Usiunganishe kwenye bidhaa ambazo zinaunda ishara ya kutoa, kwa kuwa hii inaweza kuharibu
kifaa. Usiunganishe chanzo chochote cha stima kwenye kiunganisha cha sauti. Ukiunganisha
kifaa chochote cha nje au vifaa vyovyote vya sauti kando na vile vilivyoidhinishwa kutumiwa na
kifaa hiki, Kiunganishi cha sauti, kuwa makini sana na viwango vya sauti.
Sehemu nyingine za kifaa hiki zina sumaku. Vitu vya chuma vinaweza kuvutwa na kifaa. Usiweke
kadi za mkopo au kadi nyingine zenye mkanda wa sumaku karibu na kifaa kwa kipindi cha muda
mrefu, kwa kuwa kadi hizo zinaweza kuharibika.
INGIZA SIM NA KADI ZA KUMBUKUMBU
Ingiza kadi za TA-1457, TA-1462, TA-1503, TA-1512
1. Fungua trei ya SIM kadi: sukuma pini ya kufungua trei ndani ya shimo la trei na uondoe trei.
2. Weka nano-SIM kwenye kipenyo cha SIM kwenye trei na eneo la mguso likiangalia chini.
3. Ikiwa una kadi ya kumbukumbu, ingiza kwenye kipenyo cha kadi ya kumbukumbu.
1. Fungua trei ya kadi ya kumbukumbu: sukuma pini ya kufungua trei ndani ya shimo la trei na
uondoe trei.
2. Weka kadi ya kumbukumbu kwenye kipenyo cha kadi ya kumbukumbu kwenye trei.
3. Telezesha trei ndani.
Muhimu: Usiondoe kadi ya kumbukumbu wakati programu inaitumia. Kufanya hivyo kunaweza
kuharibu kadi ya kumbukumbu na kuharibu data iliyohifadhiwa kwenye kadi.
Kidokezo: Tumia kadi ya kumbukumbu ya microSD yenye kasi, na ya hadi GB 512 kutoka kwa
mtengenezaji anayefahamika.
1. Chomeka chaja inayotangamana kwenye soketi ya ukuta.
2. Unganisha kebo kwenye kompyuta kibao yako.
Kompyuta kibao yako inakubali kebo ya USB ya C. Pia unaweza kuchaji kompyuta kibao yako
kutoka kwenye kompyuta kwa kutumia kebo ya USB, lakini inaweza kuchukua muda mrefu zaidi.
Kama betri imeisha moto kabisa, huenda ikachukua dakika kadhaa kabla ya kiashiria chaji
kuonyeshwa.
WASHA NA USANIDI KOMPYUTA KIBAO YAKO
Washa kompyuta kibao yako
1. Kuwasha kompyuta kibao yako, bonyeza na ushikilie kitufe cha nishati hadi kompyuta kibao
iwake.
2. Fuata maagizo yalioonyeshwa kwenye skrini.
FUNGA AU FUNGUA KOMPYUTA KIBAO YAKO
Fung vitufe na skrini yako
Ili kufunga vitufe na skrini yako, bonyeza kitufe cha nishati.
Fungua vitufe na skrini
Bonyeza kitufe cha nishati, na utelezeshe juu kwenye skrini. Ukiulizwa, toa hati tambulishi za
ziada.
TUMIA SKRINI YA MGUSO
Muhimu: Epuka kugwara skrini ya mguso. Usitumie kamwe kalamu, penseli halisi, au kitu
Skrini huzunguka kiotomatiki wakati unapindua kompyuta kibao kwa digrii 90.
Kufunga skrini katika hali ya wima, telezesha chini kutoka upande wa juu wa skrini, na uguse
Zungusha kiotomatiki > Zima .
Rambaza kwa kutumia ishara
Kuwasha kwa kutumia urambazaji wa ishara, gusa Mipangilio > Mfumo > Ishara >
Urambazaji wa mfumo > Urambazaji wa ishara .
• Ili kuona programu zako zote, telezesha
juu kutoka kwenye skrini.
• Ili kwenda kwenye skrini ya mwanzo,
telezesha juu kutoka chini ya skrini.
Programu uliyokuwa ukitumia hubakia
imefunguliwa chinichini.
• Kuona programu gani umefungua,
telezesha juu kutoka chini ya skrini bila
kutoa kidole chako hadi uone programu,
kisha uondoe kidole chako.
Rambaza kwa kutumia vitufe
Kuwasha vitufe vya urambazaji, gusa Mipangilio > Mfumo > Ishara > Urambazaji wa mfumo
> Urambazaji wa vitufe 3 .
• Ili kuona programu zako zote, pitisha
juu kwenye kitufe cha mwanzo
.
• Ili kubadilisha kwa programu nyingine
iliyofunguliwa, gusa programu.
• Ili kufunga programu zote zilizofunguliwa,
gusa FUTA ZOTE .
• Ili urudi kwenye skrini ya awali ambayo
ulikuwa unatumia, telezesha kutoka
upande wa kulia au kushoto ya skrini.
Kompyuta kibao yako hukumbuka
programu na tovuti zote ulizotembelea
tangu wakati wa mwisho skrini yako
ilipofungwa.
• Ili kubadilisha kwa programu nyingine
iliyofunguliwa, telezesha kulia na uguse
programu.
• IIi kwenda kwenye skrini ya mwanzo, gusa
kitufe cha mwanzo. Programu uliyokuwa
ukitumia hubakia imefunguliwa chinichini.
• Ili kuona ni programu gani ulizofungua,
gusa .
• Ili kufunga programu zote zilizofunguliwa,
gusa FUTA ZOTE .
• Ili kurejesha kwenye skrini ya awali
uliyokuwa, gusa . Kompyuta kibao yako
hukumbuka programu na tovuti zote
ulizotembelea tangu wakati wa mwisho
skrini yako ilipofungwa.
Loading...
+ 25 hidden pages
You need points to download manuals.
1 point = 1 manual.
You can buy points or you can get point for every manual you upload.