Muhimu: Kwa maelezo muhimu kuhusu matumizi salama ya kifaa na betri yako, soma ”Kwa
usalama wako” na maelezo ya ”Usalama wa Bidhaa” katika mwongozo uliochapishwa wa
watumiaji, au kwenye www.nokia.com/support kabla uanze kutumia kifaa. Ili kujua jinsi ya
kuanza kutumia kifaa chako kipya, soma mwongozo uliochapishwa wa watumiaji.
Usiunganishe kwenye bidhaa ambazo zinaunda ishara ya kutoa, kwa kuwa hii inaweza kuharibu
kifaa. Usiunganishe chanzo chochote cha stima kwenye kiunganisha cha sauti. Ukiunganisha
kifaa chochote cha nje au vifaa vyovyote vya sauti kando na vile vilivyoidhinishwa kutumiwa na
kifaa hiki, Kiunganishi cha sauti, kuwa makini sana na viwango vya sauti.
Sehemu nyingine za kifaa hiki zina sumaku. Vitu vya chuma vinaweza kuvutwa na kifaa. Usiweke
kadi za mkopo au kadi nyingine zenye mkanda wa sumaku karibu na kifaa kwa kipindi cha muda
mrefu, kwa kuwa kadi hizo zinaweza kuharibika.
INGIZA SIM NA KADI ZA KUMBUKUMBU
Ingiza kadi TA-1495, TA-1505, TA-1521
1. Fungua trei ya SIM kadi: sukuma pini ya kufungua trei ndani ya shimo la trei na uondoe trei.
2. Weka SIM kadi ya nano kwenye kipenyo 1 na aidha SIM ya pili au kadi ya kumbukumbu
kwenye kipenyo 2 kwenye trei eneo la mguso likiangalia chini.
1. Fungua trei ya kadi ya kumbukumbu: sukuma pini ya kufungua trei ndani ya shimo la trei na
uondoe trei.
2. Weka kadi ya kumbukumbu katika kipenyo cha kadi ya kumbukumbu kwenye trei na eneo la
mguso likiangalia chini.
3. Telezesha trei ndani.
Muhimu: Usiondoe kadi ya kumbukumbu wakati programu inaitumia. Kufanya hivyo kunaweza
kuharibu kadi ya kumbukumbu na kuharibu data iliyohifadhiwa kwenye kadi.
Kidokezo: Tumia kadi ya kumbukumbu ya microSD yenye kasi, na ya hadi GB 512 kutoka kwa
mtengenezaji anayefahamika.
1. Chomeka chaja inayotangamana kwenye soketi ya ukuta.
2. Unganisha kebo kwenye kompyuta kibao yako.
Kompyuta kibao yako inakubali kebo ya USB ya C. Pia unaweza kuchaji kompyuta kibao yako
kutoka kwenye kompyuta kwa kutumia kebo ya USB, lakini inaweza kuchukua muda mrefu zaidi.
Kama betri imeisha moto kabisa, huenda ikachukua dakika kadhaa kabla ya kiashiria chaji
kuonyeshwa.
WASHA NA USANIDI KOMPYUTA KIBAO YAKO
Washa kompyuta kibao yako
1. Kuwasha kompyuta kibao yako, bonyeza na ushikilie kitufe cha nishati hadi kompyuta kibao
iwake.
2. Fuata maagizo yalioonyeshwa kwenye skrini.
FUNGA AU FUNGUA KOMPYUTA KIBAO YAKO
Fung vitufe na skrini yako
Ili kufunga vitufe na skrini yako, bonyeza kitufe cha nishati.
Fungua vitufe na skrini
Bonyeza kitufe cha nishati, na utelezeshe juu kwenye skrini. Ukiulizwa, toa hati tambulishi za
ziada.
TUMIA SKRINI YA MGUSO
Muhimu: Epuka kugwara skrini ya mguso. Usitumie kamwe kalamu, penseli halisi, au kitu
Skrini huzunguka kiotomatiki wakati unapindua kompyuta kibao kwa digrii 90.
Kufunga skrini katika hali ya wima, telezesha chini kutoka upande wa juu wa skrini, na uguse
Zungusha kiotomatiki > Zima .
Rambaza kwa kutumia ishara
Kuwasha kwa kutumia urambazaji wa ishara, gusa Mipangilio > Mfumo > Ishara >
Urambazaji wa mfumo > Urambazaji wa ishara .
• Ili kuona programu zako zote, telezesha
juu kutoka kwenye skrini.
• Ili kwenda kwenye skrini ya mwanzo,
telezesha juu kutoka chini ya skrini.
Programu uliyokuwa ukitumia hubakia
imefunguliwa chinichini.
• Kuona programu gani umefungua,
telezesha juu kutoka chini ya skrini bila
kutoa kidole chako hadi uone programu,
kisha uondoe kidole chako.
Rambaza kwa kutumia vitufe
Kuwasha vitufe vya urambazaji, gusa Mipangilio > Mfumo > Ishara > Urambazaji wa mfumo
> Urambazaji wa vitufe 3 .
• Ili kuona programu zako zote, pitisha
juu kwenye kitufe cha mwanzo
.
• Ili kubadilisha kwa programu nyingine
iliyofunguliwa, gusa programu.
• Ili kufunga programu zote zilizofunguliwa,
gusa FUTA ZOTE .
• Ili urudi kwenye skrini ya awali ambayo
ulikuwa unatumia, telezesha kutoka
upande wa kulia au kushoto ya skrini.
Kompyuta kibao yako hukumbuka
programu na tovuti zote ulizotembelea
tangu wakati wa mwisho skrini yako
ilipofungwa.
• Ili kubadilisha kwa programu nyingine
iliyofunguliwa, telezesha kulia na uguse
programu.
• IIi kwenda kwenye skrini ya mwanzo, gusa
kitufe cha mwanzo. Programu uliyokuwa
ukitumia hubakia imefunguliwa chinichini.
• Ili kuona ni programu gani ulizofungua,
gusa .
• Ili kufunga programu zote zilizofunguliwa,
gusa FUTA ZOTE .
• Ili kurejesha kwenye skrini ya awali
uliyokuwa, gusa . Kompyuta kibao yako
hukumbuka programu na tovuti zote
ulizotembelea tangu wakati wa mwisho
skrini yako ilipofungwa.
Nokia T21 Mwongozo wa mtumiaji
3 Linda kompyuta yako kibao
LINDA KOMPYUTA KIBAO YAKO KWA KUFULI YA SKRINI
Unaweza kuweka kompyuta kibao yako kuhitaji uhalalishaji wakati unapofungua skrini.
Weka kufuli ya skrini
1. Gusa Mipangilio > Usalama > Kufuli ya skrini .
2. Chagua aina ya kufuli na ufuate maelekezo kwenye kompyuta kibao yako.
LINDA KOMPYUTA KIBAO YAKO KWA KUTUMIA USO WAKO
Sanidi uhalalishaji wa uso
1. Gusa Mipangilio > Usalama > Fungua kwa kutumia uso .
2. Chagua ni mbinu gani ya hifadhi nakala ya kufungua unayotaka kutumia kwenye skrini ya
kufunga na ufuate maagizo yaliyoonyeshwa kwenye kompyuta kibao yako.
Fungua macho yako na uhakikishe uso wako unaonekana kikamilifu na hujafunikwa na kitu
chochote, kama vile kofia au miwani.
Kumbuka: Kutumia uso wako kufungua kompyuta kibao yako si salama kama kutumia pin au
ruwaza. Huenda kompyuta kibao yako imefunguliwa na mtu au kitu chenye mwonekano huo
mmoja. Huenda kufungua kwa uso kusifanye kazi vizuri katika mazingira yenye mwangaza wa
nyuma au wenye giza au mkali.
Fungua kompyuta kibao yako kwa kutumia uso wako
Ili kufungua kompyuta kibao yako, washa skrini yako na uangalie kamera ya mbele.
Ikiwa kuna hitilafu ya kutambua uso, na huwezi kutumia mbinu mbadala za kuingia ili kurejesha
au kuweka upya kompyuta kibao kwa njia yoyote ile, kompyuta kibao yako itahitaji huduma.
Huenda gharama ya ziada ikatumika, na data yote ya kibinafsi kwenye kompyuta kibao yako
huenda ikafutwa. Kwa maelezo zaidi, wasiliana na kituo cha huduma kilichoidhinishwa kilicho
karibu cha kompyuta kibao yako, au muuzaji wa kompyuta kibao yako.