Muhimu: Kwa maelezo muhimu kuhusu matumizi salama ya kifaa na betri yako, soma maelezo
ya ”Kwa usalama wako” na ”Usalama wa Bidhaa” katika mwongozo uliochapishwa wa mtumiaji,
au kwenye www.nokia.com/support kabla utumie kifaa. Ili kujua jinsi ya kuanza kutumia kifaa
chako kipya, soma mwongozo uliochapishwa wa mtumiaji.
Sasisha simu yako na ukubali visasisho vinavyopatikana vya programu ili upate vipengee vipya
na vilivyoboreshwa vya simu yako. Kusasisha programu kunaweza pia kuboresha utendakazi wa
simu yako.
VITUFE NA SEHEMU
Simu yako
Mwongozo huu wa mtumiaji hutumika kwa modeli zifuatazo: TA-1205, TA-1216, TA-1207.
1. Mweko
2. Kamera
3. Kiunganisha kifaa cha sauti
4. Kisaidizi cha Google/Kitufe cha Utafutaji
wa Google*
Baadhi ya vifaa vya ziada vilivyotajwa katika mwongozo huu wa mtumiaji, kama vile chaja, kifaa
cha kichwa, au kebo ya data, huenda vikauzwa kando.
*Kisaidizi cha Google hakipatikani katika lugha na nchi zingine. Ambapo hakipatikani
Kisaidizi cha Google hubadilishwa kwa Utafutaji wa Google. Angalia upatikanaji katika
https://support.google.com/assistant.
Sehemu na viunganishaji, hali ya sumaku
Usiunganishe kwenye bidhaa ambazo zinaunda ishara ya kutoa, kwa kuwa hii inaweza kuharibu
kifaa. Usiunganishe chanzo chochote cha stima kwenye kiunganisha cha sauti. Ukiunganisha
kifaa chochote cha nje au vifaa vyovyote vya sauti kando na vile vilivyoidhinishwa kutumiwa na
kifaa hiki, Kiunganishi cha sauti, kuwa makini sana na viwango vya sauti.
Sehemu nyingine za kifaa hiki zina sumaku. Vitu vya chuma vinaweza kuvutwa na kifaa. Usiweke
kadi za mkopo au kadi nyingine zenye mkanda wa sumaku karibu na kifaa kwa kipindi cha muda
mrefu, kwa kuwa kadi hizo zinaweza kuharibika.
1. Weka kucha ya kidole chako katika nafasi kati ya kifuniko cha nyuma na skrini, funga kona
ya kifaa, kunja ili kufungua kifuniko cha nyuma, na ukiondoe. Ikiwa una ugumu wa kufungua
nyuma ya kifuniko, jaribu kuifungua kutoka kwenye kipenyo cha USB. Usitumie zana zozote,
kwa kuwa zinaweza kuharibu simu.
2. Telezesha nano-SIM kwenye kipenyo cha 1 na eneo la mguso likiangalia chini. Ikiwa una simu
ya SIM mbili, telezesha SIM ya pili kwenye kipenyo cha 2.
3. Ikiwa una kadi ya kumbukumbu ya microSD, telezesha kadi kwenye kipenyo cha kadi ya
kumbukumbu.
4. Rudisha kifuniko cha nyuma.
Tumia kadi halisi ya nano-SIM tu. Matumizi ya SIM kadi zisizotangamana huenda yakaharibu
kadi au kifaa, na huenda yakaharibu data iliyohifadhiwa kwenye kadi.
Tumia tu kadi za kumbukumbu zinazotangamana zilizoidhinishwa kutumiwa na kifaa hiki. Kadi
zisizotangamana zinaweza kuharibu kadi na kifaa na kuharibu data iliyohifadhiwa kwenye kadi.
Kidokezo: Ili kujua ikiwa simu yako inaweza kutumia SIM kadi 2, angalia lebo kwenye sanduku
la mauzo. Ikiwa kuna misimbo 2 ya IMEI kwenye lebo, una simu yenye SIM mbili.
Muhimu: Usiondoe kadi ya kumbukumbu wakati programu inaitumia. Kufanya hivyo kunaweza
kuharibu kadi ya kumbukumbu na kuharibu data iliyohifadhiwa kwenye kadi.
Kidokezo: Tumia kadi ya kumbukumbu ya microSD yenye kasi, na ya hadi GB 400 kutoka kwa
mtengenezaji anayefahamika.
CHAJI SIMU YAKO
Chaji betri
1. Chomeka chaja inayotangamana kwenye soketi ya ukuta.
2. Unganisha kebo kwenye simu yako.
Simu yako inakubali kebo ya USB ya micro-B. Pia unaweza kuchaji simu yako kutoka kwenye
kompyuta kwa kutumia kebo ya USB, lakini inaweza kuchukua muda mrefu zaidi.
Kama betri imeisha moto kabisa, huenda ikachukua dakika kadhaa kabla ya kiashiria chaji
kuonyeshwa.
2. Chagua ni data gani unayotaka irejeshwe kwenye simu yako mpya. Usawazishaji huanza
kiotomatiki punde simu yako inapounganishwa kwenye intaneti.
Rejesha mipangilio ya programu kutoka kwenye simu yako ya awali ya Android™
Ikiwa simu yako ya awali ilikuwa ya Android, na uhifadhi nakala ya akaunti ya Google kwayo,
unaweza kurejesha mipangilio ya programu yako na manenosiri ya Wi-Fi.
1. Gusa Mipangilio > Mfumo > Hifadhi nakala rudufu .
2. Badilisha Hifadhi nakala kwenye Google Drive kwa Washa .
MIPANGILIO YA SIM MBILI
Ikiwa una simu ya SIM mbili, unaweza kuwa na SIM 2 kwenye simu yako, kwa mfano, moja ya kazi
yako na nyingine ya matumizi yako ya kibinafsi.
Kwa mfano, wakati unapiga simu, unaweza kuchagua ni SIM gani ya kutumia kwa kugusa kitufe
kinacholingana cha SIM 1 au SIM 2 baada ya kupiga nambari hiyo.
Simu yako huonyesha hali ya mtandao ya SIM zako kitofauti. SIM kadi zote zinapatikana kwa
wakati mmoja wakati kifaa hakitumiki, lakini wakai SIM kadi moja inatumika, kwa mfano, wakati
wa kupiga simu, ile nyingine inawezakosa kupatikana.
Dhibiti SIM zako
Hutaki kazi iingiliane na muda wako huru? Au una muunganisho wa bei nafuu wa data kwenye
SIM moja? Unaweza kuamua ni SIM gani unayotaka kutumia.
Gusa Mipangilio > Mtandao na Intaneti > SIM Kadi .
Badili jina la SIM kadi
Gusa SIM unayotaka kubadilisha jina, na uandike jina unalotaka.
Chagua ni SIM gani ya kutumia kwa simu au muunganisho wa data
Chini ya SIM unayopendelea ya , gusa mpangilio unaotaka kubadilisha na uchague SIM.
FUNGA AU FUNGUA SIMU YAKO
Funga simu yako
Kiwa unataka kuepuka kupiga simu kwa makosa wakati simu yako iko kwenye mfuko au begi
lako, unaweza kufunga vitufe na skrini yako.
Ili kufunga vitufe na skrini yako, bonyeza kitufe cha nishati.
Fungua vitufe na skrini
Bonyeza kitufe cha nishati, na utelezeshe juu kwenye skrini. Ukiulizwa, toa hati tambulishi za
ziada.
TUMIA SKRINI YA MGUSO
Muhimu: Epuka kugwara skrini ya mguso. Usitumie kamwe kalamu, penseli halisi, au kitu
• IIi kwenda kwenye skrini ya mwanzo, gusa
kitufe cha mwanzo. Programu uliyokuwa
ukitumia hubakia imefunguliwa chinichini.
• Ili kuona ni programu gani ulizofungua,
gusa .
• Ili kubadilisha kwa programu nyingine
iliyofunguliwa, gusa programu.
• Ili kufunga programu zote zilizofunguliwa,
gusa Futa zote .
• Ili kurejesha kwenye skrini ya awali
uliyokuwa, gusa . simu yako hukumbuka
programu na tovuti zote ulizotembelea
tangu wakati wa mwisho skrini yako
ilipofungwa.
Gusa Mipangilio > Sauti > Mlio wa simu wa SIM1 au Mlio wa simu wa SIM2 , na uchague mlio.
Badilisha sauti ya taarifa ya ujumbe wako
Gusa Mipangilio > Sauti > Mipangilio ya kina > Sauti chaguo-msingi ya arifa .
ARIFA
Tumia paneli ya taarifa
Unapopokea arifa mpya, kama vile ujumbe au simu zisizojibiwa, aikoni ya kiashiriaji huonekana
kwenye upau wa hali juu ya skrini. Ili kuona maelezo zaidi kuhusu arifa, kokota chini upau wa
hali. Ili kufunga mwonekano, pitisha juu kwenye skrini.
Ili kufungua paneli ya arifa, kokota upau wa hali chini. Ili kufunga paneli ya arifa, pitisha juu
kwenye skrini.
Ili kubadilisha mipangilio ya taarifa ya programu, gusa Mipangilio > Programu na arifa > na
uguse jina la programu ili ufungue mipangilio ya programu. Gusa Arifa . Unaweza kuzima au
kuwasha arifa kwa kila programu kivyake.
Ili kuamilisha vipengele, gusa ikoni za mipangilio ya haraka kwenye paneli ya arifa. Ili kuona ikoni
zaidi, kokoa menyu chini.
Ili kupanga upya ikoni, gusa , gusa na ushikilie ikoni, na uikokote kwenye eneo lingine.
DHIBITI SAUTI
Badilisha sauti
Ikiwa una tatizo la kusikia simu yako ikiita katika mazingira yenye kelele, au simu ina sauti ya
juu, unaweza kubadilisha sauti kama upendavyo kwa kutumia vitufe vya sauti upande wa simu
yako.
Usiunganishe kwenye bidhaa ambazo zinaunda ishara ya kutoa, kwa kuwa hii inaweza kuharibu
kifaa. Usiunganishe chanzo chochote cha stima kwenye kiunganisha cha sauti. Ukiunganisha
kifaa chochote cha nje au vifaa vyovyote vya sauti kando na vile vilivyoidhinishwa kutumiwa na
kifaa hiki, Kiunganishi cha sauti, kuwa makini sana na viwango vya sauti.
Badilisha sauti ya midia na programu
Bonyeza kitufe cha sauti upande wa simu yako ili uone upau wa hali ya sauti, gusa , na
ukokote kitelezi kwenye upau wa sauti kwa midia na programu kushoto au kulia.
Weka simu kimya
Ili kuweka simu kuwa kimya, bonyeza kitufe cha kupunguza zaidi, gusa ili uweke simu yako
kutetema pekee na uguse ili kuiweka kimya.