfano, vinjari intaneti au washa kushiriki Bluetooth kwenye hali ya
ndege.
BLUETOOTH
Unaweza kuuunganisha pasi waya kwenye vifaa vingine vinavyotangamana, kama vile simu,
kompyuta, vifaa vya sauti, na vifaa vya gari. Unaweza pia kutuma picha zako kwa simu
zinazotangamana au kwenye kompyuta yako.
Unganisha kwenye kifaa cha ziada cha Bluetooth
Unaweza kuunganisha simu yako na vifaa vingi muhimu vya Bluetooth. Kwa mfano, na vifaa vya
sauti vya pasi waya (kinauzwa kando), unaweza kuongea na simu bila kutumia mikono - unaweza
kuendelea unachofanya, kama kufanya kazi kwenye kompyuta, wakati wa simu. Kuunganisha
simu kwenye kifaa cha Bluetooth huitwa kuoanisha.
Huenda ukahitajika kuanzisha mchakato
wa kuoanisha kutoka kwenye kifaa kingine.
Kwa maelezo zaidi, angalia mwongozo wa
kifaa hicho kingine.
Kwa kuwa vifaa vyenye teknolojia pasi waya ya Bluetooth huwasiliana kwa kutumia mawimbi ya
redio, havihitaji kuwa vinaangaliana. Hata hivyo, lazima vifaa vyako vya Bluetooth viwe mita 10
(futi 33) na kifaa kile kingine, ijapokuwa muunganisho unaweza kuathiriwa na vizuizi kama vile
kuta au kutoka vifaa vingine vya elektroniki.
vifaa vilivyolinganishwa vinaweza bado kuunganishwa kwenye simu yako wakati Bluetooth
imewashwa. Vifaa vingine vinaweza kugundua simu yako tu ikiwa mwonekano wa mipangilio ya
Bluetooth imefunguliwa.
Usilinganishe au kukubali maombi ya muunganisho kutoka kwa kifaa kisichojulikana. Hii
husaidia kulinda simu yako dhidi ya maudhui mabaya.
4. Ili kuoanisha simu yako na kifaa, gusa kifaa
kwenye orodha ya vifaa vilivyogunduliwa
vya Bluetooth.
5. Huenda ukahitaji kucharaza alamasiri
za ruhusa. Kwa maelezo zaidi, angalia
mwongozo wa kifaa hicho kingine.
Tenganisha kifaa kilichooanishwa cha Bluetooth
Ikiwa hutaki tena simu yako iwe imeunganishwa kwenye kifaa kingine, unaweza kuitenganisha.
1. Gusa Mipangilio > Bluetooth .
2. Gusa jina la kifaa kilichooanishwa.
3. Gusa Sawa ili kuthibitisha.
Unapowasha simu yako tena, muunganisho hujifungua tena kiotomatiki.
Ondoa uoanishaji
Ikiwa huna kifaa ulichooanisha na simu yako, unaweza kuondoa uoanishaji huo.
1. Gusa Mipangilio > Bluetooth .
2. Gusa kando ya jina la kifaa.
3. Gusa SAHAU .
Unganisha kwenye simu ya rafiki yako kwa kutumia Bluetooth
Unaweza kutumia Bluetooth pasi waya kuunganisha kwenye simu ya rafiki yako, ili kushiriki
picha, na zaidi.
2. Hakikisha Bluetooth imewashwa katika
simu zote.
3. Hakikisha simu zote zinaonekana kwenye
zingine. Unahitaji kuwa katika mwonekano
wa mipangilio ya Bluetooth kwa simu yako
Msimbosiri hutumika tu wakati unaunganisha kifaa kwa mara ya kwanza.
Tuma maudhui yako kwa kutumia Bluetooth
Wakati unataka kushiriki maudhui yako au kutuma picha ulizopiga kwa rafiki, tumia Bluetooth
kuzituma kwenye vifaa vinavyotangamana,
Unaweza kutumia zaidi ya muunganisho mmoja wa Bluetooth kwa wakati mmoja. Kwa mfano,
wakati unatumia vifaa vya sauti vya Bluetooth, unaweza bado kutuma vitu vingine kwenye kifaa
kingine.
kuonekana kwenye simu zingine.
4. Unaweza kuona simu za Bluetooth zilizo
karibu. Gusa simu unayotaka kuunganisha.
5. Ikiwa simu inahitaji msimbosiri, uaandike
au kubali msimbosiri, na uguse Oanisha .
1. Gusa Mipangilio > Bluetooth .
2. Badilisha Bluetooth kwa Washa .
3. Nenda kwenye maudhui unayotaka
kutuma, na uguse > Bluetooth .
4. Gusa kifaa unachotaka kuunganisha.
Unaweza kuona vifaa vya Bluetooth vilivyo
Eneo la faili zilizopokewa hutegemea kifaa kile kingine. Kwa maelezo zaidi, angalia mwongozo
wa kifaa hicho kingine.
karibu.
5. Kama kifaa kinahitaji msimbosiri, charaza
msimbosiri huo. Msimbosiri, ambao
unaweza kuubuni, lazima uwekwe kwenye
vifa vyote. Msimbosiri katika vifaa vingine
huwa vimewekwa. Kwa maelezo zaidi,
angalia mwongozo wa kifaa hicho kingine.
NFC
Chunguza ulimwengu karibu na wewe. Gusa vifaa vya ziada ili kuviunganisha, na uguse lebo
ili kumpigia mtu simu au kufungua tovuti. Mawasiliano ya Karibu na Maeneo (NFC) hufanya
kuunganisha kuwa rahisi na inayopendeza.
Anza Kutumia NFC
Washa vipengele vya NFC kwenye simu yako, na uanze kugusa ili kushiriki vitu au kuunganisha
kwenye vifaa.
• Unganisha kwenye vifaa vya ziada vinavyotangamana vya Bluetooth ambavyo vinakubali
NFC, kama vile vifaa vya sauti au kipasa sauti pasi waya
• Gusa lebo ili upate maudhui zaidi ya simu yako, au kufikia huduma za mtandaoni
• Lipa kwa kutumia simu yako, ikiwa inakubaliwa na mtoa huduma wa mtandao wako
Eneo la NFC liko nyuma ya simu yako. Gusa simu, vifaa vya simu, lebo, au visomaji vingine na
eneo la NFC.
1. Gusa Mipangilio > Zaidi > NFC .
2. Badilisha NFC kwa Washa .
Kabla ya kutumia NFC, hakikisha skrini na vitufe vimefungwa.
Soma lebo za NFC
Lebo za NFC zinaweza kuwa na maelezo, kama vile anwani ya wavuti, nambari ya simu, au kadi
ya biashara. Maelezo unayotaka yako umbali wa mguso tu.
Ili kusoma lebo. gusa lebo na eneo la NFC ya simu yako.
Wezesha malipo ya NFC
Unaweza kutumia NFC ya simu yako kulipia ununuzi wako.
Ili kuwezesha malipo, gusa Mipangilio > Gusa na ulipe .
Kumbuka: Malipo na programu na huduma za tikiti zinatolewa na wahusika wengine. HMD
Global haitoi waranti yoyote au kuwajibika kwa programu au huduma zozote kama hizo
ikiwemo usaidizi, utendakazi, miamala, au upotezaji wa thamani ya kipesa. Huenda ukahitaji
kusakinisha upya na kuamilisha kadi ulizoongeza na hata pia programu ya malipo au tikiti
baada ya kifaa chako kukarabatiwa.
Unganisha kwenye kifaa cha ziada cha Bluetooth na NFC
Unatumia mikono yako? Tumia vifaa vya sauti. Au kwa nini usisikilize muziki kwa kutumia vipasa
sauti pasi waya? Unahitaji tu kugusa kifaa cha ziada kinachotangaman na simu yako.
1. Gusa eneo la NFC na kifaa cha ziada na eneo la NFC ya simu yako.*
2. Fuata maagizo kwenye skrini.
*Vifaa vya ziada vinauzwa kando. Upatikanaji wa vifaa vya ziada hutofautiana kimaeneo.
Ikiwa hutaki kuunganishwa tena kwenye kifaa cha ziada, unaweza kutenganisha kifaa hicho cha
ziada.
Gusa tena eneo la NFC la kifaa cha ziada.
Kwa maelezo zaidi, angalia mwongozo wa mtumiaji wa kifaa cha ziada.
VPN
Huenda ukahitaji muunganisho wa mtandao pepe wa binafsi (VPN) ili kufikia rasilimali za
kampuni yako, kama vile intraneti au barua ya kampuni, au utumie huduma ya VPN kwa malengo
ya kibinafsi.
Wasiliana na msimamizi wa IT wa kampuni yako kwa maelezo ya usanidi wa VPN yako, au
kukagua tovuti ya huduma ya VPN yako kwa maelezo zaidi.
Tumia muunganisho salama wa VPN
1. Gusa Mipangilio > Zaidi > VPN .
2. Ili kuongeza wasifu wa VPN, gusa .
3. Charaza maelezo ya wasifu kama ilivyoagizwa na msimamizi wa IT wa kampuni yako au
huduma ya VPN.
Sikiliza muziki wako unaopenda mahali popote ulipo.
Cheza muziki
1. Gusa Cheza Muziki > > Maktaba ya muziki .
2. Gusa msanii, albamu, wimbo, mtindo, au orodha ya kucheza unayotaka kucheza.
Sitisha au endelea kucheza
1. Gusa upau wa Inayocheza Sasa chini ya skrini ili ufungue Inayocheza Sasa .
2. Gusa au .
Dokezo: Ili kucheza nyimbo bila mpangilio, gusa .
Unda orodha ya kucheza
Panga nyimbo zako kwenye orodha za kucheza, ili uweze kusikiliza muziki ambao unafaa hisia
yako.
1. Wakati unacheza wimbo, gusa > Ongeza kwenye orodha ya kucheza .
2. Ili kuongeza wimbo kwenye orodha yako mpya ya kucheza, gusa
ORODHA MPYA YA KUCHEZA , au, ili kuongeza wimbo kwenye orodha ya kucheza iliyopo,
chagua orodha ya kucheza kwenye orodha.
Ongeza nyimbo kwenye simu yako
Ikiwa una muziki au video iliyohifadhiwa kwenye kompyuta yako, lakini unataka kuzifikia kwenye
simu yako, tumia kebo ya USB ili kusawazisha midia kati ya simu na kompyuta yako.
1. Unganisha simu yako kwenye kompyuta inayotangamana na kebo ya USB.
2. Kwenye kidhibiti cha faili cha kompyuta yako, kokota au dondosha nyimbo na video zako
kwenye simu yako.
Fuatilia muda – jifunze jinsi ya kusasisha miadi, kazi, na ratiba zako.
Dhibiti kalenda
1. Gusa Kalenda .
2. Gusa .
3. Kagua kalenda unazotaka kuona. Geuza kalenda yako kukufaa ili kufaa mahitaji yako. Gusa
Mipangilio ili upate njia badala zaidi.
Kalenda huongezwa kiotomatiki wakati unapoongeza akaunti kwenye simu yako. Ili kuongeza
akaunti mpya na kalenda, gusa Mipangilio > Akaunti > Ongeza akaunti .
Ongeza tukio
Ili kukumbuka miadi au tukio, iongeze kwenye kalenda yako.
1. Katika Kalenda , gusa na uchague aina ya ingizo.
2. Charaza maelezo unayotaka, na uweke saa.
3. Ili kufanya tukio lijirudie siku fulani, gusa Chaguo zaidi > Isijirudie , na uchague ni mara
ngapi tukio linapaswa kujirudia.
4. Ili kuhariri muda wa ukumbusho, gusa muda unaosalia, na uchague muda unaotaka.
Dokezo: Ili kuhariri tukio, gusa tukio na , na uhariri maelezo.
Ramani za Google hukusaidia kupata maeneo na biashara mahsusi.
1. Gusa Ramani .
2. Andika maneno ya kutafuta, kama vile anwani ya mtaa au jina la mahali, katika upau wa
utafutaji.
3. Chagua kipengee kwenye orodha ya matokeo yanayopendekezwa unapokuwa ukiandika, au
gusa ili kutafuta.
Eneo huonyeshwa kwenye ramani. Ikiwa hakuna matokeo ya utafutaji yatakayopatikana,
hakikisha tahajia ya maneno yako ya utafutaji ni sahihi.
Angalia eneo lako la sasa
Gusa Ramani > .
Tafuta mikahawa na maeneo mengine yanayovutia karibu nawe
Gusa Ramani na upau wa utafutaji, na uchague kategoria
Pata maelekezo ya mahali
Pata maelezo ya kutembea, kuendesha gari, au kutumia uchukuzi wa umma - tumia eneo lako la
sasa au eneo lingine kama mahali pa kuanzia.
1. Gusa Ramani . Ingiza eneo unalotaka kupata maelekezo kwenye upau wa utafutaji.
2. Gusa Maelekezo . Aikoni kwenye mviringo huwakilisha hali ya uchukuzi. Hali msingi ya
mwelekeo ni gari . Kama unataka maelekezo ya kutembea au ya uchukuzi wa umma,
chagua hali chini ya upau wa utafutaji.
3. Kama hutaki mahali pa kuanza kuwa eneo lako la sasa, gusa Eneo lako , na utafute mahali pa
kuanza.
4. Gusa ANZA ili kuanza urambazaji.
Njia huonyeshwa kwenye ramani, pamoja na makadirio ya muda unaochukua kufika hapo. Ili
kuona maelekezo tondoti, pitisha juu kuanzia chini ya skrini kwa maelezo.
Ramani za nje ya mtandao > na ubadilishe Sasisha ramani za nje ya mtandao kiotomatiki
na Pakua ramani za nje ya mtandao kiotomatiki kwa Washa .
Futa ramani
1. Gusa Ramani > > Ramani za nje ya mtandao na jina la ramani.
2. Gusa FUTA .
TUMIA HUDUMA ZA ENEO
Tumia Ramani ili kujua uko wapi, na ambatisha eneo lako kwenye picha unazopiga. Maelezo ya
eneo yanaweza kuambatishwa kwenye picha au video, kama eneo lako linaweza kubainishwa
kwa kutumia teknolojia ya mtandao. Ukishiriki picha au video ambayo ina maelezo ya eneo,
maelezo ya eneo yanaweza kuonyeshwa kwa wale wanaotazama picha au video. Baadhi ya
programu zinaweza kutumia maelezo yako ya maeneo ili kutoa huduma mbalimbali.
Washa huduma za maeneo
Picha yako huonyesha eneo lako kwenye ramani kwa kutumia mfumo wa mkao wa setileti,
Wi-Fi, au mkao wa mtandao (Cell ID). Upatikanaji, usahihi na ukamilifu wa maelezo ya eneo
hutegemea, kwa mfano, eneo lako, maeneo ya karibu, na vyanzo vya mhusika mwingine, na
huenda ukazuiwa. Huenda maelezo ya eneo yasipatikane, kwa mfano, ndani ya majengo au
chini ya ardhi. Huduma ya mtandao ya GPS Iliyosaidiwa (A-GPS) na maboresho mengine sawa
na GPS na maeneo ya kuepua eneo la GLONASS kwa kutumia mtandao wa simu, na inasaidia
katika kuhesabu mahali pako pa sasa. Baadhi ya mifumo ya mkao wa setilaiti inaweza kuhitaji
uhamishaji wa viwango vidogo vya data kwenye mtandao wa simu. Kama unataka kuepuka
gharama ya data, kwa mfano wakati unasafiri, unaweza kuzima muunganisho wa data ya simu
katika mipangilio ya simu yako. Mkao wa Wi-Fi huboresha usahihi wa mkao wakati mawimbi ya
setileti hayapatikani, hasa wakati uko ndani au kati ya majengo marefu. Ukiwa uko katika mahali
matumizi ya Wi-Fi yamekatazwa, unaweza kuzima Wi-Fi katika mipangilio ya simu yako.
Gusa Mipangilio > gusa Eneo na ubadilishe kwa Washa Eneo .
Simu yako ya Android inaweza kutumika kikamilifu kwa kutumia Google Play – programu,
muziki, filamu na vitabu vinapatikana zote uweze kuzifurahia. Unachohitaji ni akaunti ya Google.
Ongeza akaunti ya Google kwenye simu yako
1. Gusa Mipangilio > Akaunti > Ongeza akaunti > Google . Ukiulizwa, thibitisha mbinu ya
kufunga kifaa chako.
2. Andika hati tambulishi za akaunti yako ya Google na uguse Inayofuata , au gusa
Au unda akaunti mpya .
3. Fuata maagizo kwenye simu yako.
Pakua programu
Fungua uwezo wa simu yako – kuna maelfu ya programu zinazosubiri katika Duka la Google Play
ya kukusaidia na hii.
1. Gusa Play Store .
2. Gusa upau wa utafutaji ili utafute programu, au chagua programu kutoka kwenye
mapendekezo yako.
3. Katika ufafanuzi wa programu, gusa SAKINISHA ili upakue na usakinishe programu.
Ili kuona programu zako, nenda kwenye skrini ya mwanzo na utelezeshe juu kutoka chini ya
skrini.
Sasisha programu
Sasisha programu zako za Play Store ili upate vipengele vyote vipya na utatue hitilafu.
1
1. Gusa Play store > > Programu na michezo yangu ili uone visasisho vinavyopatikana.
2. Gusa programu yenye kisasisho na SASISHA .
Unaweza pia kusasisha programu zote mara moja. Katika Programu na michezo yangu , gusa
Gusa Play Store > > Programu na michezo yangu , chagua programu unayotaka kuondoa,
na uguse SANIDUA .
Pata muziki, filamu, au vitabu kwa kutumia Google Play
Ukiwa na Google Play, unaweza kupata mamilioni ya nyimbo, filamu, na vitabu.
Gusa Muziki , Filamu , au Vitabu ili kujifunza zaidi.
1
Unahitaji kuongeza akaunti ya Google kwenye simu yako ili utumie huduma za Google Play. Mabadiliko
yanaweza kutumika kwa baadhi ya maudhui yanayopatikana kwenye Google Play. Ili kuongeza mbinu
ya malipo, gusa Play Store > Menyu > Akaunti > Mbinu za malipo . Hakikisha kila wakati una kibali
kutoka kwa mmiliki wa mbinu ya malipo wakati unanunua maudhui kutoka Google Play.
Kuwa katika hali sawa na mdundo - sasisha programu ya simu yako pasi waya ili upate vipengee
vipya na vilivyoboreshwa vya simu yako. Kusasisha programu kunaweza pia kuboresha
utendakazi wa simu yako.
Sakinisha visasisho vinavyopatikana
Gusa Mipangilio > Kuhusu simu > Visasisho vya mfumo > Kagusa sasisho ili kukagua kama
visasisho vinapatikana.
Wakati simu yako inapokuarifu kwamba sasisho linapatikana, fuata maagizo yaliyoonyeshwa
kwenye simu yako. Ikiwa simu yako inaishiwa na kumbukumbu, huenda ukahitaji kusogeza
programu, picha na vitu vyako vingine kwenye kadi ya kumbukumbu.
Onyo: ukisakinisha kisasisho cha programu, huwezi kutumia kifaa hicho, hata kupiga simu za
dharura, mpaka usasishaji ukamilike na kifaa kiwashwe upya.
Kabla ya kuanza kusasisha, unganisha chaja ua hakikisha betri ya kifaa ina nishati ya kutosha,
na unganishe kwenye Wi-Fi, kwa kuwa vifurushi vya kusasisha vinaweza kutumia data nyingi ya
simu.
HIFADHI NAKALA YA DATA YAKO
Ili kuhakikisha data yako ni salama, tumia kipengele cha kuhifadhi nakala kwenye simu yako.
Data ya kifaa chako (kama vile manenosiri ya Wi-Fi na historia ya simu) na data ya simu (kama
mipangilio na faili zilizohifadhiwa na programu) zitahifadhiwa kwa umbali.
Washa kuhifadhi nakala kiotomatiki
1. Gusa Mipangilio > Hifadhi nakala na urejeshe mipangilio ya kiwanda
Hifadhi nakala ya data yangu kwa Washa .
2. Gusa Akaunti mbadala ili uchague ni akaunti gani data yako itahifadhiwa kwayo.
REJESHA MIPANGILIO HALISI NA UONDOE MAUDHUI BINAFSI KWENYE SIMU
YAKO
Ajali zinaweza kutokea - Ikiwa simu yako haifanyi kazi vizuri, unaweza kurejesha mipangilio
yake halisi. Au, ukinunua simu mpya, au uwe unataka kutupa au kuchakata upya simu yako, hivi
ndivyo unavyoweza kuondoa maelezo na maudhui yako ya kibinafsi. Kumbuka kwamba ni wajibu
wako kuondoa maudhui yote ya kibinafsi.
1. Gusa Mipangilio > Kuhifadhi nakala na kuweka upya > Uwekaji upya data ya kiwandani .
2. Fuata maagizo yaliyoonyeshwa kwenye simu yako.
HIFADHI
Tumia menyu ya Hifadhi ili ukague kiasi cha kumbukumbu unacho.
Kagua kumbukumbu inayopatikana kwenye simu yako
Ikiwa kumbukumbu ya simu inajaa, kwanza kagua na uondoe vitu usivyovihitaji tena:
• Maandishi, medianuwai, na ujumbe wa barua
• Ingizo na maelezo ya majina
• Programu
• Muziki, picha, au video
Badala ya kuondoa, unaweza pia kusogeza faili kwenye kadi ya kumbukumbu.
Ubora wa kadi ya kumbukumbu unaweza kuathiri utendakazi wa simu yako pakubwa. Ili uweze
kunufaika zaidi na simu yako, tumia kadi ya 4–128GB kutoka kwa mtengenezaji anayefahamika.
Tumia tu kadi za kumbukumbu zinazotangamana zilizoidhinishwa kutumiwa na kifaa hiki. Kadi
zisizotangamana zinaweza kuharibu kadi na kifaa na kuharibu data iliyohifadhiwa kwenye kadi.
Ili kukagua kiasi cha kumbukumbu unacho na jinsi inavyotumika, gusa Mipangilio > Hifadhi .
Ondoa programu zilizopakuliwa
Gusa Play Store > > Programu na michezo yangu , chagua programu unayotaka kuondoa,
na uguse SANIDUA .
Zima programu
Huwezi kufuta baadhi ya programu ambazo zilisakinishwa mapema kwenye kifaa chako. Lakini
unaweza kuzilemaza na zitafichwa kutoka kwenye orodha ya programu kwenye kifaa chako.
Ukilemaza programu, unaweza kuiongeza kwenye kifaa chako.
3. Gusa LEMAZA . Huenda usiweze kulemaza programu zote.
Ikiwa programu iliyosakinishwa inategemea programu iliyotolewa, programu iliyosakinishwa
inaweza koma kufanya kazi. Kwa maelezo, angalia nyaraka za mtumiaji kwenye programu
iliyosakinishwa.
Rejesha programu iliyolemazwa
Unaweza kuongeza programu iliyolemazwa kwenye orodha ya programu.
1. Gusa Mipangilio > Programu .
2. Gusa Mipangilio yote > Imelemazwa .
3. Gusa jina la programu.
4. Gusa WEZESHA .
Nakili maudhui kati ya simu yako na kompyuta
Unaweza kunakili picha, video, na maudhui mengine yaliyoundwa na wewe kati ya simu na
kompyuta yako ili kuonyesha au kuzihifadhi.
1. Unganisha simu yako kwenye kompyuta inayotangamana na kebo ya USB inayotangamana.
2. Kwenye kompyuta yako, fungua kisimamia faili, na uvinjari kwenye simu yako.
3. Kokota na udondoshe vipengee kutoka kwenye simu hadi kompyuta yako, au kutoka kwenye
kompyuta hadi simu yako.
Hakikisha umeweka faili katika folda sahihi kwenye simu yako, au huenda usiweze kuziona.
Unaweza kuweka simu yako kuhitaji uhalalishaji wakati unapofungua skrini.
Weka kufuli ya skrini
1. Gusa Mipangilio > Usalama > Kufuli ya skrini .
2. Gusa Funga skrini ili uchague aina ya saa na ufuate maagizo kwenye simu yako.
BADILISHA MSIMBO WAKO WA PIN YA SIM
Ikiwa SIM kadi yako ilikuja na msimbo msingi wa PIN ya SIM, unaweza kuibadilisha ili kuwa
salama zaidi. Sio watoa huduma wote wa mtandao wanakubali hii.
Chagua PIN ya SIM yako
Unaweza kuchagua nambari zako mwenyewe za PIN ya SIM. Msimbo wa PIN ya SIM unaweza
kuwa wa dijiti 4-8.
2. Chini ya kadi iliyoteuliwa ya SIM, gusa Badilisha nenosiri la kuzuia .
Dokezo: Kama hutaki kulinda SIM yako kwa msimbo wa PIN, katika Sanidi kufuli ya SIM kadi ,
badilisha Funga SIM kadi kwa Zima , na ucharaze PIN yako ya sasa.
MISIMBO YA UFIKIAJI
Jifunze misimbo tofauti kwenye simu yako ni ya nini.
Msimbo wa PIN au PIN2
Misimbo ya PIN au PIN2 ina dijiti 4-8.
Misimbo hii hulinda SIM kadi yako dhidi ya matumizi yasioidhinishwa au huhitajika ili kufikia
vipengee vingine. Unaweza kuweka simu yako kukuuliza msimbo wa PIN wakati unapoiwasha.
Ukisahau misimbo au iwe haijatolewa pamoja na kadi yako, wasiliana na mtoa huduma wa
mtandao wako.
Ukicharaza msimbo vibaya mara 3 zikifuatana, unahitaji kufungua msimbo kwa kutumia msimbo
wa PUK au PUK2.
Misimbo ya PUK au PUK2 zinahitajika ili kufungua msimbo wa PIN au PIN2.
Ikiwa misimbo haijatolewa na SIM kadi yako, wasiliana na mtoa huduma wako wa mtandao.
Msimbo wa kufunga
Msimbo wa kufunga unajulikana pia kama msimbo au nenosiri la usalama.
Msimbo wa kufunga hukusaidia kulinda simu yako dhidi ya matumizi yasiyoidhinishwa. Unaweza
kuweka simu yako kukuuliza msimbo wa kufunga ambao unafasili. Weka msimbo kuwa siri na
mahali salama, kando na simu yako.
Ukisahau msimbo na simu yako imefungwa, simu yako itahitaji huduma. Huenda gharama ya
ziada ikatumika, na data yote ya kibinafsi kwenye simu huenda ikafutwa. Kwa maelezo zaidi,
wasiliana na kituo cha huduma kilichoidhinishwa kilicho karibu cha simu yako, au muuzaji wa
simu yako.
Msimbo wa IMEI
Msimbo wa IMEI hutumiwa kutambua simu katika mtandao. Huenda pia ukahitaji kupeana
nambari kwa kituo chako kilichoidhinishwa cha huduma au muuzaji wa simu.
Ili kuona nambari yako ya IMEI, piga *#06# .
Msimbo wa IMEI wa simu yako umechapishwa pia kwenye simu yako au kwenye trei ya SIM
kulingana na modeli ya simu yako. Ikiwa simu yako ina kifuniko kinachoweza kuondolewa cha
nyuma, unaweza kupata msimbo wa IMEI chini ya kifuniko.
IMEI inaweza kuonekana pia kwenye kisanduku halisi cha mauzo.
Tafuta au funga simu yako
Ukipoteza simu yako, unaweza kuitafuta, kuifunga, au kuifuta kwa mbali ikiwa umeingia kwenye
Akaunti ya Google. Tafuta Kifaa Changu huwashwa kimsingi kwa simu zinazohusishwa na
Akaunti ya Google.
Ili utumie Tafuta Kifaa Changu, lazima simu yako iwe:
• Imewashwa
• Umeingia kwenye Akaunti ya Google
• Imeunganishwa kwenye data ya simu au
Wi-Fi
Wakati Tafuta Kifaa Changu kinapounganishwa na simu yako, utaona eneo la simu, na simu
itapata arifa.
1. Fungua android.com/find kwenye kompyuta, kompyuta kibao au simu iliyounganishwa
kwenye intaneti na uingie kwenye Akaunti yako ya Google.
2. Ikiwa una zaidi ya simu moja, bofya simu iliyopotea juu ya skrini.
3. Kwenye ramani, angalia kuhusu mahali simu iko. Eneo huwa ukadiriaji na huenda lisiwe
sahihi.
Iwapo kifaa chako hakiwezi kupatikana, Tafuta Kifaa Changu itaonyesha eneo la mwisho
linalojulikana, ikiwa ipo. Ili kufunga au kufuta simu yako, fuata maagizo kwenye tovuti.
Soma maelekezo haya rahisi. Kutoyafuata kunaweza kuwa hatari au kinyume cha sheria na
masharti. Kwa maelezo zaidi, soma mwongozo kamili wa mtumiaji.
ZIMA KATIKA MAENEO YALIYOKATAZWA
Zima kifaa wakati matumizi ya kifaa cha mkononi yamekatazwa au wakati yanaweza
kusababisha mwingiliano au hatari, kwa mfano, ndani ya ndege au hospitalini, au karibu na vifaa
vya matibabu, mafuta, kemikali, au maeneo yenye mlipuko. Tii maagizo yote katika maeneo
yaliyozuiwa.
USALAMA BARABARANI HUJA KWANZA
Tii sheria zote za mahali ulipo. Daima iache mikono yako iwe huru kuendesha gari. Kitu cha
kuzingatia kwanza unapoendesha gari unapaswa kuwa usalama barabarani.
Vifaa vyote visivyotumia waya vina uwezekano wa kupata mwingiliano, ambao unaweza kuathiri
utendaji kazi wake.
HUDUMU ILIYOIDHINISHWA
Watu walioidhinishwa tu ndio wanaweza kuweka au kukarabati bidhaa hii.
BETRI, CHAJA, NA VIFAA VINGINE VYA ZIADA
Tumia betri, chaja, na vifaa vya ziada ambavyo vimeidhinishwa na HMD Global Oy kwa ajili ya
matumizi na kifaa hiki tu. Usiunganishe bidhaa ambazo hazitangamani.
WEKA KIFAA KIKIWA KIKAVU
Ikiwa kifaa chako kinazuia maji, angalia ukadiriaji wake wa IP katika ainisho za kiufundi za kifaa
kwa maelekezo zaidi tondoti.
Kifaa na/au skrini yake imetengenezwa kwa glasi. Glasi hii inaweza kuvunjika kifaa kikiangushwa
mahali pagumu au kupokea mgongano mzito. Glasi ikivunjika, usiguse sehemu za glasi za kifaa
au ujaribu kuondoa glasi iliyovunjika kutoka kwa kifaa. Acha kutumia kifaa hadi glasi ibadilishwe
na mhudumu aliyeidhinishwa.
LINDA UWEZO WAKO WA KUSIKIA
Kuzuia madhara yanayowezekana ya kusikia, usisikilize katika viwango vya juu vya sauti kwa
muda mrefu. Kuwa mwangalifu wakati unashikilia kifaa chako karibu na sikio wakati kipaza sauti
kinatumika.
SAR
Kifaa hiki kinatimiza matakwa ya maelekezo ya ujiwekaji wazi kwa frikwensi za redio wakati
kikitumika ama kwenye mkao wa kawaida kwenye sikio au wakati kikiwekwa angalau sentimita
1.5 (inchi 5/8) kutoka kwenye mwili. Thamani maalum za juu za SAR zinaweza kupatikana
katika sehemu ya Maelezo ya Cheti ya (SAR) ya mwongozo huu wa mtumiaji. Kwa maelezo zaidi,
angalia sehemu ya Maelezo ya Cheti (SAR) ya mwongozu huu wa mtumiaji au nenda kwenye
Kutumia baadhi ya vipengele na huduma, au kupakia maudhui, pamoja na vipengee
visivyolipishwa, uhitaji muunganisho wa mtandao. Hii huenda ikasababisha uhamishaji wa
viwango vikubwa vya data, ambayo inaweza kusababisha gharama ya data. Huenda pia
ukahitajika kujisajili kwa baadhi ya vipengele.
Muhimu: Huenda 4G/LTE isikubaliwe na mtoa huduma wa mtandao wako au na mtoa huduma
unayemtumia wakati unasafiri. Katika hali hizi, huenda usiweze kupiga au kupokea simu,
kutuma au kupokea ujumbe au kutumia miunganisho ya data ya simu. Ili kuhakikisha kifaa
chako kinafanya kazi vizuri wakati huduma ya 4G/LTE haipatikani, inapendekezwa kwamba
ubadilishe kasi ya juu zaidi ya muunganisho kutoka 4G hadi 3G. Ili kufanya hivi, kwenye
skrini ya mwanzo, gusa Mipangilio > Zaidi > Mitandao ya simu za mkononi , na ubadilishe
Aina ya mtandao unaopendelewa kwa 2G/3G .
_Kumbuka:_Kutumia Wi-Fi huenda kumezuiwa katika nchi zingine. Kwa mfano, katika Ulaya,
unaruhusiwa tu kutumia 5150-5350 MHz Wi-Fi ukiwa ndani tu, na nchini Marekani na Kanada,
unaruhusiwa kutumia 5.15-5.25 GHz Wi-Fi ukiwa ndani tu. Kwa maelezo zaidi, wasiliana na
utawala wa eneo lako.
Kwa maelezo zaidi, wasiliana na mtoa huduma wako wa mtandao.
SIMU ZA DHARURA
Muhimu: Miunganisho katika hali zote haiwezi kuhakikishwa. Kamwe usitegemee tu simu
pasiwaya kwa mawasiliano muhimu kama vile tiba za dharura.
Kabla ya kupiga simu:
• Washa simu.
• Kama skrini na vitufe vya simu vimefungwa, vifungue.
• Nenda eneo lenye mawimbi ya simu ya kutosha.
Kwenye skrini ya mwanzo, gusa .
1. Charaza namba rasmi ya dharura ya eneo lako la sasa. Nambari za simu ya dharura
hutofautiana kimaeneo.
2. Gusa .
3. Toa maelezo yanayofaa kwa usahihi kama iwezekanavyo. Usikate simu hadi upewe ruhusa ya
kufanya hivyo.
Huenda pia ukahitajika kufanya yafuatayo:
• Weka SIM kadi ndani ya simu. Ikiwa huna SIM kadi, kwenye skrini ya kufunga, gusa Dharura .
• Ikiwa simu yako itakuuliza msimbo wa PIN, gusa Dharura .
• Zima vizuizi vya simu katika simu yako, kama vile uzuiaji simu, upigaji uliopangwa, au kikundi
maalum cha watumiaji.
• Ikiwa mtandao wa simu haupatikani, unaweza pia kujaribu kupiga simu ya intaneti, ikiwa
unaweza kufikia intaneti.
KUHUDUMIA KIFAA CHAKO
Shughulikia kifaa chako, betri, chaja na vifaa vya ziada kwa uangalifu. Mapendekezo yafuatayo
yatakusaidia kufanya kifaa chako kifanye kazi.
• Weka kifaa kikiwa kikavu. Taka za
mtuamo, unyevu wa hewa, na aina zote
za vimiminiko au unyevu zinaweza kuwa
na madini yanayoweza kutia kutu saketi za
elektroniki.
• Usitumie au kuhifadhi kifaa chako kwenye
maeneo yenye vumbi au uchafu.
• Usihifadhi kifaa kwenye halijoto ya juu au
ya chini. Halijoto ya juu huenda ikaharibu
kifaa au betri.
• Usihifadhi kifaa kwenye halijoto baridi.
Wakati kifaa kimerudi kwenye joto
lake la kawaida, unyevunyevu unaweza
kutengenezeka ndani ya kifaa.
• Usifungue kifaa kando na ilivyoagizwa
katika kiongozi cha mtumiaji.
• Mabadiliko yasioidhinishwa yanaweza
kuharibu kifaa hiki na kukiuka sheria
zinazosimamia vifaa vya redio.
• Usiangushe, kugonga, au kutingisa kifaa
au betri. Kukishika kiholela kunaweza
kuivunja.
• Tumia kitambaa laini, kisafi na kikavu
kusafisha uso wa kifaa hiki.
• Usipake rangi kifaa. Rangi inaweza kuzuia
utendaji kazi wa kawaida.
• Weka kifaa chako mbali na sumaku au
maeneo ya sumaku.
• Ili kuweka data yako muhimu salama,
ihifadhi angalau katika maeneo mawili
tofauti, kama vile kifaa chako, kadi ya
kumbukumbu, au kompyuta au andika
maelezo muhimu.
Wakati wa utendajikazi kwa muda mrefu, kifaa kinaweza kuwa na joto. Katika hali nyingi, hii
ni kawaida. Kuepuka kupata joto sana, huenda kifaa kikapunguza kasi kiotomatiki, kikafunga
programu, kikazima kuchaji, na ikiwezekana, kikajizima. Kama kifaa hakifanyi kazi sawasawa,
kipeleke kwenye kitengo cha mtengenezaji aliyeidhinishwa kilicho karibu.
Daima rudisha bidhaa zako za elektroniki, betri na nyezo za kifurushi zilizotumiwa kwa maeneo
maalum ya ukusanyaji. Kwa njia hii utasaidia kuzuia utupaji taka usiodhibitiwa na kukuza
uchakataji upya wa nyenzo. Bidhaa za umeme na elektroniki huwa na nyenzo nyingi za thamani,
ikiwa ni pamoja na madini (kama vile shaba, aluminiamu, chuma, na magnesiamu) na madini ya
thamani (kama vile dhahabu, fedha, na paladiamu) Nyenzo zote za kifaa zinaweza kufufuliwa
kama nyenzo na nishati.
ALAMA YA PIPA ILIYO NA MKATO
Alama ya pipa iliyo na mkato
Alama ya pipa iliyo na mkato kwenye bidhaa, betri, maandishi, au kifurushi chako
hukukumbusha kwamba bidhaa zote za elektroniki na betri lazima zipelekwe kwenye
mkusanyiko tofauti wakati bidhaa inapokwisha. Usitupe bidhaa hizi kama takataka
zisizochambuliwa za manispaa: zipeleke zichakatwe. Kwa maelezo juu ya eneo la uchakataji lililo
karibu na wewe, wasiliana na mamlaka ya taka ya eneo lako.
MAELEZO YA BETRI NA CHAJA
Maelezo ya betri na chaja
Ili ukague ikiwa simu yako ina betri inayoweza kuondolewa au isiyoweza kuondolewa, angalia
Mwongozo wa kuanza kutumia.
Vifaa vilivyo na beti inayoweza kuondolewa Tumia kifaa chako na betri halisi tu inayoweza
kuchajiwa upya. Betri inaweza kuchajiwa na kuondolewa chaji hata mara mia, lakini hatimaye
itachoka. Wakati muda wa kuongea na muda wa kusubiri unaonekana wazi kuwa mfupi kuliko
kawaida, badilisha betri.
Vifaa vilivyo na betri isiyoweza kuondolewa Usijaribu kuitoa betri, kwa sababu unaweza
kuharibu kifaa. Betri inaweza kuchajiwa na kuondolewa chaji hata mara mia, lakini hatimaye
itachoka. Wakati muda wa kuongea na muda wa kusubiri unaonekana wazi kuwa mfupi kuliko
kawaida, kubadilisha betri, peleka kifaa hicho kwenye kitengo cha mtengenezaji aliyeidhinishwa
kilicho karibu.
Chaji kifaa chako na chapa inayotangamana. Aina ya plagi ya chaja huenda ikatofautiana. Muda
wa kuchaji unaweza kutofautiana kulingana na uwezo wa kifaa.
Kifaa chako kikikamiliza kuchajiwa, chomoa chaja kutoka kwenye kifaa na soketi ya umeme.
Tafadhali kumbuka kwamba kuchaji kwa mfululizo hakupaswi kuzidi saa 12. Ikiachwa bila
kutumika, betri iliyokuwa imejaa chaji itapoteza chaji yake kadri muda unavyopita.
Halijoto ya juu sana hupunguza uwezo na maisha ya betri. Daima jaribu kuweka betri kwenye
halijoto kati ya 15°C na 25°C (59°F na 77°F) kwa utendakazi bora. Kifaa chenye betri moto au
baridi kinaweza kisifanye kazi kwa muda. Kumbuka kwamba huenda betri ikaisha haraka katika
halijoto baridi na kupoteza nishati ya kutosha na kuzima simu katika dakika chache. Ukiwa nje
katika halijoto baridi, weka simu yako ikiwa na joto kiasi.
Tii sheria za eneo lako. Peleka ichakatwe upya ikiwezekana. Usitupe kama takataka za kawaida
za nyumbani.
Usiweke betri kwenye shinikizo la chini sana la hewa au kuiwacha kwenye halijoto ya juu sana,
kwa mfano kuitupa kwenye moto, kwa kuwa hiyo inaweza kusababisha betri kulipuka au kuvuja
kiowevu au gesi inayoweza kuwaka moto.
Usifungue, kukata, kuvunja, kukunja, kutoa, au kuharibu betri kwa njia yoyote ile. Kama betri
itavuja, usiruhusu umaji uguse ngozi au macho. Hii ikifanyika, osha maeneo yaliyoathirika mara
moja na maji, au tafuta msaada wa kitabibu. Usirekebishe, kujaribu kuingiza vitu vigeni kwenye
betri, au kuizamisha au kuiweka kwenye maji au aina nyingine ya umaji. Betri zinaweza kulipuka
kama zimeharibika.
Tumia betri na chaja kwa matumizi yaliyokusudiwa tu. Matumizi mabaya, au matumizi
yasiyoidhinishwa au yasiyotangamana na betri au chaja huenda yakaleta hatari ya moto,
mlipuko au hatari nyingine, na huenda ikabatilisha uhalali wowote ulioidhinishwa au waranti.
Kama unaamini betri au chaja imeharibika, ipeleke kwa kituo cha huduma au muuza simu
yako kabla ya kuendelea kuitumia. Kamwe usitumie betri au chaja yoyote iliyoharibika.
Tumia chaja ndani ya nyumba tu. Usichaji kifaa chako wakati wa dhoruba ya radi. Wakati
chaja haijajumuishwa katika furushi la mauzo, chaji kifaa chako kwa kutumia kebo ya data
(iliyojumuishwa) na adapta ya nishati ya USB (inaweza kuuzwa kando). Unaweza kuchaji kifaa
chako na kebo za wahusika wengine na adapta za nishati ambazo zinatangamana na USB 2.0
au baadaye na kanuni husika za nchi na viwango vya usalama vya kimataifa na mkoa. Huenda
adapta nyingine zisitimize viwango husika vya usalama, na kuchaji kwa kutumia adapta hizo
kunaweza kusababisha hatari ya kupoteza mali au majeraha ya kibinafsi.
Ili kuchopoa chaja au kifaa chochote cha ziada, kamata na uvute plagi na siyo waya.
Kwa kuongezea, zifuatazo hutumika ikiwa kifaa chako kina betri inayoweza kuondolewa:
• Daima zima na ung’oe chaja kabla ya kuondoa betri.
• Mkato wa umeme wa bahati mbaya unaweza kutokea kwa bahati mbaya kama kitu cha
chuma kitagusa vipapi vya chuma kwenye betri. Huenda hii ikaharibu betri au kifaa kile
kingine.
WATOTO WADOGO
Kifaa chako na viboreshaji vyake sio sesere. Vinaweza kuwa na sehemu ndogo ndogo. Viweke
mbali na watoto wadogo.
Utendajikazi wa kifaa cha kupitisha mawimbi ya redio, pamoja na simu zisizotumia waya, huenda
zikaingiliana na utendaji wa vifaa vya matibabu visivyokingwa vizuri. Wasiliana na daktari au
mtengenezaji wa kifaa cha matibabu ili ubainishe kama kimekingwa vizuri dhidi ya nguvu ya nje
ya radio.
VIFAA VYA MATIBABU VINAVYOPACHIKWA
Kuepuka mwingiliano unaowezekana, watengenezaji wa vifaa vilivyopachikwa vya matibabu
(kama vile vipima mapigo ya moyo, pampu za insulini, na yurostimuleta wanapendekeza nafasi
isiyopungua sentimita 15.3 (inchi 6) kati ya kifaa kisichotumia waya na kifaa cha matibabu.
Watu ambao wana vifaa kama hivyo wanapaswa:
• Daima weka kifaa kisichotumia waya kwa
umbali wa sentimita 15.3 (inchi 6) kutoka
kwa kifaa cha matibabu.
• Usibebe kifaa pasiwaya katika mfuko wa
shati.
• Shikilia kifaa pasiwaya kwenye sikio kando
Ikiwa una maswali yoyote kuhusu kutumia kifaa chako pasiwaya na kifaa cha matibabu
kilichopachikwa, wasiliana na mtoa huduma wako wa afya.
na kifaa cha matibabu.
• Zima kifaa pasiwaya kama kuna sababu
yoyote ya kushuku kwamba mwingiliano
unafanyika.
• Fuata maagizo ya mtengeneza kifaa cha
matibabu kilichopachikwa.
VIFAA VYA KUSAIDIA KUSIKIA
Onyo: Wakati unatumia vifaa vya sauti, uwezo wako wa kusikiliza sauti za nje unaweza
kuathirika. Usitumie vifaa vya sauti mahali ambapo kinaweza kuhatarisha usalama wako.
Baadhi ya vifaa pasiwaya vinaweza kuingiliana na baadhi ya vifaa vya kusaidia kusikia.
LINDA MTOTO WAKO DHIDI YA VITU VYENYE MADHARA
Kifaa chako kinaweza kupata virusi na vitu vingine vyenye madhara. Chukua tahadhari
zifuatazo:
• Kuwa mwangalifu wakati wa kufungua
ujumbe. Huenda zikawa na programu
mbaya au yenye kudhuru kifaa au
kompyuta yako.
• Kuwa mwangalifu wakati unakubali maombi
ya muunganisho, unapovinjari tovuti, au
kupakua yaliyomo. Usikubali miunganisho
ya Bluetooth kutoka kwenye vyanzo
usivyoviamini.
• Sakinisha na tumia huduma na programu
kutoka vyanzo ambavyo unaviamini tu na
ambavyo vinatoa usalama na ulinzi.
Nokia 6 Mwongozo wa mtumiaji
• Sakinisha kizuia virusi na programu
zingine za usalama kwenye kifaa chako
na kompyuta yoyote iliyounganishwa.
Tumia tu programu moja ya kinga virusi
kwa wakati mmoja. Kutumia zaidi ya moja
huenda kukaathiri utendakazi na utumizi
wa kifaa na/au kompyuta.
• Ikiwa unafikia vialamisho vilivyosakinishwa
mapema na viungo kwa tovuti vya mhusika
wa tatu, chukua tahadhari zinazohitajika.
HMD Global haiidhinishi wala kuwajibika
kwa tovuti hizo.
MAGARI
Huenda mawimbi ya redio yakaathiri vibaya mifumo ya elektroniki iliyowekwa vibaya au
isiyokingwa vizuri katika magari. Kwa maelezo zaidi, wasiliana na mtengeneza gari lako au vifaa
vyake. Watu walioidhinishwa tu ndio wanapaswa kuweka kifaa ndani ya gari. Usakinishaji wenye
kasoro huenda wa hatari na ukabatilisha waranti yako. Hakikisha mara kwa mara kwamba vifaa
vyote visivyotumia waya ndani ya gari vimefungwa vizuri na vinafanya kazi sawasawa. Usihifadhi
au kubeba vifaa vinavyoweza kuchomeka au kulipuka katika eneo sawa kama kifaa, sehemu
zake, au vifaa vya ziada. Usiweke kifaa chako au viboreshaji kwenye eneo ambalo mfuko wa
hewa hutumika.
MAZINGIRA YANAYOWEZA KULIPUKA
Zima kifaa chako katika eneo lolote lenya mazingira yanayoweza kulipika, kama vile karibu na
pampu za mafuta katika vituo vya mafuta. Cheche zinaweza kusababisha mlipuko au moto
unaoweza kuleta majeraha au kifo. Kumbuka vikwazo katika maeneo yenye mafuta; viwanda
vya kemikali; au mahali ambapo shughuli za ulipuaji zinaendelea kufanyika. Maeneo yenye
mazingira yenye uwezekano wa milipuko yanaweza kuwa na alama zisizo dhahiri. Haya kwa
kawaida ni maeneo ambapo unaweza kushauriwa kuzima injini yako, chini ya sitaha kwenye boti,
uhamishaji kemikali au suhula za kuhifadhi, na ambapo hewa ina kemikali au chembechembe
kama vile nafaka, vumbi au poda ya chuma. Wasiliana na watengenezaji wa magari yanayotumia
mafuta aina ya gesi oevu ya petroli iliyoyeyushwa (kama vile propeni au buteni) ikiwa kifaa hiki
kinaweza kutumiwa vizuri katika maeneo yao.
HABARI YA UTOAJI CHETI (SAR)
Kifaa hiki cha mkononi kinatimiza maelekezo yanayohusu ujiwekaji wazi kwa mawimbi ya
redio.
Kifaa chako cha mkononi ni transmita na kipokezi cha redio. Kimeundwa kutozidi kikomo cha
ufichuzi kwa mawimbi ya redio (nyuga za sumaku za masafa ya redio), yanayopendekezwa
na maelekezo ya kimataifa kutoka kwa shirika huru la kisanyansi ICNIRP. Maelekezo haya
yanajumuisha viwango vya tahadhari ya ziada iliyowekwa kuhakikisha usalama wa watu wote,
bila kujali umri wala afya. Maelekezo ya ufichuzi yanategemea Kiwango Maalum cha Ufyonzaji
(SAR), ambacho ni onyesho la nguvu za kiwango cha masafa ya redio (RF) zinazowekwa kichwani
au mwilini wakati kifaa kinapitisha. Kikomo cha ICNIRP SAR kwa vifaa vya mkononi ni 2.0
wati/kilogramu (W/kg) kilichotokana na wastani wa gramu 10 za tishu.
Vipimo vya SAR hutekelezwa na kifaa katika mikao wastani ya matumizi, kwa hivyo kupitisha
kwa kiwango chake cha juu zaidi kilichoidhinishwa, katika bendi zake zote za masafa.
Tafadhali rejelea www.nokia.com/phones/sar for the maximum SAR value of the device.
Kifaa hiki kinatimiza matakwa ya maelekezo ya ujiwekaji wazi wa RF wakati kinatumiwa karibu
na kichwa au kikiwekwa angalau inchi 5/8 (sentimita 1.5) mbali na mwili. Wakati kikasha cha
kubebea, kishikiza kwenye mkanda au aina nyingi ya kishikizi kikitumika kwa matumizi ya
kuvaliwa mwilini, kinatakiwa kisiwe na chuma na kinatakiwa kuweka angalia umbali uliotajwa
hapo juu kutoka kwenye mwili.
Kutuma data au ujumbe, muunganisho salama wa mtandao unahitajika. Utumaji unaweza
kucheleweshwa hadi muunganisho huo upatikane. Fuata maagizo ya umbali wa kutenganisha
hadi utumaji ukamilike.
Wakati wa matumizi ya kawaida, thamani za SAR kwa kawaida huwa chini ya thamani zilizotajwa
hapa juu. Hii ni kwa sababu, kwa malengo ya ubora wa mfumo na kupunguza mwingiliano
kwenye mtandao, nguvu ya kufanya kazi ya kifaa chako cha mkononi hupunguzwa kiotomati
wakati nguvu kamili haihitajiki kwa simu. Nguvu towe inavyoendelea kuwa chini, ndivyo thamani
ya SAR inavyokuwa chini.
Huenda modeli za vifaa zikawa na matoleo tofauti na zaidi ya thamani moja. Mabadiliko ya
vijenzi na muundo yanaweza kufanyika baada ya muda na baadhi ya mabadiliko yanaweza
kuathiri thamani za SAR.
Kwa maelezo zaidi, nenda kwenye www.sar-tick.com. Kumbuka kwamba vifaa vya mkononi
huenda vikapitisha hata kama hupigi simu.
Shirika la Afya Duniani (WHO) limesema kwamba maelezo ya sasa ya kisayansi hayaashirii
hitaji la tahadhari zozote maalum wakati wa kutumia vifaa vya mkononi. Ikiwa unavutiwa
na kupunguza ufichuzi wako, wanapendekeza upunguze matumizi yako au utumie kifaa
kisichotumia mikono ili kuweka kifaa mbali na kichwa na mwili wako. Kwa maelezo zaidi
na ufafanuzi na majadiliano kuhusu ufichuzi wa RF, nenda kwenye tovuti ya WHO kwenye
Unapokuwa ukitumia kifaa hiki, tii sheria zote na heshimu utamaduni wa wenyeji, uhuru binafsi
wa mtu na haki halali za wengine, ikiwemo hakimiliki. Kinga za hakimiliki zinaweza kukuzuia dhidi
ya kunakili, kurekebisha au kuhamisha picha, muziki na maudhui mengine.
HAKIMILIKI NA ILANI
Hakimiliki na ilani nyingine
Upatikanaji wa bidhaa, vipengele, programu na huduma huenda zikatofautiana kimaeneo. Kwa
maelezo zaidi, wasiliana na mchuuzi au mtoa huduma wako. Kifaa hiki kinaweza kuwa na bidhaa,
teknolojia au programu ambayo inaathiriwa na sheria na kanuni za usafirishaji nje ya nchi kutoka
Marekani na nchi nyingine. Uchepushaji kinyume na sheria ni marufuku.
Yaliyomo katika waraka huu yametolewa ”kama yalivyo”. Isipokuwa kama inatakiwa hivyo na
sheria husika, hakuna dhamana za aina yoyote, ama za moja kwa moja au zisizo bayana, pamoja
na, lakini isiyokomea hapo, dhamana zisizo bayana za uuzikaji wa kibiashara na ufaaji kwa
matumizi fulani, zinazotolewa kuhusiana na usahihi, uaminikaji au yaliyomo ndani ya waraka
huu. HMD Global ina haki ya kupitia na kusahihisha waraka huu au kuuondoa wakati wowote bila
kutoa taarifa kwanza.
Kwa kadiri inayohusiwa na sheria husika, hakuna wakati wowote ule HMD Global au wenye leseni
wake watawajibika kwa upotevu wowote wa data au mapato au uharibifu wowote ule, uwe
maalum, wa ajali, unatokana na, au usiokuwa wa moja kwa moja uliosababishwa.
Ni marufuku kutoa upya, kuhamisha au kusambaza sehemu ya yaliyomo au yote katika waraka
huu katika hali yoyote ile bila ya kupewa kwanza idhini ya kuandikwa kutoka kwa HMD Global.
HMD Global inaendesha sera ya kuendelea kubuni. HMD Global ina haki ya kufanya mabadiliko
na kuboresha bidhaa yake yoyote iliyoelezwa katika waraka huu bila kutoa taarifa kwanza.
HMD Global haitoi wakilishi wowote, waranti au kuwajibika kwa utendaji kazi, maudhui, au
usaidizi wa mtumiaji wa programu za mhusika wa tatu zilizotolewa na kifaa chako. Kwa kutumia
programu, unakubali kwamba programu imetolewa kama ilivyo.
Upakuaji wa ramani, michezo, muziki na video na upakiaji taswira na video huenda ukajumuisha
upitishaji wa viwango vikubwa vya data. Huenda mtoa huduma wako akatoza kwa upitishaji
data. Upatikanaji wa bidhaa, huduma na vipengele fulani unaweza zikatofautiana kimaeneo.
Tafadhali wasiliana na muuzaji wa eneo lako kwa maelezo zaidi na upatikanaji wa chaguo za
lugha.
Vipengele, utendakazi na ainisho nyingine za bidhaa zinaweza kutegemea mtandao na
hutegemea masharti, sheria, na gharama za ziada.
Hizi zote zinaweza kubadilika bila ilani.
HMD Global Oy ndio ina leseni ya kipekee ya chapa ya Nokia ya simu na kompyuta kibao. Nokia
ni alama ya biashara iliyosajiliwa ya Nokia Corporation.
Sera ya Faragha ya HMD Global, inapatikana kwenye http://www.nokia.com/phones/privacy,
hutumika kwa matumizi yako ya kifaa.
Qualcomm na Snapdragon ni alama za biashara za Qualcomm Incorporated, zilizosajiliwa
Marekani na nchi nyingine.
Android, Google na Google Play ni alama za biashara za Google Inc.
Alama nyingine zote za biashara ni rasilimali za wamiliki wake.